fasiliteta
JF-Expert Member
- Jul 2, 2014
- 2,165
- 3,655
Nafikiri ni muda sahihi sasa wa Serikali kulazimisha usafiri wa umma kubeba level seat Ili si tu kukabiliana na COVID bali hata magonjwa mengine ikiwamo TB,Magonjwa yote ya kuambukiza kuanzia UTI,CHOLERA n k.
Watu wanahemeana sana mpaka wanapakana majasho na kuhemeana usoni kabisa.
Serikali naona inacheza tu na mustakabali wa raia wake,Ni bora wasitutangazie uwepo wa huu ugonjwa kuliko kutangaza watu wavae barakoa,kunawa mikono na kukaa distance huku wakiacha usafiri wa umma kusimamisha na kurundika watu kwenye usafiri wa umma(Daladala,mwendokasi,pantoni).
Waende mbali na kuangalia mikusanyo ya watu kuanzia masokoni,masherehe mpaka mipirani.
Kuendelea kuruhusu haya ni kujitekenya tu then unacheka mwenyewe.
Watoto Mashuleni tuone nao kuna juhudi gani zinafanyika kwa mashule hasa watoto wenye matatzo mbalimbali ya kiafya.
Vyuo navyo pia tahadhari ziendelee kuchukuliwa huku baadhi ya masomo walazimishwe kusoma kwa mtindo wa ZOOM/LECTURES mtandaoni.
All in All still naamini njia aliyotumia Mwendazake ni nafuu kubwa kwa nchi Maskini kuliko hizi za Sasa ambazo zimefeli nchi za dunia ya kwanza.
Tukumbuke pia vifo vinavyotokana na balaa la njaa vimeongezeka zaid ya mara tatu ukilinganisha na Kabla ya Janga hili la COVID kwa mujibu wa takwimu za UN.
Serikali pia idhibiti kiwango cha mauzo ya chakula kama Mahindi,Mchele na Maharage kwa nchi za nje ilikua kuchukua tahadhari Zaid kutokana na mwenenendo huu wa kiCOVID COVID.