Naona kama mabinti waliohitimu vyuo wanakabiliana vizuri na changamoto ya ajira kuliko vijana wa kiume

Waachaaa... Naona mada imekugusa kweli.
Imenifuraisha wanawake tumeamka ukiwa na hela yako ndogo Raha sio mpaka mtu akuzalilishe utu wako kisa shida si Bora uuze Chip's kwa Raha zako, wanaume wenyewe hata kununulia magelo friend wenu chupi hamuwezi. Wanawake tukiwa na uchumi imara na dhambi nyingi zinatutoka
 
Vicoba hoyeee, siku hizi wanawake ni watafutaji kuliko me
Kwa kweli tumeamka ujue kuomba hela ni utumwa mpaka tutoe kipochi manyoya tumegoma kabisa. Vikundi vya vicoba vinatusaidia sana
 
Imenifuraisha wanawake tumeamka ukiwa na hela yako ndogo Raha sio mpaka mtu akuzalilishe utu wako kisa shida si Bora uuze Chip's kwa Raha zako, wanaume wenyewe hata kununulia magelo friend wenu chupi hamuwezi. Wanawake tukiwa na uchumi imara na dhambi nyingi zinatutoka
Sio kwamba hatupendi mtafute na kuzipata pesa. Wengi mkipata vihela mnajawa na kiburi na kuutaka ukichwa wa familia. Mkiwa na vipesa mnaota vimapembe kama mbuzi ndio shida.
 
Yani na degree yangu nichome mishikaki mkuu?
Kuna co-relation ya degree na mishikaki? Kazi yeyote ukiwa binadamu unaweza kuifanya. Au wanaochoma mishikaki ni nusu binadamu nusu wadudu? Ukiwa na degree unakuwa super human?

Tulitarajia kwa sababu wewe ni mhitimu wa shahada utafute namna bora ya kuchoma mishikaki kisomi na sio kuona degree kama inakufanya binadamu na nusu!
 
Sio kwamba hatupendi mtafute na kuzipata pesa. Wengi mkipata vihela mnajawa na kiburi na kuutaka ukichwa wa familia. Mkiwa na vipesa mnaota vimapembe kama mbuzi ndio shida.
Sio kwamba tunataka kichwa Cha familia vile hela huongeza confidence na nyie huji feel inferior tu. So nawasisitiza wanawake tutafte hela KWA bidii, changamoto nyingi zetu wanawake ni uchumi, ukiwa na uchumi hata mda mchafu wa kuhangaika na mume na michepuko unakuwa huna, na dhambi na maumivu ya moyo yanaisha
 
NAUNGA MKONO HOJA.

Kuna moja anauza karanga hiz za mayai juzi alikuwa ananicheki kama huku mkoa nilipo naweza mtaftia wateja wa kujumua.

Mwengine yupo anapika nyumbani kwao ikifika mchana anapakia kwene bajaji anaenda kuuza kwenye frem yake

Mwengine anasambaza juisi

Mwengine anatengeneza keki

Mwengine yupo anajitolea kazi tangu mwaka jana, saizi anapewa 300,000 kila mwezi kwa kujitolea,

Mifano ni mingi jamani, na kwa wanaume huku sio kwamba hawapo wasiojisguguliisha, wapo lakini hawafikii uwiano wa wanawake, wengi huishia kuwa meme lords mitandaoni (watunga vituko / memes), kucheza ps muda mwingi, kubeti, kutumia muda mwingi kuwapa mimba mabinti na kuwakimbia, kuanza kuvuta bangi, kunywa pombe, n.k huku wakiwa wanasingizia kwamba wana apply kila siku kazi na jusubiri interview.

Watoto wa kiume amkeni, Mtoa maada asante kwa kuweka hii maada, kumbe ni wengi tunayaona haya
 
Sio kwamba tunataka kichwa Cha familia vile hela huongeza confidence na nyie huji feel inferior tu. So nawasisitiza wanawake tutafte hela KWA bidii, changamoto nyingi zetu wanawake ni uchumi, ukiwa na uchumi hata mda mchafu wa kuhangaika na mume na michepuko unakuwa huna, na dhambi na maumivu ya moyo yanaisha
Ke akishakuwa na visenti vyake anahitaji kuwa na busara sana kuishi na Me aliyemzidi kipato.
 
Acheni kulaumu vijana,

Hakuna kijana mwenye akili timamu anayekataa kufanya kazi ndogondogo.

Hivi unakuta Dada pisi Kali ya maana inauza uji jioni au hereni kwenye baa, na wewe kweli unasema anauza uji.

Jiongeze hiyo ni njia mpya ya kudanga.
 
Ke akishakuwa na visenti vyake anahitaji kuwa na busara sana kuishi na Me aliyemzidi kipato.
Wala wanawake huwa hatuna shida ni nyie tu, Mimi siwezi acha tafta hela nitoke kwa umaskini eti kisa mwanaume atanionaje, nikiwa na hela nitalipa Ada za watoto, watakula vzuri ujue umaskini sio jambo zuri kabisa ni laana ile.
 
Ok, tafuta pesa ila pia baki mtiifu.😀
Sio ndio kufanya chochote kisa unaweza ishi mwenyewe.
 
Wakiume akjaribu biashara hzo anafirisika mapema tu,maana hana pakurudishia
 
Hii ni kitu nimeiona baada ya kufanya utafiti wa kijuu juu. Nimeona mabinti wengi wanachakarika na ujasiriamali.

Ninekutana na wahitimu wa vyuo ambao ni mama ntilie. Wanapiga umachinga mdogomdogo wa nguo za kike, juice, viatu nk. Pia wamekuwa mstari wa mbele kuhudhuria mafunzo ya ujasiriamali kama kutengeneza sabuni nk.

Imekuwa kazi sana kumkuta mhitimu wa kiume akifanya hizi ishu ndogondogo kama kuchoma chips na mishkaki. Nini shida kwa vijana wakiume kuingia kwenye sekta isiyo rasmi baada ya kumaliza chuo?

Rai yangu, Serikali ijitahidi kwa nguvu zote kuweka mazingira ya vijana kuweza kujiajiri.
KATIKA MAZINGIRA YETU SISI WATANZANIA, MWANAMKE AKIFANYA HIZO BIASHARA NDOGO NDOGO NI RAHISI KUPATA WATEJA KULIKO SISI WANAUME. MFANO MWANAMKE AKIUZA JUISI AU UJI NA CHAI NI RAHISI ZAIDI VIJANA WA KIUME KUMUUNGISHA KULIKO AKIUZA HIVYO VITU MWANAUME MWENZAO NA HII IPO WAZI HATA BAR INAYOUZWA NA WANAWAKE NI RAHISI KUJAA WATEJA KULIKO ANAYOUZA MWANAUME.
KWANZA MWANAUME UKIFANYA BIASHARA HIZO UTAISHIA KUFILISIKA KWA KUKOPWA NA MASELA AMBAO HAWALIPAGI MADENI.
 
Wanaume busy na online opportunities... Busy na forex,cryptoz na kubet... Wanamawazo ya kutoboa pakubwa bila kujua ndo wanapoteza muda zaid.
keep it up ladies
 
Endelea kukaa na kula kwa shemeji.Ipo siku utaombwa visivyoombwa.
Jiongeze jombaa!
Hizo kazi za uchuuzi bora ningezianzaga miaka 16/ uko nyuma baada ya Mimi kumaliza la saba.

Alafu Leo hutalala usingizi mzuri lazima usiku nikuijie, unaniambia nakaa kwa shemeji,

Nipo nachanja watu chale na kupiga vibuyu
 
Mkuu hakuna namna toka hapo ulipo uchakarike

Kaka yangu alimaliza chuo 2011 kipindi hicho ifm pale Information Technology huwezi amini alifungua duka la kushona viatu vya kimasai pale Kigamboni mji mwema

Wazungu wakienda beach wananunua, watz nao hawakua nyuma akapata wateja wengi sana

Kuna siku akikuja mteja pale ndo akamuunganisha kazi Jpaego sijui kama nimepatia hilo jina ila wanahusika na mambo ya takwimu hasa ukimwi , Malaria n.k

Duka baadae lilikufa baada ya kumuachia kijana mwingine ila nakushauri tuu toka hapo ulipo anza kufanya chochote mkuu, siku moja utapata kazi ya ndoto yako.

Binafsi nilipata bahati sikukaa sana mtaani, ndani ya wiki 3 baada ya kumaliza nikaanza kazi ila kaka yangu alisota sana mpaka tulifanya visomo kwamba amerogwa.

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
Hongera sana mkuu wiki tatu kitaa ukalamba shavu.

Maoni mazuri hata ivo na mpango wa kuwa konda wa daladala nimeanza taratibu.
(Simu 2000_makumbusho)
 
Back
Top Bottom