Nikiwa kama Daktari nashauri Serikali itangaze Rasmi Wananchi wachukue hatua za kujikinga na huu ugonjwa ambao tayari ushaua watu milioni 3 duniani.
Jamani sina uhakika kama huu ugonjwa upo kwetu lakini la kujiuliza ni kuwa upo kwa majirani zetu wote, achilia mbali nchi za Ulaya, Marekani, Amerika ya Kusini na Nyinginezo.
Tuache kukaa kwenye mikusanyiko, tuvae barakoa, kunawa mikono, kutosalimiana kwa kupeana mikono, kukaa mbali mbali (Distancing).
Nawapongeza Maaskofu na Mapadri Makanisani kwa kufuata utaratibu huu. Nawashauri BAKWATA, tena kwa kukaribia MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI kuwashauri waumini wa kiislamu kufuata utaratibu huu misikitini na hasa Distancing.
Nimetoa ushauri kwa Serikali yangu kwa nia njema kabisa hasa ukizingatia kwa sasa Dunia ni kama kitongoji.
Ahsanteni.