Naombeni msaada, nahisi kukata tamaa ya maisha

Naombeni msaada, nahisi kukata tamaa ya maisha

waza zaidi kipato...unaweza kuolewa alafu ukawa huna ajira gubu za mume zikaanza unapewa hela ya mawazooo aise inaboa..mcheki mjamaa m1 hussein huenda akakuvusha...
ila my dear usibague kazi..nakuomba sana sana....
nikupe mfano hai halisia...kuna siku 2 sikwenda kazini nilikuwa mgonjwa...basi kwa jirani yangu kukaanza ujenzi wa msingi..saa1usk ndo niliona msingi unajengwa baada ya mm kutoka nje..eti nikajikuta nimeenda kuongea na mafundi..nikajikuta nawauliza mnakula wapi?wakajibu hatujala leo unatakaje?nikawaambia naweza kuwapikia?wakasema ww tu!wakaask aina ya msos nikawaambia mtakachotaka..wakahis km nawaenjoy.. nikawahakikishia nitawapikia..walikua 7@1500/plate..
asbh mume akaniambia kuna mafundi wanakuja kumalizia ujenzi hapa kwetu..wakaja mafundi 4 nikawaeleza nitawapikia wanilipe wakakubali kwa hyi siku ya 1 nikawapikia mafundi 11..@1500..
Mungu alivyo mwema na jiran yangu akawa anapaka rangi nyumba yake(usishangae hvyo tupo mji mpya kila mtu anajenga)nikaenda kuongea nao na wale mafundi..shoga kazini nikaomba ruhusa ya kibabe nimefiwa..so nikawa napika msos wa watu 18 daily... ruhusa yangu ilipoisha nikawa napika asbh wali (walikubaliana wote wale wali)nauweka kwa pots dada wa kazi akawa anapika mboga tu..maharag na nyama na mchicha...saa 7 anawapelekea kwa sahan.. wameenda kwa week 3.. i mean wote 18..sasa u can imagine tulimake sh ngap za bure bure ..na watu 18 nilikua napika 4kgs..maharage kilo na nusu nyama 1kg..pesa mfukoni..maisha haya yapo tu..na ukumbuke nikawateka na juice..dadake amka! pesa ipo ni ww kufikiria tu jinsi ya kuitafuta..hii ishu nimeifanya mwenyewe sijasimliwa[emoji4][emoji4] tafuta kazi hata kwa mama ntilie
Wee ni mpambanaji kweli kweli, big up
 
kuolewa sio.dili..mimi ningekuwa na akili nilizonazo sasa kwakweli nisingeolewa....ukiolewa unabanwa mnoo kila.kitu unachowaza kufanya unafikiria mume...mie kakangu anapiga pesa za madini musoma huko nataman kumjoin lakini ndo nashindwa!ndoa!dadeki
Yani wewe unandoa, harafu uamshauri mwenzio asiolewe duh! Kweli za kuambiwa changanya na, akwako.
 
Usiende kwa mganga kisa kuolewa kwani siku zote huwa naamn mchawi wa kwanza katika kuoa au kuolewa ni tabia zetu binafsi za nje na ndani

Jitahd katika kubadilika nakuwa mwanamke halisi mwenye moyo malezi na akili kama mwanamke halisi kila. Kitu kitakuwa sawa
 
Ni makosa kukata tamaa.

Wapi??

Hapana, Huu sio ufumbuzi hata kidogo.

Je umejitafakari ni kwanini? inakuwa hivyo.
- Vipi kauli zako?
- Vipi tabia na mwenendo kwa ujumla?

- Kwa hiyo kuna mawili unahitaji
1. Kazi.
2. Kuolewa.

My Take.
- Badili makazi, nenda kamsalimie shangazi/ndugu mkoa mwingine kaa japo miezi 6.
- Ukiwa huko iwe ni kiguu na njia kwenye nyumba za ibada,
- Hakika ndani ya huo muda huenda ukabahatika kumpata mwenza.
Najitolea hiyo miezi sita aje kwangu huku mbeya
 
Dada kama unajiamini ni wife material na unaweza kusimamia biashara kama ukipewa basi njoo PM. Nina jamaa yangu mfanyakazi kwenye company hapa dar kila siku ananisistiza nimtafutie mke aoe Ila awe na uwezo wa kusimamia biashara Zake. Hadi leo kaniambia kama nimepata mwanamke anae faa kuwa mke nimuunganishe nae. Kama upo serious njoo PM naweza nikakuunganisha nae.
 
Nenda insta kule kuna matangazo kibao hope utasaidiw na utafanikiwa
 
Nimekaa nikawaza miaka na miaka kwanini sipati kazi nanikipata sidumu nimejaribu kujua nini tatizo sijaona ila kweli na shida kuolewa tabu madharau sina naheshimu kila mtu na pia sinaga ugomvi wala chuki watu wananipendaga sana sio mtaani au maofisini ila kuolewa ngumu kila mtu anashangaa naombeni msaada umri unaenda ila sioni faida .

Yaani nimekata tamaa naona niende kule kama wengine naombeni msaada mahali pakwenda ni wapi ambapo sintajutia hela yangu kwa maana na hitaji suluhisho kwa ambaye anamjua mtaalamu mzuri naomba ani pm nipo serious so nahitaji na mtu ambaye yupo makini kunisaidia asanteni kwa muda wenu naamini nitasaidika.
Una umri gani? Unaishi wapi? Je muonekano wako unadhani kwa walio wengi wanauchukuliaje? unatatizo la kibaiolojia kama harufu nk.?
 
Nilikuwa na msikiliza tu yeye kaolewa ila ananiambia mimi nisiolewe .
😂😂😂kwahyo unahisi walioolewa wanafaidiiiiiii wenyew...than kuminywauhuru wako..unapata madili mazuri lakini kikwazo ndoa😊😊olewa mwayego....
 
Nimekaa nikawaza miaka na miaka kwanini sipati kazi nanikipata sidumu nimejaribu kujua nini tatizo sijaona ila kweli na shida kuolewa tabu madharau sina naheshimu kila mtu na pia sinaga ugomvi wala chuki watu wananipendaga sana sio mtaani au maofisini ila kuolewa ngumu kila mtu anashangaa naombeni msaada umri unaenda ila sioni faida .

Yaani nimekata tamaa naona niende kule kama wengine naombeni msaada mahali pakwenda ni wapi ambapo sintajutia hela yangu kwa maana na hitaji suluhisho kwa ambaye anamjua mtaalamu mzuri naomba ani pm nipo serious so nahitaji na mtu ambaye yupo makini kunisaidia asanteni kwa muda wenu naamini nitasaidika.
Huko unapotaka kwenda ndio unakwenda kuharibu kabisa
 
Back
Top Bottom