mshamba_hachekwi
JF-Expert Member
- Mar 3, 2023
- 16,797
- 51,966
Mimi ni kijana mdogo wa miaka 19. Hivi karibuni nimekua nikipatwa na msukumo mkubwa wa kunywa pombe na kuvuta bangi. Kusema kweli najaribu sana kujizuia, lakini naona kama hizi jitihada zangu hazitozaa matunda.....
Kwa muda mrefu sasa, marafiki zangu nawaona wanachukulia hii ishu kawaida sana..... Tukiwa kwenye mitoko, hawawezi acha kulewa ovyo, kuvuta bangi na shisha, na ku-vape. Kwa mtazamo wao, ni kitu cha kawaida sana, na wanaona kama hakuna madhara yoyote yanaweza kutokea. Wanasema 'wanakula ujana', 'wanamwagilia moyo'.....
Miaka mingi sasa tumekua tukiishi haya maisha.... kwenda maclub weekend na 'kula bata'. Mimi nimekua nikijizuia mno...... nazugazuga chupa moja nainya hata masaa 2-3.....
Unaweza sema niko kwenye makundi mabaya, lakini mimi sioni hivyo.... hawa ni marafiki zangu wa muda mrefu, tumekua tukisaidiana sana, sema hapo kwenye mambo ya starehe ndo tunatofautiana.....
Pia ndugu, ukizingatia kwamba mimi ni mchaga(kote upande wa baba na mama), wanatumia sana haya mazaga na wamekua wakinishawishi sana, na hata wengine kuonyesha dharau.... Nakumbuka kuna siku nilitoka na bamkubwa nikakataa kunywa pombe.... alicheka sana na kunishangaa.....
Najua wengine mnaweza sema hakuna shida yeyote kwenye kutumia kidogo, lakini kama nilivosema..... mimi ni kijana mdogo, bado maisha yangu ni marahisi, nategemea wazazi, hivyo bado nina ndoto za kufanya vitu vikubwa na maisha yangu, hivyo naogopa sana pombe na bangi vitanirudisha nyuma. Nimeona watu wengi wakiharibikiwa kwasababu ya pombe na bangi....
Najua humu JF watu wazima mko wengi, naomba mnishauri..... Kuna namna ya kubalance maisha ya kawaida na hizi starehe?? Au niendelee kukaa navyo mbali.... na ikiwa hivyo, nitumie mbinu gani??