#COVID19 Marufuku hospitali za umma, binafsi kulipisha chanjo ya COVID-19

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa angalizo kwa wasimamizi wa chanjo kutolipisha watu fedha kwani chanjo hizo ni bure.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi wakati wa usambazaji wa chanjo hizo kwenda mikoa mbalimbali nchini tukio lililofanyika bohari kuu ya dawa MSD, Kurasini Dar es salaam.

Akitoa rai kwa wasimamizi, Prof. Makubi, amesema utoaji wa chanjo hizo kwenye hospitali za Umma na binafsi utatolewa bila kulipisha gharama za chanjo.

"Naelekeza kwa huu mgao wa Covax Facility ni marufuku Hospitali za umma au binafsi kulipisha Wananchi gharama yoyote katika zoezi hili la chanjo na lifanyike kwa uadilifu na kwa haki kwa walengwa wa sasa." amesema Prof. Makubi.

Ameongeza kuwa, pamoja na serikali kufanikisha upatikanaji wa chanjo hizo na kuanza kuchanja Wananchi, Wizara ya afya inaendelea kuwashauri wananchi kujikinga na UVIKO-19.

"Kwa kuzingatia kanuni za UVIKO-19, tunapaswa kunawa mikono, kuvaa barakoa, kukaa umbali za mita moja au zaidi, kuepuka misongamano na kufanya mazoezi.

Aidha, amesema ugawaji wa chanjo umezingatia taarifa ya visa vya wagonjwa waliohisiwa kuwa na UVIKO-19, idadi ya walengwa kwa kundi la kipaumbele pamoja na idadi ya chanjo zilizopatikana kwa sasa.

Katika hatua nyingine serikali kupitia TMDA, Maabara ya Mkemia Mkuu, Maabara kuu ya Taifa na Vyombo vingine vyote vimehakiki na kujiridhisha usalama na ubora wa chanjo za Janssen kutoka Kampuni ya Johnson & Johnson nchini Marekani.

Prof. Makubi amebainisha kuwa, kutokana na Mwongozo wa Chanjo wa Taifa dhidi ya Ugonjwa wa UVIKO-19, Shirika la Afya Duniani (WHO), maelekezo ya Covax Facility na upungufu wa uzalishaji wa chanjo toka viwandani, Chanjo hizo kwa sasa zinatolewa kwa kufuata vipaumbele vya makundi yenye uhitaji mkubwa.

"Makundi ambayo yataanza chanjo ni pamoja na: Watumishi wa sekta ya Afya, Watu wazima umri wa miaka 50 na kuendelea na Watu wenye magonjwa. Kama ambavyo Serikali imekuwa ikieleza, uchanjaji kwa makundi yote nchini ni wa hiari au huru kwa kila mwananchi.

Kwa kuwa chanjo zilizopokelewa kwa sasa hazitoshelezi walengwa wa makundi yote nchini, makundi mengine yatapata chanjo katika awamu inayofuata, mara zitakapowasili." amesema Prof. Makubi.

Hadi sasa Serikali inategemea kutoa chanjo kwa makundi yanayolengwa kuanzia Agosti 3,2021, siku ya Jumanne, katika vituo 550 vya kutolea huduma katika mikoa yote ya Tanzania bara ambapo Orodha ya vituo hivyo inapatikana pia katika tovuti ya wizara; www.moh.go.tz.

Wananchi wote walengwa, wanaotaka kuchanjwa kwa hiari yao, huku wakitakiwa; kujihakiki kama wapo ndani ya makundi matatu ya walengwa kwa sasa.

Ippmedia
 
Hivi wanategemea IST na Aga Khan wakubali kuchanja bure? Kwa chanjo za watoto wanakubaligi kama mtoto alizaliwa hospitali yao hata hii wataweka masharti yao tu.
 
Is it practical? Nani anagharamia cost ya kuweka madaktari/manesi wa ku administer hizo chanjo?
Mishahara mikubwa waliyonayo pamoja na Posho zao ambazo zimeongezeka Kisiri unadhani haziwatoshi Wao Kutekeleza Wajibu wao huo ( huu ) wa Kiutendaji wa Kuhudumia Watu?
 
Kwani madaktari na manesi si wapo siku zote? Au sijaelewa point yako mkuu nieleweshe
Anachoongelea ni extra cost kwa hospital hasa binafsi hii ya kuchanja corona ni extra duty haikuwemo kwenye kazi zao za kawaida

Itahitaji waongeze manesi na madaktari sababu kazi zitaongezeka na manesi hufanya kazi chini ya madaktari

Swala la cost lazima litaibuka utekelezaji ukianza
 
Hivi wanategemea IST na Aga Khan wakubali kuchanja bure ? Kwa chanjo za watoto wanakubaligi kama mtoto alizaliwa hospitali yao hata hii wataweka masharti yao tu.
Kwani hao ist wanaagiza wenyewe chanjo au serikali ndio inawapelekea?
 
Kimsingi wanaojitolea kushiriki kwenye majaribio ya chanjo ndo wanatakiwa kulipwa fidia (compensation), sasa wameigeuza ionekane kwamba wanapewa msaada wa chanjo ya bure wakati siyo chanjo iliyopata final approval. Msitufanye hatuna akili aiseee!
 
Kimsingi wanaojitolea kushiriki kwenye majaribio ya chanjo ndo wanatakiwa kulipwa fidia (compensation), sasa wameigeuza ionekane kwamba wanapewa msaada wa chanjo ya bure wakati siyo chanjo iliyopata final approval msitufanye hatuna akili aiseee!
Kwani haya bado majaribio?
 
Kimsingi wanaojitolea kushiriki kwenye majaribio ya chanjo ndo wanatakiwa kulipwa fidia (compensation), sasa wameigeuza ionekane kwamba wanapewa msaada wa chanjo ya bure wakati siyo chanjo iliyopata final approval msitufanye hatuna akili aiseee!
Kwani mkuu chanjo si hiari?!!wewe na familia yako ipotezeeni tu, wale wako tayari waende wakachome, ikipata final approval ndio utachoma!

Kwani naona mnatumia nguvu nyingi sana kuikataa , achaneni na fikra za meko, japo najua kuna muda utafika tu utaitafuta mwenyewe!

Halafu nashangaa sana kwenye hili yaani mijitu ambayo haina hata elimu/masikini ndio imeshupalia eti wazungu wanataka kutuua!!kisa sumu ya meko bado anayo kichwani!!
 
Kwani mkuu chanjo si hiari?!!wewe na familia yako ipotezeeni tu, wale wako tayari waende wakachome, ikipata final approval ndio utachoma!!kwani naona mnatumia nguvu nyingi sana kuikataa...
Nafsi zetu zinatusuta kutotimiza wajibu wetu kwa jamii kutokuwafahamisha tulicho na uelewa nacho, kodi za wanyonge wa kitanzania ndo zimetusomesha tukawa na maarifa tuliyo nayo sasa.

Kwa hiyo tunachofanya ni kurudisha fadhila kwa jamii ya watanzania wenzetu, wewe kama una maslahi binafsi kwenye hizi chanjo za majaribio huna uhalali huo wa kunifunga mdomo nisiwaelimishe watanzania wanyonge wenzangu ambao wanahitaji kupata taarifa sahihi zisizo na kificho au kuegemea maslahi yoyote.
 
Hivi wanategemea IST na Aga Khan wakubali kuchanja bure ? Kwa chanjo za watoto wanakubaligi kama mtoto alizaliwa hospitali yao hata hii wataweka masharti yao tu.
 
Kwani hao ist wanaagiza wenyewe chanjo au serikali ndio inawapelekea?
Chanjo ni bure ila huduma ya kutoa chanjo sio bure, nani anawalipa hao ma nurse, accomodation facilities na usumbufu unaokuja na kuwa kundi kubwa la watu hospitali yako.
 
K
Is it practical? Nani anagharamia cost ya kuweka madaktari/manesi wa ku administer hizo chanjo?
Kuna mzigo wa kueleweka toka marekani bila shaka. Kama Biden ametangaza dau la dola 100 kwa kila mmarekani atakayekubali kuchanjwa atashindwaje kuleta mzigo wa kueleweka huku kwetu. Inaelekea "tunapendwa" sana!! Akili ya kuambiwa changanya na ya kwako! Tatizo ni kwamba huo mzigo utakuwa ni mkopo wa muda mrefu wenye riba!! Watoto wetu tutawaachia mzigo mkubwa usiobebeka!! Ni utumwa!!!
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Back
Top Bottom