Mkoroshokigoli
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 14,593
- 5,587
Wewe mnafiki tu siamin kama umesoma Mzumbe na lengo lako ni kuchafua chuo na watu wa IT wa Mzumbe wapo wafuatilie kwa ukaribu watu wa namna hii maana wanaharibu kwa kueneza uvumi ambao hauna ushahidi. Ungeleta cheti chako hadharani na kusema ulivyokipata ungekuwa wa maana lakin kujificha na kusema bila kuthibitisha unayoyasema na unataka tuamini ya moyoni mwako ni unafki. Kila mwanafunzi anajuhudi zake binafsi katika kufikia malengo kutegemeana na uwezo wake kichwani. Kama una akili za kufanya kazi usingekubali kufanyiwa bali kwa vile kilaza unasema hadharani udhaifu wako. Walimu pia ni binadamu wanapoamua kukusaidia ili umalize kazi yako ujue wewe mwenyewe ulionekana unamatatizo ya kiakili juu ya kazi yako bora wakusaidie uondoke ukajue na mwajiri wako. Maana kama wamekusaidia na kisha shukrani yako kwao ni kuwasema vibaya jua wewe akili yako ni mbovu! Je unataka wanafunzi wengine vilaza wasisaidiwe na wao wamalize kama wewe? Kama una akili nzuri kitupe hicho cheti hadharan na ukatafute MBA coorperate nyingine kama utaweza!!! Na hii inaonesha wewe una akili mbovu na kisha una roho mbaya kiasi ambacho ukimwoona mwenzako ana elimu kama yako unatamani afe ubaki wewe duniani na kama roho yako ingekuwa na ncha kali ungetumia kuwachoma washindani wako ili wafe. Acha roho mbaya mwombe Allah akupe roho yenye kutulizana na kuridhika na akuepushe na unafiki na pia akupe uwezo wa kutafakari unayoandika mtandaoni yawe na manufaa kwa jamii na si kuharibu na kubomoa kama uwezo wako ulivyo sasa.
'Usiusemee Moyo'-LADY JAY DEE