Naomba ushauri kuhusu dini

Naomba ushauri kuhusu dini

Unaelewa nini pale nguzo ya Imani ya Dini yetu ya Kiislamu inapotaka kuviamini vitabu vya Mwenyezi Mungu?.
Pili mimi ntamuelewesha asiye Muislamu kwa njia atakayo ielewa kwa wepesi kwa kutumia mifano na njia alizo zoea.
Ningekuwa najadiliana na Muislamu mwenzangu,basi nisingetumia Injili bali ningetumia Qur'an,hadithi na sunna za mtume.

Nafikiri umenielewa.
Najitahidi kuelewa, nadhani nimeelewa kuwa tutumie maneno yenye hikma ya Mungu haijalishi yanatokea kitabu gani.

Na wewe unajitahidi kutumia zaidi kile ambacho muhusika ataelewa. Okay ni nzuri hata mi hufanya vivyo hivyo kadri navyoweza
 
Usikimbie hoja.

Hebu ingizia huo mfano wako wa gari linalomilikiwa na familia na hizo sifa zake, katika kufafanua utatu uone unavyojichanganya.
Tumiaa mfano wa mwana mpotevu huo utakuonesha jinsi ufalme wa mbingu ulivyo. Katika masuala ya umiliki.

Achana na huo mfano wangu wa gari, katika huo nilitaka zaidi kuonesha kuwa kidogo kikifanana kila kitu chake na kikubwa unaweza sema ni kimoja na kikubwa na hapohapo ukasema ni kitoto cha kikubwa.
 
Msonjo na KING KIGODA kuna mambo mengi tu ambayo hayawapaswi watoto. Lakini ukishakuwa mtu mzima unapaswa kuyaelewa. Acha watoto wadogo wapewe maziwa sisi tule hadi makande.

Mnaweza kuona hata wenyewe, ukweli wake pale ambapo kila maagizo yanapotoka kwa Mwenyezi Mungu yanakuja kwa wingi. Kwa nini msipinge hili?

Ndo maana nikasema tusimuweke Mungu kama 'concrete' being tumuache hivyohivyo kama Roho ama wazo 'abstract' being

Unajua katika mawazo hakunaga utofauti kama ni lengo moja? Nitatoa mfano.
Kama lengo ni kujenga bomu. Chochote kitakachowazwa kuhusiana na uelekeo wa kujenga bomu kinaangukia kwenye wazo lilelile moja. Ni wazo moja. Ila kikitokea kingine kikawazwa kikawa cha kubomoa huo mpango wa bomu ndio kitaitwa wazo tofauti wazo la pili. Ndio tutapata mawazo mawili 1. kujenga bomu 2. kuharibu/kutojenga bomu
Nisaidie tafsiri ya maneno haya-

Tito 2:13

tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu
 
Sawa ila Kama unasali makanisa toka Western world nikuambia tu unapoteza mda
 
Naomba utambuzi wako katika dhana isiyo egemea kwenye imani

Jiwe ni koumbe hai au siyo?
Mkuu!Jibu langu lipo wazi sana,mimi nimekujibu kuwa sifahamu juu ya jiwe kuwa kiumbe hai au kiumbe mfu kwa sababu mimi sina elimu ya mawe!.
Lakini kama unataka nikujibu kwa upeo wa macho yangu,sawa ntakujibu.
 
Dini zimeundwa na watu, wewe fuata dhamira yako, mimi naamini Mungu ni "JUA" kitu ninachokiona. Hata kama sio kweli, hakuna mwenye ukweli, siku roho ikiachana na mwili nitaujua ukweli na kumuona Mungu wa kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nisaidie tafsiri ya maneno haya-

Tito 2:13

tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu
Hapa nadhani utafurahi kusikia mkristu anatamka hivi.

Tunatofautiana uelewa kiroho kuna watoto na watu wazima. Paul alitumia usomi wake kuwaelekeza watu katika lugha ambayo wataielewa kwa urahisi. Kuna vitu alivilainisha kwa kusudi jema tu kulingana na anaowaandikia. Wasomi wote hufanya hivyo.

Mitume wote na manabii wote walifanya hivyo, kuliwasilisha jambo kwa namna inayoeleweka kwa wanaowaambia. Ndo maana lazima tutumie akili kuelewa maana na muktadha

Mimi tafakari yangu itakuwa: Katika dunia ilokuwa na miungu mingi kwa levo walokuwa nayo wa juu kuliko wote akawaambia ni Yesu. Ukilinganisha na hiyo miungu. Ndiyo maana akasema Mungu mkuu kwa levo yao.

Titus 2:13, CSB: while we wait for the blessed hope, the appearing of the glory of our great God and Savior, Jesus Christ.
 
Sawa nakubali havifanani vyote kama vyote. Havifanani. Ninakubali kimaterial kuwa 'Mwana hawezi kuwa sawa na baba au mama aliye mzaa' Ila kimalengo, kiabstract, kiroho, kilogic hilo lipo.

Na utofauti wake upo hivi tukiuangalia sisi tulio wadooogo sana. Ni kwamba kutokana na udogo wetu sisi tunamuona Mwana kama 'infinity' kwetu. Ila tena tukijaribu kumuimagine Baba basi tutasema yeye anakuwa 'infinity plus one' au hata 'infinity plus hundred' au potelea pote labda ni 'infinity plus infinity' au ngoja tuvuruge labda baba ni 'infinity plus infinity, infinitely'

Sasa kwa kuwa sisi ni wadogo, finite beings: infinity ya aina yoyote na ukubwa wowote makes no difference in our perception of infinity. Ndo maana unaona kama tunajichanganya. Subset kwetu ni infinity [kikwetu] japo tunatambua kuwa imo ndani ya universal set ambayo ni infinity infinity
Kijana kuna vitu unaandika mpaka unanipa uzito kukujibu. Hakuna uhalisia katika "Infinity" kwa ufupi "Infinity" hai exist.

Kingine usiseme kikwenu kwamba infinity ni subset. Bado unaokena una uwezo mdogo sana wa kufikiri. Kimaana tu infinity ni kisicho mpaka vipi kiwe tena subset yaani kipatikane ndani ya kitu fulani ?

Nakuuliza swali dogo, unakubali kwamba kuna "Infinity series ?"
 
Mbona hizi nyuzi za kunanga uislam zimeibuka ghafla sana hapa Jukwaani ndani ya hii wiki?Kwani kuna ajenda gani?

Mara waislam milioni kumi wanakuwa wakristo kila mwaka,Mara ushauri kuhusu dini na nyingine nyingi kama hizo.

Nadhani kuna haja ya moderators kuwa makini katika kipindi hiki. Nadhani kuna project baadhi ya members wanataka kuifanya.
 
Umeeleweka lakini mkuu ndiyo maana kuna ushauri
Vizuri madam kama umeelewa.

Mimi pia nilikuwa mfungwa wa dini mpaka nilipopata maarifa sahihi kumuhusu Mungu.

Dini zina kifungo na utumwa, kutishana tishana na kujengeana nidhamu ya woga. Tena wanaokutisha wenyewe wanajijua kuwa ni wa hovyo kweli kweli katika nafsi zao.

Simamia hapo hapo unapo paamini dada angu usiyumbishwe upo sehemu salama.

Warumi 8:1 (KJV) Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
 
umezingua dada, kama hupendi uislamu huwezi kuanza kukashfu mazingira mazima ya uislam, ungeenda kwa wakristo moja kwa moja ili wakupe sababu zaidi ya kuipenda dini yao. shida umehusisha mada yako jf kwenye muktadha wenye dini zote..hupendi shule za kiislam sawa hujalazimishwa kuwapeleka huko, lakini pia uislam haukushikii bunduki ubaki. ndio maana asili ya imani.

Penda dini yako bila kuleta bugdha kwenye dini ya wenzio.
 
Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata. Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.
Yn 10:27‭-‬28 SUV

Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;
Yn 11:25 SUV

Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Yn 14:6 SUV


Haujakosea, upo mahali sahihi. Mungu azidi kunena na ww uzidi kuujua ukweli.
 
Mbona hizi nyuzi za kunanga uislam zimeibuka ghafla sana hapa Jukwaani ndani ya hii wiki?Kwani kuna ajenda gani?

Mara waislam milioni kumi wanakuwa wakristo kila mwaka,Mara ushauri kuhusu dini na nyingine nyingi kama hizo.

Nadhani kuna haja ya moderators kuwa makini katika kipindi hiki. Nadhani kuna project baadhi ya members wanataka kuifanya.
Mashehee kulawitiii hilo naloo limekaaje..
 
Back
Top Bottom