Naomba ushauri kuhusu hii ndoto

Naomba ushauri kuhusu hii ndoto

Ndugu unajua kutafsiri ndoto sio kila mtu anaweza na pia ni mojawapo ya karama kubwa sana, na hata kuota tu yenyewe. Jambo mfano unaloota mtu anaweza kudhania linaweza kua na mana ya Moja kwa Moja kumbe sivyo ni ujumbe mwingine unawasilishwa. Ningekufafanulia ila sio hadharani hapa. Na pia usipende kusema ndoto zako ovyo ovyo kama hivi kwenye mitandao. Ukijitambua zaidi utakuja kufahamu sababu kwanini NIMEKUAMBIA hivyo.
 
Hakuna ndoto isiyo na maana,ila tu sisi siyo watu wa kuagua ndoto

Ila kwa ushauri wangu: jiandae, hakuna atakae ishi milele

Jiandae
 
Ndoto imejigawa sehemu mbili kiimani, sehemu ya kwanza ni kwamba ukiona unakumbuka matukio yote ya ndoto yako, ujue hiyo ilikuwa ndoto ktk mfumo wa kuchoka ubongo na hisia, yaani hiyo ni ndoto kama ndoto haina maana yoyote.
Lkn sehemu ya pili imejikita kwenye usahaulifu, yaan ukiota ndoto mara kadhaa au mara moja na ndani ya maisha ya ndoto hiyo ukapata hisia za uchungu yaan ukahis moyo na hisia vimekosa Amani kisha uliposhtuka ukasahau baadhi ya matukio ya ndoto yako ujue huo ulikuwa ni ujumbe mzito kiroho! Sasa kama ni mwanaume hakikisha wiki 2/4 usishiriki ngono vivyo hivyo kwa mwanamke, na kwa mwanaume usikae jiran wala kushea lolote na mwanamke aliye ktk siku zake,, ndoto hiyo inamaana ya kuishi umri mrefu hivyo hakikisha unakumbuka ndugu waliotangulia ktk haki, nenda kasafishe makaburini kwakuwa roho zao zinakuombea kheri na kukumbusha maisha endelevu na mwisho, ndiomana umeota kifo badala ya kufa ukaamka na kutafakari ndoto!
 
Nimeota zaidi ya Mala tano kwamba nimekufa,hii ndoto inanipa mawazo sana naomba ushauri wenu,je ina maana gani?@mshana
Unaota umekufa, elezea mazingira kuna wengine wanaota wameufa wapo kaburini wamefukiwa, mwingine anaota nafsi ipo pembeni inahuzunika ikijiangalia watu wanavyoomboleza kwenye jeneza. Mwingine anaota yupo kwenye jeneza anasikia watu.
 
Na ile ndoto uliyokuwa unakimbizwa na ng'ombe mkubwa kama nyati.....
Halafu kila ukijaribu kumkimbia unaanguka...
 
Back
Top Bottom