Naona kama kupata hati pengine ni suala la wachache hapa nchini

Jul 25, 2020
65
125
Wadau Naombeni msaada kidogo pengine hapa naweza kusaidiwa hata mawazo, hili jambo limenitesa sana nimekuwa nikifuatilia kupata hati ya eneo langu ambalo limepimwa na nimelipia kila kitu na risiti ninazo ila changamoto nilizokutana nazo mpaka nafanikiwa kupata invoice ya kwenda kulipia na kupata michoro ya hati hazielezeki Naona kama kupata hati pengine ni swala la wachache hapa nchini maana licha ya kulipia bado ninaona kama ndoto kuwa ntapata hati na pia kibali cha ujenzi.

Lakini licha ya kulipia ila mpaka nafuatilia ni mwaka mzima unaisha na kila ukienda hata kama uende kila siku utakayoambiwa uende basi ni kalenda zile zile wiki mpaka miezi njoo kesho bado nina kazi zingine kibao kama unavoziona haya ndio maneno huwa tunaambiwa mara kwa mara, na maneno kama subiri au njoo tena jumatatu ijayo.

Kinachoniuma ni kuona alonikuta nahangaikia hati nusu mwaka unakaribia kuisha nasikia watu wakiteta pembeni kuwa yeye kapata hati yake pale pale ndani ya siku 2 ambapo mi nimeambiwa subiri nusu mwaka. Hivi hili likoje na wengine wanafanyaje mpaka wanapata ndani ya wiki moja wakati mwingine nusu mwaka unaambiwa subiri asaini.

shida yangu kubwa nayopitia hapa kama kijana mjini ni kutaka kujenga na mjini siwezi kujenga bila kibali sijui au hati ya kiwanja chako, pili najua ni taaluma za watu ila pia ni changamoto kubwa kwangu kuambiwa ramani ya nyumba lazima ninunue kwa alosomea ili waipitishe ninatakiwa lipia hela kibao la sivyo sijengi, jamani hili linaumiza sana kwanini wasiniruhusu nikajenga au wanisaidie bure kuwa ukijenga nyumba hakikisha iwe na vigezo hiki na hiki kuliko huu mlolongo mkubwa sana ambao vijana wa mjini unatumiza sana.

kama kuna anayeweza nitumie ramani yake ya nyumba ambayo alishajenga na hana kazi nayo tena ilokamilika vyumba vitatu na fensi ili watu wa jiji wakaipitishe yoyote maana mi sijui kuchora nimesomea BAPA chenga tu Kichwani naomba nitumie kwa inbobo niwapelekee msaada wakubwa tusinyimane SINA HELA ila angalau nikipata hati miliki haraka nitaomba kibali cha ujenzi ili hata kama siwezi jenga nyumba kubwa nisimamishe hata chumba kimoja nihamie kwangu.

NAOMBENI USHAURI NIFANYEJE ILI NIPATE HATI HARAKA MAANA NAENDA KILA SIKU NAAMBIWA SUBIRI NI NUSU MWAKA SASA HAKUNA HATA DALILI TUAMBIANE UKWELI.
 
Tatizo kubwa ni watu kutaka pesa kwanza kana kwamba ndio kitendea kazi.

Wivu usio na tija, akiona unafuatilia hati, anaona una hela na ni haki yake kupata sehemu ya hela hiyo.

Ni kama unapoenda polisi kutaka mchoro wa ajali kwaajili ya bima, anaanza kukwambia, unaenda kulipwa ela nyingi ujue, so what?
 
Back
Top Bottom