Lancashire
JF-Expert Member
- Sep 20, 2014
- 14,082
- 10,454
Mke ni malkia katika uislam.Dada yangu alidondoka hapo ! Mambo yakuendekeza Moyo kuliko facts. Maisha ya kiislam ili uyaweze lazima uukubali uislam! Bila kuukubali hutaweza kuendana nao.
Ni hivi dada alikacha familia akaslim sio kwamba aliukubali uislam ila alifanya ili asitengane na ampendaye! Akaolewa, Maisha yanaanza mama wa kiislam! Mziki hauchezeki, masharti hayabebeki, Shemeji mstaarabu ila ndio anasisitiza mkewe lazima aishi kiislam, Dada anajitahidi lakini kwa sababu sivyo alivyokuzwa ni mateso!
Hapo hakuongezewa mke -angezimia kabisa. Alivumilia lakini alishindwa.
Kama unadhani unaweza kuvaa viatu vya mke kwa maadili ya kiislam sawa. Kama huwezi wakati ni sasa ! Chukua hatua
Sent from my SM-J200H using JamiiForums mobile app