Naomba Ushauri na Msaada Kuhusu OCD Inayonitesa Kila Siku

Naomba Ushauri na Msaada Kuhusu OCD Inayonitesa Kila Siku

Wakuu salamuni.

Nimeamua kuanzisha huu uzi baada ya kuona hii hali imeanza kunipa usumbufu mkubwa kwenye maisha yangu ya kila siku. Kuna baadhi ya vitu navifanya kwa kurudia rudia sana kiasi kwamba vinanichosha na kunipotezea muda bila sababu ya msingi.

Mfano nikifunga mlango, baada ya kuondoka nahisi kama sijaufunga vizuri hivyo narudi tena kwenda kuangalia. Wakati mwingine narudia mara mbili hadi tano kuhakikisha tu umefungwa. Pia nikizima switch au vifaa vya umeme, lazima nijiridhishe mara nyingi kama kweli nimezima. Hata nikishaangalia bado mawazo yananilazimisha nirudi tena kuhakiki.

Hii hali imekuwa ikinifanya nichelewe mambo mengi, nipoteze muda kwenye vitu vidogo vidogo na wakati mwingine nikose kabisa amani ya moyo na raha ya kawaida. Kinachoniumiza zaidi ni kwamba akili yangu huwa inajua kabisa kuwa tayari nimefanya hicho kitu, lakini bado kuna msukumo wa kutaka kurudia kuhakiki tena na tena.

Nilijaribu kuwauliza baadhi ya watu kuhusu hii tabia, wengi wakaniambia huenda ni tatizo la OCD. Ndiyo maana nimekuja kwenu wakuu, labda kuna mwenye experience au uelewa kuhusu hili aniambie namna ya kupambana nalo au kupata solution yake.

Karibuni ushauri wenu wakuu.
unatumia kilevi chochote?
kwa kawaida huwa una lala masaa mangapi?
 
Mkuu jambo la kufanya inaonekana muda mwingi akili yako kuna kitu unawaza kukitekeleza au jinsi kilivyo hata unapotekeleza majukumu mengine unafanya lakini kumbukumbu zake hazipo kwasababu kuna jambo umelipa muda zaidi , ili uweze kama kuna ishu unaiwaza sana chukulia kawaida ili kisiwe kinachukua sehemu ya mawazo yako wakati wote na kile unachokitekeleza wakati huo akili ndio iwe hapo . Yale kama kuna magumu unayoweza kuacha acha Mungu mwenyewe ndio anaijua usiwaze namna itakavyokuwa maana wakati mwingine unaweza kumuwaza mwenye tatizo wewe ndio likakuingia na kukusababishia madhara kuliko yule aliye na tatizo ukamwacha na afya njema. kama ni mpenda vitabu , kuna kitabu cha SAMEHE NA KUSAHAU CHA MWAKASEGA, NA VINGINE VINAVYOENDANA VITAKUJENGA NA AFYA YA AKILI
 
mtu amekuja hapa kuomba msaada ila naona watu wengi wanaleta masihara na kebehi.. Hembu wacheni masihara nyie vijana na kama mtu huna jambo zuri la kusema ni vema ukakaa kimya
 
Sasa sijui kipi nakiwaza sana
 
mtu amekuja hapa kuomba msaada ila naona watu wengi wanaleta masihara na kebehi.. Hembu wacheni masihara nyie vijana na kama mtu huna jambo zuri la kusema ni vema ukakaa kimya
Achana nao migo mimi naangalia nimeshauriwa nini tu.
 
Back
Top Bottom