Naomba ushauri kuhusu dini

Naomba ushauri kuhusu dini

Ni ipi ilikuwa ‘Aqidah na Manhaj yako huko zamani?

mmmh!

mmh!

Nina maswali mengi. Ila ngoja nikae kimya.

cc Kisai Kazakh destroyer naombeni muweke neno hapa.

رَبَّنَا لَا تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْهَدَيْتَنَا وَهَبْ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً ۚ إِنَّكَ أَنتَ ٱلْوَهَّابُ

“Our Lord, let not our hearts deviate after You have guided us and grant us from Yourself mercy. Indeed, You are the Bestower.” (Qur’an 3:8)


Ewe Mwenye kuzigeuza Nyoyo, uthibitishe Moyo wangu katika Dini yako.
Hawa watu wa namna hii wako wengi sana, wanajidai Waislamu kumbe si Waislamu, lengo lao ni kuichafua dini ya Allah, ila hili haliwezkani.


Hii mada nawaachia nyinyi ndugu zangu mmalizane, mimi naona kama anmtanipotezea muda. Nasoma maoni yenu nipate faida.
 
Mkuu dini zote tunamuabudu Mungu na sio kwamba kwa sababu mtu ni dini flani basi ataenda mbinguni isipokuwa matendo yako yatakupeleka na uamini wako,dini zote zinahubiri mambo yaleyale hivyo kama una amani zaidi kwenye ukristo basi fata moyo wako.
 
Hata Catholic bado hujafika bado
Tafuta mahali Kristo anahubiriwa na Mungu anajifunua. Uokoke umpokee Yesu maji ya baraka yanakupotezea muda tu
 
Mimi ni Muislam kwa baba na mama na hatuna historia ya dini nyingine labda huko nyuma kabisa ambapo hata bibi zangu hawakuwepo au hawajui, imetokea mimi tu kuupenda ukiristo kiasi ambacho tangu niko form one miaka zaid ya ishirini kubadili majina yangu na kuwa ya kikiristo na nilikua nikisema baba yangu mktisto mama yangu ndiyo muislam, bahat mbaya nikiwa form two nilikaa hostel ya waroma kwahivyo nilikuwa napenda wakati mwingine kwenda kanisani japo nilikua sielew kitu, kuna wakati napotezea naanza kusali kiislam kwasabu dini ya kiislam naijua nimesama madrasa nikiwa mdogo na hakuna kitabu cha dini kina kina kinanishinda kusoma na hapo zaman nilikua nikisia mtu anasoma kuruan nalia bila kujua nalilia nini nikawa namwambia mama mbona nie nalia nikiona au kusikia kuruan inasomwa? Mama ananiambia tu inaitwa midadi hiyo.

Nimejikuta tu wanangu sijawapeleka madrasa na shule nimewapeleka shule za kikiristo na sipend kabisa za kiislam wala madrasa na huwa nawaambia wanangu nendeni kanisani, na utu uzima huu kuna wakati nilipata majanga makubwa nikaona njia sahihi ni kuombewa kanisani nikaenda roma kuombewa ndani ya siku tatu pepo likatoka na nimeendelea kusali kiroma nikiwa nyumban na natumia maji ya baraka wakat mwingi nahis kabisa yananisaidia, halaf nikiwa kanisani nina aman zote nachokisema nakielewa nachokisali nakielewa! Naona mahubir ya father nayaelewa vizuri na hapa nyumban redio nasikiliza redio maria tu na naifurahia.

Sasa wakuu nisaidieni hili ni pepo au nini? Je nibadili dini na utu uzima huu? Au nifanyaje nifute historia hii? Yaan sahiv ndiyo nazid kuzama kwenye ukristo kiasi ambacho hata wanangu nataman waanze mafundisho, au kuna sehem sijielewi?
You are just a Scammer.

Wewe ni mkristo pure, tena mgonga kengele kanisani.

Acha ulaghai, kwa jifanya eti..... Blah .. blah.. blah.

Dini zinyewe za kuja tu...
Amini chochote tu... Acha ulaghai.

Ila

Hakuna moto wala pepo.
 
Njoo atheism huku hakuna viingilio vyenye kupewa majina kupunguza ukali kama sadaka au swadaka
 
Je alivyoweka wanyama, vyakula, vinywajink akasema kuleni hivi na msile vile ni kwa nini? Alivyokua adamu bustanin akaambiwa asile lile tunda ni kwa nini?
Jibu ni kukujaribuni je mtamtii katika maamrisho yake au mtakwenda kinyume. Hivyo uwepo wa dini mia au mia mbili ipo iliyosahihi na ni uislamu kazi kwako ukubali au ukatae au ulete unlogical argument skwa maarifa na ujuzi aliokupa wewe. Na ili kuwataini watakaofaulu na watakaoshindwa ndio maana kutakua na kiyama ambapo wapo watakao fuzu watapewa mm pepo waliyoahidiwa na watakao feli basi mafikio yao yatakua ni motoni, allah atujalie pepo yake na atuepushe na adhabu ya moto

Hebu pumzika dada huendi popote na hamna aliyeenda akarudi ebooh
 
Huwa naumia roho yangu nikiona mikwara ya kutishana badala ya kuelimishana! Nimezaliwa kwenyw uislam lakini nimekua nawaza ukiristo sijapenda hivyo yaan sijawaza kubadilika ila mabadiliko yamenipenda na kule nimekuta hakuna kutishana bali kuna kuelimishana na kuhubiriwa kwa lugha ninayoielewa kiswahili, ninaomba na kusali ninachokielewa! Kwahiyo mkuu usinitishe hakuna aliyekufa akafufuka akaeleza aliyoyakuta huko! Hata yesu sijui kama alisema kwa mungu kukoje au unielekeze
Nakupenda sana
 
Inatosha, upo vizuri labda tu tuongeze kitu hapa ili kuelewana:

Ukisikia Mkristu anasema Yesu ni Mungu usidhani amemuondoa Mungu kwamba hayupo. Huku kuna fundisho la utatu, lakini huo utatu ni 'mmoja'. Akili yako ikiweza kuyachukulia haya ndio utaelewa kuwa wakristu pia tunamtambua Mungu mmoja na hakuna Mungu mwingine isipokuwa yeye.

Mfano familia fulani inamiliki gari moja.
Sentesi A. Tunalo gari jeusi, zuri linalotumia petroli na linakimbia kwa kasi sana.
Sentensi B. Tuna gari linalokimbia

Tunaruhusiwa kusema sentensi B na sentensi A ni moja. Tunaruhusiwa pia kusema sentensi B ni mwana wa sentensi A na wakati tulisha sema ni moja na hatujachanganyikiwa! Kosoa hii logic kwanza kama iko na makosa. Kama haifai niambie nitumie miduara[cocentric circles labda tutaelewana
Kwa upande wangu sidhani kama kuna ulazima wa kutumia neno lenye utata na kuliacha neno lisilo utata ili hali maneno yote hayo yana maana moja.
 
Huwa naumia roho yangu nikiona mikwara ya kutishana badala ya kuelimishana! Nimezaliwa kwenyw uislam lakini nimekua nawaza ukiristo sijapenda hivyo yaan sijawaza kubadilika ila mabadiliko yamenipenda na kule nimekuta hakuna kutishana bali kuna kuelimishana na kuhubiriwa kwa lugha ninayoielewa kiswahili, ninaomba na kusali ninachokielewa! Kwahiyo mkuu usinitishe hakuna aliyekufa akafufuka akaeleza aliyoyakuta huko! Hata yesu sijui kama alisema kwa mungu kukoje au unielekeze
Namna pekee ya kuepuka hivyo vitisho ni kuwa atheist tu

Huku tunaogopa umasikini sio mythical hell
 
Ukisikia Mkristu anasema Yesu ni Mungu usidhani amemuondoa Mungu kwamba hayupo. Huku kuna fundisho la utatu, lakini huo utatu ni 'mmoja'. Akili yako ikiweza kuyachukulia haya ndio utaelewa kuwa wakristu pia tunamtambua Mungu mmoja na hakuna Mungu mwingine isipokuwa yeye.
Hivi hili fundisho la UTATU nani aliliweka kwa mara ya kwanza ? Maana najua kabisa Yesu hawezi kusema haya, sababu alikuwa ni nabii wa Allah.
Mfano familia fulani inamiliki gari moja.
Sentesi A. Tunalo gari jeusi, zuri linalotumia petroli na linakimbia kwa kasi sana.
Sentensi B. Tuna gari linalokimbia
Kutete ushirikina kazi sana. Natamani ungekielewa hiko ulichokiandika. Kanuni ya utoaji mifano umeiitupilia na hili nina uhakika kabisa kwamba huijui. Usilete falsafa na logic katika uhalisia. Mfano wako ulio utoa hauingii katika mfano wa utatu au kupitia mfano huo ukahalalisha utatu, hapo umedhibirisha wazi ni kwa namna gani Wakristo mnauwezo mdogo sana wa kuhoji.

Kwanza ulitakiwa utuambie Mungu ni nani hasa ? Sifa zake na tabia zake.

Mfano ulio utoa una leta maswali mengi sana miongoni mwa maswali hayo ni lazima tumjue nani mmiliki hasa wa hilo gari ? Kama wanamiliki wote ushirika wao uko sawa ? Lakini je hawapingani katika maamuzi juu ya gari hilo ? Sasa unapo toa mfano mambo hay unatakiwa kuyatilia maanani.
Kingine siyo unachosema "mnalo" basi wewe ni mmiliki au wewe una miliki, bali una muwakilisha yule mwenye kumiliki ambaye katika huo umiliki hamuwezi kuwa sawa.
Tunaruhusiwa kusema sentensi B na sentensi A ni moja.
Hakuna ruhusa hii katika lugha yoyote hata kimantiki inakataa sababu kikubwa hakiwezi kwa sawa na kidogo, yaani "Subset" haiwezi kuwa sawa na "Universal set" mpaka uanishe baadhi ya mambo na kuyatoa mengine.
Tunaruhusiwa pia kusema sentensi B ni mwana wa sentensi A na wakati tulisha sema ni moja na hatujachanganyikiwa! Kosoa hii logic kwanza kama iko na makosa. Kama haifai niambie nitumie miduara[cocentric circles labda tutaelewana
Hapa ndipo mlipoharibu dini yenu kuruhusu mawazo ya watu yaamue juu ya maandiko na cha ajabu mawazo yao hayakuweza kung'amua maandiko.

Hili jambo linakosolewa kwa uhalisia sababu hiyo logic imekwepa uhalisia. Hakuna nafsi tatu muda huo huo zikawa moja, huko ni kuikosea adabu akili mliyo pewa bure kwa kuipuuza na kuifanyia kazi.
 
Kwa upande wangu sidhani kama kuna ulazima wa kutumia neno lenye utata na kuliacha neno lisilo utata ili hali maneno yote hayo yana maana moja.
Hapa ndipo Wakristo mlipo angukia pua, ukisoma maelezo ya mwenzako anaonyesha wazi hicho alichokiandika hakijui na hawezi kukitetea, anawezaje kuelezea maandiko ya dini kwa kutumia falsafa na logic ? Elimu dhaifu namna hii ?

Hapa alitakiwa aende na maana za maandiko na uhalisia ila huko alipoenada hapakidhi haja.
 
Swadakta. Yaani islam ingekuwa dini ya haki kama wanavodai ingekuwa inatawala dunia, na mungu asingeruhusu dini nyingine itawale
Mwenyezi Mungu humpa nguvu amtakaye na umnyima amtakaye na vyote(kunyimwa na kupewa) sio kiashiria cha kupendwa au kuchukiwa bali ni mtihani .

Mbona Wana Israel kipindi cha mateso ya firauni Mwenyezi Mungu aliruhusu wateseke huku firauni akiwatawala je hapo firauni alikuwa kipenzi cha Mwenyezi Mungu kwa vile alikuwa super power kwa wakati ule ? na vipi mwisho wake ukikuwaje ?
 
Uzima wa milele, Wakati tunaona makaburi ya Wakristo yamejaa, sawa tu na wasiyo Wakristo, unachekesha wewe.
Hebu nenda Mburahati ukaone, angalau mngedanya, kuwa wakristo mtafufuliwa baada ya kufa, maana kufa lazima ufe hivyo hakuna uzima wa milele.
.
Mkuu!Hivi hata kiswahili ni kigumu kwako?.Ni wapi andiko limeongelea kufa mwili?Na niwapi nimekuambia kuwa mimi mkristo?
Usipoelewa kinachoelezwa na mtu ni bora zaidi ukikaa kimya kuliko kujidharirisha hivi.
 
NAOMBA KWANZA ICHUNGUZE MISINGI ZA IMANI HIZI 2 KAMA ZINAVYOJIELEZA.

UKRISTO
- Ni kuamini katika UTATU yaani Mungu,Mwana wa Mungu na Roho Mtakatifu.
-Kuamini kusulubiwa,kufa na kufufuka kwa Yesu.
-Kuamini hakuna maombi yanayoweza mfikia Mungu bila kupitia kwa Yesu.
-Kuamini kuwa Yesu pia ndiye Mungu mwenyewe mkuu.


UISLAMU
-Kuamini kuwa Mwenyezi Mungu ni mmoja na hana wa kufanana naye Duniani na Mbinguni.
-Kuamini kuwepo kwa Malaika na utendaji wao.
-Kuamini Vitabu vyake vyote Mwenyewe Mungu vikiwemo Torati,Zaburi,Injili na Quran.
-Kuwaamini Mitume wote walitumwa na Mwenyezi Mungu akiwemo na Yesu.
-Kuamini katika Qadar yake Mwenyezi Mungu,yaani matokeo yote ya kheri na Shari ni katika ruhusa yake.
-Kuamini kuwepo kwa siku ya mwisho,siku ambayo watu wote watafufuliwa kwa ajili ya hesabu ya matendo yao.


Mkuu!Ukijikita katika kuchunguza MISINGI hiyo ya IMANI,nina hakika utapata majibu ya wapi ufuate japo kwa kuanzia.Asante.
We una amini jiwe ni kiumbe hai?
 
Ni ipi ilikuwa ‘Aqidah na Manhaj yako huko zamani?

mmmh!

mmh!

Nina maswali mengi. Ila ngoja nikae kimya.

cc Kisai Kazakh destroyer naombeni muweke neno hapa.

رَبَّنَا لَا تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْهَدَيْتَنَا وَهَبْ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً ۚ إِنَّكَ أَنتَ ٱلْوَهَّابُ

“Our Lord, let not our hearts deviate after You have guided us and grant us from Yourself mercy. Indeed, You are the Bestower.” (Qur’an 3:8)


Ewe Mwenye kuzigeuza Nyoyo, uthibitishe Moyo wangu katika Dini yako.
huyu amepatwa na shambulizi la shetani na limempata akiwa hana kinga hata 0.00000 so ni suala la muda tu atahamia huko anapotamani, aaamyn atuepushe sote kaka.
 
Kwenye Biblia Yona aliitwa na Mungu akaokoe watu wa Ninawi lakini hakutaka kufuata sauti ya Mungu badala yake akapanda Meli kwenda Tarshishi ili asitii agizo lq Mungu lakini meli aliyopanda ilipata mawimbi sana hadi alipojitokeza akajisalimisha walivyomtupa baharini meli ikatulia na akamezwa na samaki akakaa kwa siku 3 tumboni kwa samaki akisali hadi samaki akamtapika kwenye ufukwe wa mji ule ule aliokua hautaki.....akafanya kazi aliyotumwa na kusudi la Mungu kikatimia.
Nimejikuta na relate habari yako na kisa cha Yona, inawezekana msukumo ulionao ni Mungu ameweka ndani yako ili akutumie kwa jambo fulani kudhihirisha ukuu wake, Inawezekana Mungu anataka akakutumie maisha yako yawe ushuhuda kwa wengine. Kuna maneno yanasema "God does not call the qualified but he qualifies the called " ....Mimi nakuombea kusudi la Mungu litimie kwako na akutumie vile anavyotaka.
Natamani sana sana uje utupe ushuhuda siku moja Empress_sheila
 
Hapa ndipo Wakristo mlipo angukia pua, ukisoma maelezo ya mwenzako anaonyesha wazi hicho alichokiandika hakijui na hawezi kukitetea, anawezaje kuelezea maandiko ya dini kwa kutumia falsafa na logic ? Elimu dhaifu namna hii ?

Hapa alitakiwa aende na maana za maandiko na uhalisia ila huko alipoenada hapakidhi haja.
Mkuu!Kwanza mimi siyo mkristo.
Lakini pia ni vema ungenifuatilia huko juu ili kujua mimi nafundisha nini na kwa aina gani ya mafundisho.
Asante.
 
Back
Top Bottom