Naombeni msaada wenu, Kila mwaka inabidi niende TRA kufanyiwa makadirio ya duka?

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,080
Habari zenu jukwaa la biashara, nina duka nilifungua mwaka jana kuna rafiki alinisaidia kukata vibali vya TRA ila kwa sasa hayupo.

Mwaka jana nilihusika tu kwenye kulipia zile kodi za kila baada ya miezi mitatu.

Sasa kwa mwaka huu nimejuzwa kwamba inabidi niende kufanyiwa makadirio upya.

Je, ni vitu gani nahitaji kwenda kufanyiwa makadirio?

Ninapewa kitu gani nikishakadiriwa kiwe ushahidi?

Kuna mambo yapi ya ziada inabidi nizingatie?
 
Usiwape mwanya TRA wakukadirie. Kama hakuna mabadiliko makubwa kibiashara ni bora ukawaomba wakutolee control number tu zile za kulipa kwa awamu.
 
Je unatumia mashine ya efd? Na kama unatumia efd na mgeni kuitumia kuwa makini kuandika usikosee badala ya 200,000 ukaandika 2,000,000 kitakulamba, TRA ukiandika risiti nyingi ni shida na usipotoa risit ni shida
situmii masgine ya efd, natumia kitabu cha kawaida
 
Usiwape mwanya TRA wakukadirie. Kama hakuna mabadiliko makubwa kibiashara ni bora ukawaomba wakutolee control number tu zile za kulipa kwa awamu.
Mkuu, kwa meseji wanazotutumia ni kwamba ukikwepa kukadiriwa kuna adhabu ya riba.
 
Habari zenu jukwaa la biashara, nina duka nilifungua mwaka jana kuna rafiki alinisaidia kukata vibali vya TRA ila kwa sasa hayupo.

Mwaka jana nilihusika tu kwenye kulipia zile kodi za kila baada ya miezi mitatu.

Sasa kwa mwaka huu nimejuzwa kwamba inabidi niende kufanyiwa makadirio upya.

Je, ni vitu gani nahitaji kwenda kufanyiwa makadirio ?

Ninapewa kitu gani nikishakadiriwa kiwe ushahidi ?

Kuna mambo yapi ya ziada inabidi nizingatie ?
nasikia harufu ......... na sikia milio ya madufu.
tafuta muhasibu wako wewe huko wanataka wakule pesa zako .hii code ndio tunatumia hata mfano kesi zilizopo polisi anayetakiwa ni mwanasheria kuwa mbele sio wewe.
na tra ni mtu mwenye kujua uzoefu na elimu ya kodi ambaye nimwasibu wako
 
Naomba ufafanuzi juu ya hili hata mtu asipo kuwa VAT anaruhusiwa kuwa na muhasibu?
 
situmii masgine ya efd, natumia kitabu cha kawaida
Kimsingi hutoi risiti. Kitabu cha kawaida hakitumiki Tanzania. Tena usije ukawaambia unatumia risiti za kitabu utawatia hasira wakulime adhabu. Wewe fika TRA mwambie ofisa kuwa umekuja unataka Tax clearance. Ukimwambia hivyo atacheki faili lako jinsi ulivyokuwa ukilipa na kukuuliza hali ya biashara. Kama atakuongezea kiasi cha kulipa atakuuliza kwanza kabla ya kufanya hivyo. TRA ni wabaya sana kama ukiwakwepa halafu wakakugundua na kukufuatilia. Ila ukienda mapema mnaongea fresh na kuyajenga
 
Na je kama nililipia Mwanzo then biashara ikanishinda? Natakiwa kwenda kuifunga?
Na kama nime delay labda miaka miwili madhara yake ninini?
 
Kimsingi hutoi risiti. Kitabu cha kawaida hakitumiki Tanzania. Tena usije ukawaambia unatumia risiti za kitabu utawatia hasira wakulime adhabu. Wewe fika TRA mwambie ofisa kuwa umekuja unataka Tax clearance. Ukimwambia hivyo atacheki faili lako jinsi ulivyokuwa ukilipa na kukuuliza hali ya biashara. Kama atakuongezea kiasi cha kulipa atakuuliza kwanza kabla ya kufanya hivyo. TRA ni wabaya sana kama ukiwakwepa halafu wakakugundua na kukufuatilia. Ila ukienda mapema mnaongea fresh na kuyajenga
asante sana kwa ushauri, maana nilipanga niende kabisa na kitabu cha risiti.

nilidhani tax clearance unapewaga ukianza tu biashara kumbe nayo ni kila mwaka.
 
Habari zenu jukwaa la biashara, nina duka nilifungua mwaka jana kuna rafiki alinisaidia kukata vibali vya TRA ila kwa sasa hayupo.

Mwaka jana nilihusika tu kwenye kulipia zile kodi za kila baada ya miezi mitatu.

Sasa kwa mwaka huu nimejuzwa kwamba inabidi niende kufanyiwa makadirio upya.

Je, ni vitu gani nahitaji kwenda kufanyiwa makadirio ?

Ninapewa kitu gani nikishakadiriwa kiwe ushahidi ?

Kuna mambo yapi ya ziada inabidi nizingatie ?
ushauri wangu ni kweli kila mwaka wanasema kuanzia januari mpaka mwezi wa tatu unatakiwa uende wakukadirie na cha msingi kama huna efd nenda na kitabu chako cha risiti ili wakikukadiria zaidi iwe utetezi wako jinsi biashara ilivyoenda. pia usisahau mkataba wako wa kupanga fremu kama umepanga kama ni eneo lako basi kithibitisho kama vile risiti ya kulipia jengo hilo au hati ya kumiliki. kama unatumia efd basi wao ni rahisi kujua mwenendo wa bishara yako utabakia na mkataba au uthibitisho wa umiliki wa fremu yako.
 
Naomba ufafanuzi juu ya hili hata mtu asipo kuwa VAT anaruhusiwa kuwa na muhasibu?
kuwa na muhasibu hata kama ni mfanyabiashara mdogo hakuna sehemu ninavyojua mimi pamekatazwa sema ni garama kwa mfanyabiashara mchanga ndiyo maana huwa tunawekewa makadirio fixed kulingana na mauzo ghafi. pia ukiwa huna VAT unaweza kujikuta unalazimika kuwa na muhasibu kwani kuna bidhaa ambazo unaweza kuwa unazuza na kununua hazina VAT ambapo utahitajika kuonyesha mahesabu na pengine biashara yako tayari imevuka milioni 100 ambapo kisheria wanatuambia tunatakiwa kutengeneza mahesabu. Nipo tayari kukosolewa kama ntakuwa nimekosea ila ndivyo navyoelewa
 
VAT registration threshold ni 200mil kwa sasa.
 
Habari zenu jukwaa la biashara, nina duka nilifungua mwaka jana kuna rafiki alinisaidia kukata vibali vya TRA ila kwa sasa hayupo.

Mwaka jana nilihusika tu kwenye kulipia zile kodi za kila baada ya miezi mitatu.

Sasa kwa mwaka huu nimejuzwa kwamba inabidi niende kufanyiwa makadirio upya.

Je, ni vitu gani nahitaji kwenda kufanyiwa makadirio ?

Ninapewa kitu gani nikishakadiriwa kiwe ushahidi ?

Kuna mambo yapi ya ziada inabidi nizingatie ?
Wewe inaonekana NI mchanga Sana kwenye biashara na usipokuwa Makini utapigwa na matapeli,
Kingine inaonekana Una hofu Sana unavyosikia kitu kinaitwa TRA

Utaratbu NI kwamba biashara yoyote inabid ulipe Kodi , na kila mwaka inabid uende ofis za TRA Kwa ajili ya makadirio yako ya Kodi na unatakiwa ulipe ,
Usiogope nenda kakadiriwe uzuri wake kuna unalipa kwa awamu NNE
 
Back
Top Bottom