Naona kama mabinti waliohitimu vyuo wanakabiliana vizuri na changamoto ya ajira kuliko vijana wa kiume

Unasoma mpaka university ili ule uuze chipsi? Shame Nikola Tesla alipoacha ajira yake kutoka kwa Thomas edison alienda kufanya hizi kazi zenu hizi sasa yeye alikuwa anasafisha vyoo yaani topaz alipoona potential aliyokuwa nayo akaamua kuacha upuuzi wa kuchimba vyoo.

Na mpaka sasa ana jina kubwa tu , ila hayo yoote yaliwezekana kwa sababu kwanza ana potential pili alipata wa kum backup , ni ujinga mkubwa serikali kusomesha wataalamu halafu wakakosa ajira ,kwa kiwango kikubwa tu hizo hela za mikopo kwanini wasingeliziongezea kwenye miradi mingine?
 
Wanawake tumeamua kuchakarika na kila shughuli ukitafta hela hamna kuona aibu. Tena tumejiunga na vikundi tunacheza na michezo hatutaki utani maisha yetu wanawake tusipofanya kazi tutakuwa jamvi la wageni.

Vicoba hoyeee, siku hizi wanawake ni watafutaji kuliko me
 
Kwanza wanamaliza wachache kuliko wakiume, baadhi wakishamaliza tu chuo huolewa, na cha mwisho nikuwa kainachofanya mpka wana drive sio huto tubiashara nyuma yao kuna mabosi wakubwa. Anyway umesema tafiti ya juu juu ko hakuna haja yakutoa majibu ya chini chini sana.
 
Kuna binti namfahamu ni best yawa mpenzi wangu walimaliza chuo wote mwaka mmoja na chuo kimoja ,kozi moja...Manzi yangu alibahatika kupata kazi mwenzie akabaki mtaani kwa mudabaadae akaamua auze nguo alianza kama utani na mimi mwanzoni nilivaa sana nguo zake za mtumba kwa sasa ana duka ni miaka 3 tu imepita na anajitegemea na maisha yanaenda.
Safi sana
 
Unasoma mpaka university ili ule uuze chipsi? Shame Nikola Tesla alipoacha ajira yake kutoka kwa Thomas edison alienda kufanya hizi kazi zenu hizi sasa yeye alikuwa anasafisha vyoo yaani topaz alipoona potential aliyokuwa nayo akaamua kuacha upuuzi wa kuchimba vyoo.

Na mpaka sasa ana jina kubwa tu , ila hayo yoote yaliwezekana kwa sababu kwanza ana potential pili alipata wa kum backup , ni ujinga mkubwa serikali kusomesha wataalamu halafu wakakosa ajira ,kwa kiwango kikubwa tu hizo hela za mikopo kwanini wasingeliziongezea kwenye miradi mingine?
Kazi ya chips na mishkaki unaweza kuifanya na ikakuingizia kipato kikubwa na kukupa heshima kuliko kazi ya ofisini. Unaweza fungua barbershop ya mtaani tu na ukaiendesha kisomi kiasi kwamba ukaheshimika na ukapata kipato.
 
Yani na degree yangu nichome mishikaki mkuu?
Mkuu hakuna namna toka hapo ulipo uchakarike

Kaka yangu alimaliza chuo 2011 kipindi hicho ifm pale Information Technology huwezi amini alifungua duka la kushona viatu vya kimasai pale Kigamboni mji mwema

Wazungu wakienda beach wananunua, watz nao hawakua nyuma akapata wateja wengi sana

Kuna siku akikuja mteja pale ndo akamuunganisha kazi Jpaego sijui kama nimepatia hilo jina ila wanahusika na mambo ya takwimu hasa ukimwi , Malaria n.k

Duka baadae lilikufa baada ya kumuachia kijana mwingine ila nakushauri tuu toka hapo ulipo anza kufanya chochote mkuu, siku moja utapata kazi ya ndoto yako.

Binafsi nilipata bahati sikukaa sana mtaani, ndani ya wiki 3 baada ya kumaliza nikaanza kazi ila kaka yangu alisota sana mpaka tulifanya visomo kwamba amerogwa.

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Mabinti gani unaongelea wewe? hawa wanaodanga au?

Maana vijana wa kiume daily wanachakarika ili wasililale njaa lakini upande wa pili ni majanga tupu
 
Wanawake wa sikubizi siyo wale wa karne ya 20

Nafikiri tumewezeshwa sana nguvunkubwa imewekwa kwetu kupitia seminar na makongamano, kwa kifupi ni kwamba nguvu kubwa imewekwa kutengeneza mwanamke

Siku izi wanawake tunacheza vikoba hata vitano kwa wakati mmoja juzi mwezi wa 12 kuna mwenzetu kavunja vikoba vyake kadhaa kapokea milion 40 kwa pamoja

Vijana wa kiume ni mabishoo wakishapata degree wanaona wamewin life anazunguka na baasha miaka nenda rudi huku
Badilikeni
 
Hali hii imesababisha ongezeko la ving'asti wengi mjini;

Sisi tunawashukuru sana, sisi wazembe sasa kazi yetu imekuwa kwenda GYM kujaza body, kuwavutia zaidi.
Mkuu mwanamke anayetafta hela ngumu kuhangaika na body builder Bora kukutana na mtu mwenye akili ya maisha
 
Back
Top Bottom