Ungenisoma vizuri na kunielewa nilicholenga usingekuja na hili la kutafuta kuhamisha hoja..
Lakini pamoja na hilo, kwa vile unahamishia hoja huko, ukweli ni kwamba waafirika wanaokwenda kufanya kazi kwenye nchi hizo hudhalilishwa sana; hili lipo wazi.
Wewe shida yako ni nini, mshahara mzuri huku ukidhalilishwa na kutwezwa utu wako?
Nchi hii imekosa kitu gani cha kuwezesha watu kujenga maisha bora kabisa, huku wakiheshimika duniani kote.
Mtwala anashindwa hata kufanya mipango tu ya wananchi wake kunufaika na mapori chungu nzima yaliyopo hapa, anaamua kuyagawa kwa hao hao wanakopelekwa watwana hawa; badala ya kuwajengea uwezo wa kuendesha mapori yao ili yawanufaishe wao huku wakilinda heshima zao?
Huu ni uongozi wa namna gani huu?