Nishauri: Mke wangu kanijibu yeye ni mrembo, anatongozwa kila siku na kunambia maisha anayaweza sio lazima kuwa na mimi

Rahul Pacquao

Senior Member
Feb 9, 2013
148
180
Habari zenu wakuu.

Sio mara ya kwanza kuomba ushauri juu ya migogoro yangu Mimi na mwenzangu (mke) pia nimekuja kwenu kwa mara nyingine tena kwakua this time naona imekua too much na nimeona bora nijitoe kwenye mashindano.

Inshort aliyekua mke wangu nilianza nae mahusiano yapata miaka 6 mpaka sasa lakini ndoa yetu ina mwaka sasa na miezi 4 ni waajiriwa wote kwani tulipata kazi kwenye kampuni ya mawasiliano ila department tofauti

Kwenye kazi sasa tuna miaka 4 tukiwa kampuni moja tulifanikiwa kupata mtoto na mwenzi wa 12, mwanetu anatimiza miaka 4 Mungu akipenda. Kumekua na tatizo ambalo sasa limekua sugu kwani sio mara ya kwanza wala yapili kutokea

Kama tunavyo fahamu matatizo kwenye mapenzi yapo tu hilo halipingiki ila kutafuta solution hilo ndio swala la msingi lakin Mimi kila tukikwaruzana na mwenzangu kosa liwe langu au lake yeye kikubwa anachotangulizaga ni kuondoka na kukomba vitu vya ndani

Kitendo hicho alishanifanyia zaidi ya mara moja lakini kila ikipita muda wiki tatuu hadi mwezi hua anarudi na machozi kujifanya anajutia hua anatumia mlango wa wazazi wangu kuomba msamaha mwisho wa siku kwakuwa nampenda hua namsamehe na kusonga mbele na kuachana na yaliyo pita.

Hivi majuzi tuligombana pia chanzo kikubwa ni simu kwani kila anaporudi nyumbani mwenzangu yuko busy na simu kujifanya Ana report zakutuma nk.

Lakin tabia hiyo siku hadi siku ikazidi kukomaa kwani imefika hatua mpaka muda wa kulala yuko busy hata nikimsogelea hataki ikabidi nikae kimya nifanye utafiti nijue shida ni nini au mchawi ni nani nilichofanya nikachukulia u-busy wake kama kitu cha kawaida na usumbufu wa usiku nikaacha kwani kila usiku nimekua wakulala na masononeko mwenzangu akiwa busy na simu

Mwisho wa siku nawaza mpakaa napitiwa na usingizi nikishtuka gafla nakuta bado anaendelea hivo hivo nikiuliza ndo nakua nimezua ugomvi na kununiwa wiki nzima.

Nielendelea kuwa mvumilivu nikiwa na target yangu yakutaka kujua kinacho endelea kwenye hiyo simu yake kwani simu yake App zake Ali lock kwa finger print ikafika siku ya siku sasa nilitangulia mimi kulala kama kawaida nayeye akiwa amejilaza huku Ana chart simu yake

Kila nikimuombaga huwa nakuta chat zimefutwa kama ilivyo za mwizi ni 40 siku hiyo nilipo lala na yeye akachart na usingizi ukampitia alipoanza kukoroma nikaichukua simu yake nikatoa lock kwa kidole chake ndipo mchele ulipo mwagika kumbe mwenzangu alikua na mahusiano mapya na jamaa mwingine

Wakati naendelea kupekua pekua akashtuka sikusita kumuuliza kwani nihakiyangu kuuliza cha ajabu mwanamke alicho nijibu ni kwamba yeye ni mrembo tena yeye ni namba D anatongozwa kila siku na kunambia maisha anayaweza sio lazima kua na mimi. Iliniuma kwanamna nlivyokua nimejitolea kwake nikajikuta hatakuongea tena siwezi kwani walikua wamepanga na appointment tena ya kukutana njeee ya mji nilishikwa na hasira kiasi cha kumpatia kichapo nilipo taka kuchukua simu nibaki na evidence akaipasua ikatawanyika kila kitu palivyo kucha akaenda police kunikatia RB

Kwani maelezo aliyoenda kutoa nikwamba Mimi namtesa nampiga kila siku na hiyo simu nimevunja Mimi anataka nilipe nilikaa sero kwa muda lakini nikapewa nafasi ya kutoa maelezo yangu walipo sikiliza na kupima huku na huku wakasema tukae dawati mwanamke akakataa na kusema kama imeshindikana sheria kufata mkondo wake yeye anataka Mimi na yeye tuachane

Kikubwa alitaka niende jela nikakubaliana na yeye tukaenda nyumbani akachukua vitu vyake na kuondoka na kuniachia mtoto hapo nilishukuru kwani nilikua na hofu sana juu ya kumkosa mwanangu alipo ondoka kwao hakuenda akaenda kwa shoga yake kuishi imepita miezi 5 sasa alikuja mara moja tu kumuona mtoto kuhusu hilo i don't care.

Sasa amekua ni mtu wakunichafulia jina kila mahali kila mahali anapopita nikuongea mambo yasiyo faa na yasio na ukweli ndanii yake baadhi ya staff wenzangu pia kunitenga kupitia maneno yakee

Hapo hapo pia boss anamtaka mke wangu sasa boss ananiandama na kunitafutia sababu kila siku japo kua majukumu yangu natimiza inavyo takiwa nashindwa hata nifanye nini kila nnapopita nimekua wakunyooshewa vidole lakini nikasema hakuna haja ya kumuelezea yoyote matatizo yangu kwani naona kama nikujichoresha na kufaidisha watu lakini kinachoniumiza pia jamii inayo nizunguka watu nnao shirikiana nao kikazi sasa wako against me kutokana na maneno aliyo spread mwanamke huyo matokeo ya kumpoteza nimekubaliana nayo lakin maneno yake juu yangu sasa imekua too much na mimi sitamani wala sihitaji kusogea karibu yake wala kuzungumza nae kwani jeraha la moyo wangu laweza nisukuma nikafanya kitu ambacho Sio dhamira yangu nifanye nini wakuu!?
 
Pole sana mkuu,kitu muhimu mtoto wako unaye wewe na unamlea,kama angechukuliwa na huyo mama yake angelelewa katika maadili ya hovyo sana,

Mkuu wewe endelea kupiga kimya na kufanya majukumu yako kama kawaida,zidisha ibada,muombe Mungu,ukweli utakuja kujulikana tu,kama upo tayari ni vizuri ukatafuta mwanamke mwingine mwenye maadili mema ukafunga naye ndoa,huyo mkeo kitendo cha kukuchafua wewe huko nje ni anakitumia kama njia tu ya kuficha mabaya yake,

Inaonekana hata wakati mlipokua mkigombana na yeye kubeba vitu vyake na kuondoka,alikua anaenda kwa huyo mchepuko wake,hakuna mwanaume anayeweza kuja kumuamini mwanamke aliyevunja ndoa yake kwa ajili yake,hiyo haipo hata siku moja,yaani ukishamkimbia mumeo kisa mimi basi hata mimi sitokuamini abadan coz hata kwangu utadanganyika tu,


Good luck brother.
 
Kama ulivyomalizia mkuu, kaa nae mbali ili kujiepusha na lolote. Kumbuka tayari una jalada polisi la unyanyasaji, ukimgusa tena ndo utapotea mazima.

Mlee mwanao ukiona ni vyema oa tena maisha lazima yaendelee.
Halafu kama mwanamke ameacha mtoto kwako tena wa miaka 4 kasoro, unaona huyo ni mke kweli??

Kifupi ni kwamba alishakuchoka na ndo maana aliweza kukugeuzia kesi, mwache aende!
POLE!
 
Mkuu hapo fanya mambo yafuatayo

1 Tafuta mwanamke mwingine asiyekuwa Muajiliwa ( Mama wa Nyumbani) akurejeshe kwenye ulimwengu wa furaha tena

2Jipange vizuri kiuchumi yaani ifike stage uweze kusimama bila ajira yako ya sasa hivi

3 Jiandae kisaikolojia kwamba muda wowote unaweza kuachishwa kazi na bosi wako

4 Mrejee Mungu wako muombe sana akavushe katika matatizo haya
 
Pole sana
1. Ongea na HR ikiwezekana uhamishiwe tawi lingine la ofisi yenu.

2. Usijibu chochote kuhusu hayo anayosema mwisho hao wanaomsikiliza watachoka hatakuwa na jipya la kuwaeleza.

Mshukuru Mungu umeachana nae salama, we live only once and we deserve to be happy.
 
Pole sana mkuu,kitu muhimu mtoto wako unaye wewe na unamlea,kama angechukuliwa na huyo mama yake angelelewa katika maadili ya hovyo sana,

Mkuu wewe endelea kupiga kimya na kufanya majukumu yako kama kawaida,zidisha ibada,muombe Mungu,ukweli utakuja kujulikana tu,kama upo tayari ni vizuri ukatafuta mwanamke mwingine mwenye maadili mema ukafunga naye ndoa,huyo mkeo kitendo cha kukuchafua wewe huko nje ni anakitumia kama njia tu ya kuficha mabaya yake,

Inaonekana hata wakati mlipokua mkigombana na yeye kubeba vitu vyake na kuondoka,alikua anaenda kwa huyo mchepuko wake,hakuna mwanaume anayeweza kuja kumuamini mwanamke aliyevunja ndoa yake kwa ajili yake,hiyo haipo hata siku moja,yaani ukishamkimbia mumeo kisa mimi basi hata mimi sitokuamini abadan coz hata kwangu utadanganyika tu,


Good luck brother.
Ur very matured and wise! Alisikika mlevi mmoja hivi

Huu ndo ushauri bora aufuate. Watu watamsema tu na kumnyooshea vidole muhimu a mind his business basi. Huyo mwanamke anamtangazia ubaya mshkaji ili kufukia mabaya yake..

Pole sana mtoa mada
 
Pole sana
1.Omega na HR ikiwezekanawuhamie tawi lingine la ofisi yenu.

2. Usijibu chochote kuhusu hayo anayosema mwisho hao wanaomsikiliza watachoka hatakuwa na jipya la kuwaeleza.

Mshukuru Mungu umeachana nae salalma, we live only once we deserve to be happy.
Hiyo namba 1 sijaelewa una maanisha nini mkuu!
 
Mkuu kuanzia sasa usipende kukaa peke yako.
Ukiona mawazo yamezidi tafuta hata mtu mwenye heshima sana mbali na kazini au nyumbani muelezee hasira na huzuni yako.
Vinginevyo unaweza kujidhuru au kumdhuru huyo mwanamke.
Mkuu usije nawe ukanunua gunia mbili za mkaa kama wa Kigamboni ,You will go down to waste.
 
Kiongozi nakushauri we kaa kimya hivyohivyo na hata hao wanaojazwa maneno incase wakakuuliza usiwaeleze chochote kuhusu maisha yako binafsi
Wewe akili yako na mapenzi yako yote hamishia kwa mwanao na na kwenye kazi yako
Binadamu huwezi kumzuia kusema atasema sana lakini ipo siku ukweli utajulikana na watu watamdharau sana
 
Back
Top Bottom