Naombeni ushauri wenu kwenye hili tafadhali.....

Naombeni ushauri wenu kwenye hili tafadhali.....

Rafiki yangu,
Pombe,Bangi,Sigara,Shisha na Starehe yoyote ile ambayo ni Addictive kwa Umri wako huo Ni hatari.Usidnagnyike wanaposema hairuhusiwi kwa wenye umri wa miaka 18 ukafikiri kwa sababu una 19 unaruhusiwa.

Ushauri wangu kama Unaweza kuamua kwamba maisha yako yote hutatumia hivo vitu basi Usijaribu.Watu wametumia vyote na hakuna walichopata.Kama ni kuhusu Starehe ziko nyingi sana.Hata kula Mlo mzuri sehemu nzuri,Kulala sehemu nzuri,kutembelea sehemu nzuri zilizotulia,kujifunza vitu vipaya kama Computer Programming,Kusoma Vitabu,Kuandika vitabu na machapisho JF vyote unaweza kuvifanya Starehe na Niamni nikikwambia kwamba Ni starehe nzuri zaidi kuliko Hizo nilizotaja hapo JUU

Hizo hapo juu ni starehe za watu ambao wako Frustrated na Maisha na kwa Umri wako bado hujawa Frustrated ili Utakapofikia hatua ya kuwa Frustrated Hutakuja huku kutuuliza bali utachagua moja na ndio itakuwa anguko lako
 
at 19 years unakunywa pombe n bangi ??/Asee wazazi wako wakogo wapi wanakupoteza

Wenzako at 19 tuko vyuo vikuu tunasaka degrees wewe uko bize na bangi asee😂😂😂 kwakweli tunatofautiana vipaumbele


Anyway badilisha marafiki huko mnakoelekea sio kuzuri, starehe gharama
 
Back
Top Bottom