emt45
JF-Expert Member
- Jan 19, 2017
- 564
- 644
Kwangu Dini na Dhehebu ndiyo kigezo cha KwanzaWasalaam wana JF, mimi binti Nina tarajia kuwa tabibu hivi karibuni. Ila Nina tatizo Fulani, nina mchumba muislam na mimi ni mlokole, tunapendana sana lakini wachungaji wangu hawamtaki kabisaaa.
Nachanganyikiwa wanadai nimuache, tutafanya maombi nitapata mlokole mwenzangu wananiambia biblia inasema "msifungiwe NIRA na MTU asiyeamini" na MTU asiyeamini ni yule ambaye hajampokea YESU kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake na haamini kifo cha msalaba, ila wazazi wetu wote hawanashida sasa nifanyeje niko njia panda.
Kama nimekosea undishi mnisamehe sana naombeni mchango wenu
Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using JamiiForums mobile app
NB. Huyu mtu nimeanza mahusiano nae kabla sijaokoka na nimeokoka ukubwani
Siyo lazma wewe ubadili dini au wewe ubadili dini kama mmoja hajaridhia mwenyewe
Nina imani hata mkiachana Huko kanisani utapata Mme na Yeye huko Msikitini atapata Mke
Haya Makanisa ya Kilokole na Jamii husika huwa Wanatowa adhabu ya Kumtenga Mfuasi wao kama tu
i.akipata mimba kabla ya ndoa
ii.akiolewa uislamu
iii.wanaingilia sana familiya yako ,yani kama wewe binti umeolewa na Mme wa dhehebu kama RCC ,AC na KKKT .
Lakini Pia ktk upande wetu wa pili sisi Muslim's tunamini asiye amini na kuwa Muslim basi yeye si Msafi na ni Khafiri
Sasa ikitokea umeowa binti wa kilokole lazma jamii yako husika itakupa maana umeowa Khafiri , kwa hiyo lazma aslimishwe ili maadili ya Uislam yakamilike
Je Yule binti alikotoka ktk jamii yake mwanamchukuliaje ?
Mimi binafsi naona tusijiendekeze sana kusema dini siyo kigezo , kiukweli kuishi dini tofauti kuna changamoto kubwa japo hata mkiwa dini moja napo kuna changamoto ila naomba uhamini zimetofautiana .
( ni mawazo yangu na si mawazo ya kiitikadi ya udini )
Sent from my itel it1556 Plus using JamiiForums mobile app