Naomba ushauri kwa ajili ya safari ya kitalii Afrika

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,397
Tafadhali naomba mchango wako wa mawazo!

Nimekuwa nikitamani sana kuzitembelea baadhi ya nchi za Afrika ambazo bado sijafika. Ninatarajia kutimiza sehemu ya hiyo hiyo ndoto hapo baadaye mwaka huu.

Ninatarajia kutembelea alau nchi nne, kama bajeti itaruhusu, nazo ni AFRIKA KUSINI, BOTSWANA, LESOTHO na NAMIBIA. Safari yangu itakuwa ya wiki moja.

Dhumuni kuu la kusafiri ni "kuosha macho", yaani, kuona jinsi maisha yalivyo katika nchi za wenzetu, n.k. Kwa kifupi, ni safari ya kitalii.

Bajeti yangu ni shilingi milioni mbili. Itagharamia mahitaji yote isipokuwa passport. Usafiri ni wa basi, na kwa upande wa malazi, nitafikia lodge za bei rahisi. Muhimu ziwe sehemu salama.

Naomba kufahamu yafuatayo:

1. Kwa bajeti hiyo, nitaweza kuzifikia nchi zote 4 au nitalazimika kuzipunguza? Hata kama nikilazikika kutumia siku moja tu katika nchi husika, itatosha. Na kama nikiona bajeti haitatosha, nitaondoa Lesotho na Namibia kwenye orodha ya nchi nitakazozitembelea.

2. Unanishauri nitembelee maeneo/ miji gani kwa kila nchi?

3. Katika hizo nchi tajwa, kuna inayohitaji visa kwa Mtanzania?

4. Wapi pa kupandia basi kwa mtu anayeanzia safari Mwanza? Lazima kwenda hadi Dar?

5. Mabasi gani yanatoa huduma husika?

6. Sina pasi ya kusafiria. Travel document itatosha? Najua yenyewe haichukui muda mrefu kupatikana.

7. Lodge zipi za bei rahisi lakini zilizopo maeneo salama?

8. Nini cha kuzingatia sana nikiwa
katika nchi husika na wakati wa safari kwa ujumla?

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa ushirikiano wako chanya. Asante sana.
 
Kwa Nchi ulizotaja zinahitaji kwa uchache safari ya mwezi mzima.

Hiyo wiki uliyosema na bajeti yako, utapoteza hela zako bure na hakuna kitu utaona/utafurahia.

Nakushauri ufanye utalii wa ndani hapa Tanzania kwa kuzunguka mikoa kadhaa na kuona vivutio mbalimbali.

(ukweli hata kutembelea tu hapa Ndani ukitaka kuona vivutio vya ukweli kama Machimpanzee kule kigoma, Nyumbu kule serengeti, Zanzibar stone town hadi beach nk hata hiyo wiki moja haitoshi...)

Kutembelea Nchi mbalimbali kwa ajili tu ya kutia mguu kwenye Nchi husika kwa masaa kadhaa, ni matumizi mabaya ya pesa hasa kwa mtu ambaye uchumi ni wa kuunga unga (nikujiongezea Umaskini)
 
Kwa Nchi ulizotaja zinahitaji kwa uchache safari ya mwezi mzima.
Hiyo wiki uliyosema na bajeti yako, utapoteza hela zako bure na hakuna kitu utaona/utafurahia. Kwa hiyo bajeti kwa wiki moja, nakushauri ufanye utalii wa ndani hapa Tanzania kwa kuzunguka mikoa kadhaa...
Lengo langu kubwa ni kuweka Historia kuwa na mimi nimeshatia migumu yangu South Africa, Botswana, Lesotho na Namibia.

Ndiyo maana nilitamani nifike kila nchi na kulala alau siku moja. Si lazima kutembelea maeneo yenye vivutio, kule kufika tu na kulala kwenye hizo nchi kwangu mimi nahesabu tayari ni utalii.
 
Back
Top Bottom