Naomba msaada kimawazo kuhusu suala la jina katika akaunti ya Benki

Attelan

JF-Expert Member
Oct 12, 2023
434
701
SUMMARY:
Jambo liko hivi, mhitimu wa kidato cha sita wa mwaka huu 2023 baada ya kuanza kufanya maombi ya Mkopo wa chuo kikuu alifungua akaunti ya benki kama yalivyo matakwa ya Bodi ya Mkopo wa Elimu ya juu (HESLB).

Baada ya kufungua akaunti jina la katikati lilionekana kuwa lingine (Badala ya John lilisomeka Joseph), baada ya kuongea na benki alishauriwa kuenda NIDA ambako angefuata taratibu za kurudisha jina kama lilivyokuwa awali kwani ilionekana mistake ilifanyika wakati wa ujazaji wa taarifa zake huko huko NIDA.


Hata mchakato wa kutafuta namba ya NIDA aliuanza baada ya kumaliza mtihani wa kidato cha Sita. Sasa baada ya kuenda benki kufanya usajili wa Akaunti jina la katikati likasoma lingine, kutoka John nakuwekwa Joseph na hapo akapewa na kadi kabisa (Jina la benki kapuni). Baada ya kuuliza kuhusu namna ya kubadili jina na kulirudisha kuwa John aliambiwa aende tena kwenye Ofisi za NIDA ili kufuatilia mabadiliko ya Jina, baada ya kumaliza Application za mkopo na dirisha kupita hatimaye NIDA wakawa wamebadilisha jina kutoka Joseph na kulirudisha kuwa John.

Kwakuwa issue ya mkopo ilitakiwa sehemu ya namba ya akaunti namba ya benki kujazwa, mhitimu huyu alijaza akaunti namba akijua inawezekana kubadilishwa jina kama alivyoambiwa na Afisa wa Benki. Sasa mkopo umerudi kapata allocation na jina NIDA wamebadili (Hii ni baada ya kufuatilia NIDA kwa muda kiasi) na kulirudisha kuwa John, shida imegeuka Benki wanadahi inabidi aende Mahakamani kuapa kuwa jina la kati la John ni lake.

Kwakuwa ni dogo tu, niliamini uwenda alishindwa kujieleza na ndio maana akaishia kupewa ushauri huo. Sasa nimekuja kwenu kupata ushauri, je ndivyo ilivyo kwamba anatakiwa akaape mahakamani au Benki wanaweza kulibadilisha jina la akaunti kwakuwa kwasasa wakijaza namba ya NIDA litasoma jina la mhitimu kamili?
 
SUMMARY:
Jambo liko hivi, mhitimu wa kidato cha sita wa mwaka huu 2023 baada ya kuanza kufanya maombi ya Mkopo wa chuo kikuu alifungua akaunti ya benki kama yalivyo matakwa ya Bodi ya Mkopo wa Elimu ya juu (HESLB)...
Kama NIDA walisha badili, aende mahakamani kama walivyomueleza. Ni utaratibu wa kawaida kwa Bank.
 
Back
Top Bottom