Naomba Ushauri na Msaada Kuhusu OCD Inayonitesa Kila Siku

Naomba Ushauri na Msaada Kuhusu OCD Inayonitesa Kila Siku

Pole sana kwa changamoto unayopitia..
kuishi na ugonjwa wa kuwaza au kurudia jambo kupita kiasi (OCD) kila siku inachosha sana kiakili, lakini ugonjwa huu unatibika na unaweza kurudisha udhibiti wa maisha yako.

OCD inajumuisha mzunguko wa mawazo yanayoingia akilini bila kupenda na kusababisha wasiwasi mkubwa, yanayokulazimisha kufanya matendo ya kurudiarudia ili kupunguza wasiwasi huo.

Kupambana na hali hii peke yako ni ngumu, hivyo unahitaji mchanganyiko wa msaada wa kitaalamu na mbinu binafsi za kila siku ili kuushinda mzunguko huu unaokutesa.

Njia kuu na ya uhakika ya kushinda OCD ni kupata tiba sahihi ya kisaikolojia kutoka kwa wataalamu wa afya ya akili.

Dar es Salaam kuna vituo vinavyotoa Tiba ya Utambuzi wa Tabia (CBT), kama vile
1. Mind Matters (Haile Selassie Road),
2. hospitali ya London Health Center,
3. daktari binafsi Bosco Psychotherapist (Mkwajuni Road).

Pia, unaweza kufika katika Idara ya Afya ya Akili Hospitali ya Taifa Muhimbili au Hospitali ya Saifee kwa ajili ya ushauri wa kibingwa na uwezekano wa kuandikiwa dawa za kupunguza ukali wa wasiwasi ikiwa itahitajika.

Wakati unatafuta msaada wa daktari, unaweza kuanza kupunguza nguvu ya OCD kila siku kwa kuahirisha matendo ya kulazimishwa na kutoshindana na mawazo yanayoingia akilini.

Ukipata msukumo wa kukagua au kusafisha kitu, jiambie utafanya hivyo baada ya dakika tano, kisha ongeza muda huo kadri siku zinavyoenda ili kuufundisha ubongo kuvumilia wasiwasi bila kufanya tendo hilo.

Kubali mawazo hayo kama "wazo la OCD tu" na uyaache yapite yenyewe bila kuyapa uzito, huku ukipunguza msongo wa mawazo kwa kufanya mazoezi na kupata usingizi wa kutosha.

Mabadiliko makubwa huanza na hatua ndogo ndogo, na jambo la msingi ni kuwa na uvumilivu kwani kupona OCD ni mchakato wa hatua kwa hatua.

Ni muhimu pia kufunguka na kumshirikisha rafiki au mtu wa familia unayemwamini ili usijihisi uko peke yako katika mapambano haya magumu.
Asante sana migo
 
Hilo tatizo lipo ila jamaa anachotakiwa ni ku-reset ubongo wake kwenda default mode maana sasa settings alizozifanya zinamletea shida
Hakika migo ila napata shida sana maana nashindwa hata kujiambia kwamba nimeshafanya tayari ila haya ni mawazo tu
 
Obsessive-Compulsive Disorder (OCD) is a chronic, long-term mental health condition characterized by a distressing cycle of obsessions and compulsions.
Nenda hospital muone psychiatrists Kwaajili ya ushauri na pengine uanze dawa. Cha kukupongeza ni kkuwa angalau umejjua shida na ukoo positive. Hiii hali itaisha ukianza dawa. Usipo ttibbiwa utaanza kuwa aggressive na unaweza pata schizophrenia. Pole sana mwamba
Sitaki nifike huko
 
Duuh! Pole sana. Wasiwasi wa nini?
Hata sijui nikuelezee nini

Ila hata ninapoandika naweza kuandika neno nimeandika kabisa naliona lakini naweza kujikuta nalisoma hata mara 20 ili kuhakikisha kama ni kweli ni lenyewe tena napitia kila herufi najiridhisha kama ni sahihi halafu wasiwasi unakuja tena mbona kama si sahihi?
 
Hilo neno "migo" unalolitumia nadhani unalikopa kutoka katika lugha fulani ya Ulaya/Central and South America.Nadhani.Kwa usahihi ni "amigo"/chap/pal/buddy/friend!Hiyo "migo" labda ni jipya.
Ni kifupi hicho migo, yaani ni kama gee kwa guy
 
Back
Top Bottom