naombeni mawazo yenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

naombeni mawazo yenu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by cheusimangala, Jun 13, 2011.

 1. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2011
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Amani ya Mungu iwe juu yenu.

  nina rafiki yangu aliniomba ushauri nikaona ni vyema niwashirikishe tushirikiane mawazo.

  Huyu rafiki yangu (msichana) ana urafiki wa kawaida na wakaka wawili,hao wakaka ni marafiki.

  rafiki yangu alianza kufahamiana na kaka A,kaka A akamtambulisha kwa kaka B,wakaunda urafiki wa watu watatu.

  Wakati rafiki yangu anaanza kufahamiana na kaka A waliheshimiana vizuri na kaka A hakuonesha dalili zozote za kumhitaji shosti wangu kimapenzi.

  Ila kaka B baada ya muda fulani akaanza kuonesha dalili za kutaka uhusiano wa kimapenzi na shosti wangu,na shosti wangu anadai na yeye pia anajihisi kumpenda kaka B.

  Tatizo ni kwamba baada ya kaka B kuonesha interest na kaka A from no where na yeye anaanza kuonesha interest zake.

  Mbaya zaidi ni kwamba,kila kaka B akitaka kumake a move kaka A anajaribu kuvuruga,mfano kaka B alisema siku moja kuwa siku yake ya off atakwenda kumfundisha shosti wangu kucheza tenis kaka A na yeye japokua hiyo sio siku yake ya off hakwenda kazini ili aende nao huko kwenye hiyo michezo.

  Shosti wangu anadai kwamba hawa wakaka wamekua kama wanashindana kumipress,ila kaka B kwa kuwa ni mpole na mstaarabu amekua kama ameamua kumuachia kaka A.

  Shosti wangu anadai kuwa pamoja na kua kaka A alikua rafiki yake lkn anajihisi kumchukia kwa sbb kaka A anatumia mbinu yakumfanya kaka B adhani kuwa kaka A na shosti walikua na kauhusiano fulani kabla.

  Sasa shosti wangu hajui afanyaje maana mwanaume mstaarabu hawezi kushindana juu ya mwanamke,na ndivyo kaka B alivyoamua kumuachia kaka A lkn shosti wangu hamtaki kaka A.

  Sasa shosti wangu hajui afanyaje ili aweze kuwa na kaka B maana kaka A alivyozidisha makeke kaka B hamuombi tena shosti wangu kutoka out na haoneshi nia sana kama mwanzo.

  natanguliza shukrani zangu.
   
 2. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #2
  Jun 13, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  The power to control that iko vestesd in the shosti her self..
  Wanawake tumeumbwa na a very strong female intuation for these things
  hasa kama wahusika wako mbele ya macho yetu... Kosa alilolafanya shosti ni
  kuacha mpaka mambo yanaelekea yako out of control kwa sasa (yawezekana
  mwanzo she didn't mind the attention ya both kwake...)

  Hata hivyo yeye kisha gundua kua anampenda kaka B, Simlaumu A kwa kumwaga sera
  baada ya B kumwaga for guy wametofautiana.. inawezekana alikua anampenda na sababu
  alikua nae close hakua na haraka mpaka A alipomwaga sera... Hata hivyo nashindwa kuelewa
  ni kwanini A na B hawaja jadili hili suala for guys are good at solving nani ampate the lady!

  Chakufanya tokana na mtazamo wangu, kwanza shosti ahakikishe kua B anampenda na
  ana mpango nae, akihakikisha hilo inabidi akae ki utu uzima na A kumueleza the situation
  kana kwamba haja notice feelings za jamaa (mana naona hajamwanga sera wazi...)
  Kua sababu yeye ndo aliwa connect anataka ajue kua they have feelings for each other...

  Cheusimangala naamini wewe ni mzima...
   
 3. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,658
  Likes Received: 8,211
  Trophy Points: 280
  Shosti wako hajatulia...!
   
 4. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Kaka A anakaba mpaka kivuli sio lool.

  Kaka A hakuwa anajiamini mwanzo mpaka alipoona Kaka B anaonesha nia ya mapenzi na rafiki yako ana respond vizuri na yeye ndio akapata nguvu ya kutupa karata yak.

  Kwa vile njia inayotumika hapa ni ya vitendo bai ni muhimu rafiki yakjo atumie vitendo pia kumuonesha kaka A kwamba hayuko intrested nae. Kama ujumbe hautomfikia itabidi tu amwambie ukweli haina haja kuumiza kichwa atumie uhuru wake wa kuchagua.

  Kingine wote ni watu wazima na yeye inabidi amuonesha kaka B kama anampenda na sio lazima kila wamshirikishe au kumjulisha kaka A ahead of time.
   
 5. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hiyo inatokea tu kama hawampendi msichana au wameamua kumfanyizia dada wa watu!

  Usiamini kwamba wanaume wanaweza kukubaliana katika jambo la namna hii. Hata huyo kaka B atakuwa amejiweka pembeni anamchora binti anavyotaka kufanya kosa la kiufundi.

  Mzee DC
   
 6. T

  Tasia I JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 1,226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  yani hii ni very simple.
  kwakua urafiki wao tooka mwanzo ulikua ni wa kaka na dada (ofcoz huku ndikomapenzi huanzia mara nyigi)
  na kwa kua kwa mujib wako, kaka B ndie alieanza kumwonesha interest za mapenzi, na kwa kua yeye shost mwenyewe
  anadai kua anahisi kumpenda kaka B na sio A, basi wala asipate kazi. Afuate kile amabacho
  moyo wake unakitaka. in this case ni kaka B.
  Hta siku moja asiingie katika mapenzi kwasabab anahisi huruma kwa mtu bali kwa kua anmpenda mhusika.\

  wala asifikirie sana jibu ni aende kwa yule anaehisi kua anapendwa nae na yeyey mwenyewe anampenda.
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Jun 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Cheusi,

  Mwambie rafiki yako aache kuchezea akili za wanaume. Wanaweza kumgeuka wakati wowote na amini usiamini atajiua (they can decide to give her rope...hope unajua kitakachofuata). Kwa vile anampenda kaka B na anakiri hivyo basi kazi yake ni rahisi sana. Amweze kaka A bila kumung'unya maneno kwamba B keshabeba mzigo na A hana chake tena. Ni jambo zito ila litampatia freedom ya mwili, akili na moyo pia, kwa leo na hata ziku zake zote.

  Mimi iliwahi kunitokea na nikamweleza dada kuwa kama hataki kumweleza huyo mshikaji wangu kwamba mimi niko speed 150km/hr wakati yeye ndoa anajaribu kuwasha gari basi she is in for it! Alifanya hivyo na jamaa akaja kuniuliza nikamrudisha kwa dada. Mchezo uliishia hapo.

  Katika hili....Binti ndiye polisi, mwendesha mashtaka na hakimu. Akifanya mchezo atajuta!
   
 8. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #8
  Jun 13, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  It is beta i have been answered na a male...
  imeweka at rest mawazo yangu...
   
 9. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #9
  Jun 13, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180


  ha ha ha... nimeipenda hii...
   
 10. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #10
  Jun 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Watu wengi wamepata shida kwa kudhani kuwa ukimhurumia mtu atakupenda sana kumbe mambo hayatabiriki. Huyu dada asipochukua hatua basi ajiandae kukabiliana na makubwa! The guys can decide to team up na kumfanyia kitu cha ajabu sana kama hataonesha msimamo!
   
 11. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #11
  Jun 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Wewe Asha,

  Did u ever think kwamba simba na chui wanaweza kukaa pamoja na kukubaliana nani amle swala hata kama hawajamuua? Forget about that.

  Wakikaa pamoja basi ujue matokeo ya hiyo paradox yatakuwa makubwa kuliko paradox yenyewe!
   
 12. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #12
  Jun 13, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  I get! Hata hivyo i don't trust the guys...
  personally am very wary of guys ambao ni friends and
  woote they are interested in me...
  I could end up kutopenda woote maana wote hawanipendi
  for if they did wangekua considerate kwangu..
   
 13. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #13
  Jun 13, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  ...........ya nini malumbano, ya nini maneno ooooooh,
  najiweka pembeni naepusha msongamano oooh,
  bora nitulieee, ningoje changu na mie eeeeeeeeeeh!!!

  Kaka B katumia busara sana, kujiweka pembeni!
  Inaonyesha kaka A, hajiamini isitoshe ni mwoga!!

  Shosti nae aonyeshe msimamo wake, au ndo zile sitaki nataka?
   
 14. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #14
  Jun 13, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  ha ha ha .. si unajua "wapemba wanajauna kwa vilemba".
   
 15. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #15
  Jun 13, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Tatizo letu tunakuaga na ushindani wa nani ataibuka na mtoto mwisho wa siku lol.
   
 16. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #16
  Jun 13, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Sio mbaya ukiwa serious... BUT guys seriously there comes a time to GROW up!! lol
   
 17. charger

  charger JF-Expert Member

  #17
  Jun 13, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 2,324
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Subira yake ndo ilomponza kaka wa watu,mmh huyo B nae kutambulishwa imekua tabu,ila kwakuwa hawa jamaa ni marafiki na bado hakuna aliyekuwa tayari kwenye uhusiano na huyo dada wanaweza kukaa na kuongea kama wanaume,lakini pia huyu dada sijui analengo gani na hao wanaume,kama anatafuta mtu wa ku exchange vows basi hapo yeye ndiye mwenye uamuzi wa mwisho kujua yupi ni original na yupi ni mchina.Angalizo inawezekana pia hao guys wamewekeana dau kum wine huyo shosti,wanaume waangalie hivohivo tu sometimes unaweza usiamini mambo yao.:lock1::lock1:
   
 18. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #18
  Jun 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ndo maana tunasema kuwa huu mpira anao dada mwenyewe. Ni uamuzi wake kuuweka kwapani na kutimua mbio au kubaki uwanjani akacheza.

  Hilo la kuwaacha wote ni gumu Asha kwa sababu hapa si suala la tu kwamba wanaume wanampenda bali naye amendondokea mmoja wao. Sidhani kama itakuwa rahisi kukikwepa kitanzi!
   
 19. M

  Marytina JF-Expert Member

  #19
  Jun 13, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  kwa sasa siwezimpa mtu ushauri wowote wa kijamii as mwenyewe yanaelekea kunishinda
   
 20. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #20
  Jun 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ukisikia wamewekeana dau ujue ni wasanii. Linapokuja suala la kupigania wife materials sidhani kama kuna compromise hapo!
   
Loading...