Katriel
JF-Expert Member
- Nov 1, 2014
- 272
- 934
Mwenyewe nasubiri kuhurumiwa 🤣🤣🤣Hutaki kuwa mama huruma🤣🤣🤣🤣
Mwenyewe nasubiri kuhurumiwa 🤣🤣🤣Hutaki kuwa mama huruma🤣🤣🤣🤣
Ah jamani kisa na mkasa? Au tako hamna?Mwenyewe nasubiri kuhurumiwa 🤣🤣🤣
Sina tako nimenyooka kama mnyoo 😂😂Ah jamani kisa na mkasa? Au tako hamna?
Sasa nyie sii ndio wife material mnaoolewa so labda wee huchangamkii fursaSina tako nimenyooka kama mnyoo 😂😂
Asante mkuu mungu akubarikiKwanza kabisa pole, usiwe pressurized na kuona km looser sababu your not ni kitendo cha muda tu kila kitu kitakaa sawa, kwanza kabisa nakusisitiza yaani hili ukilifanya utaona mabadiliko makuu...jaribu kuweka hata alarm uwe unaamka usiku mida ya kuanzia saa saba na nusu usiku mpk saa tisa usiku..OMBA MUNGU, I mean it OMBA MUNGU, kwa nini mida hiyo? Sababu ni muda ambao anga limetulia upande wa Mungu ila upande wa nguvu za giza mambo ndio yanashamiri hivyo ni muda mzuri sana wa Mungu kusikia sala zako.
Omba Mungu utavyoweza tena bila formula yaani omba tu mlilie Mungu kwa yote yanayokusibu..omba akuvushe na shukuru Mungu kwa imani kua atakufanikisha tu, yawezekana usijue utafanikiwa vipi ila trust me atakufanikisha tu.
Pili, epuka kukaa au kuhang out na watu waliokata tamaa au wanaokukatisha tamaa sababu kwenye maisha kila mtu ana muda wake wa kufanikiwa...pia penda kukaa na company ya watu waliofanikiwa hata km haupo nayo karibu jaribu kwenda kwenye bar za maana au lounges, nimesema za maana sababu hata watu wataokua wanafika hapo ni wa maana pia hata km ww si mnywaji we nenda tu jichanganye na km unakunywa nunua hata bia zako mbili mwezi hautapita bila kupata mchongo wa maana au hata mawazo ya maana.
Tatu, wanawake tupo wengi ila wachache ndio sahihi so usitumie nguvu nyingi usije ukaokota tapeli..we relax tu jenga urafiki na mabinti tofauti anza na mazungumzo ya kawaida ya urafiki mwanamke sahihi utamjua tu kwa mwenendo na matendo yake...RELAX,mke utapata na watoto utapata.
Mwisho, ukiwa unaomba Mungu usisahau kuomba kufunguliwa vifungo vyovyote km unavyo unavyojua na usivyovijua, omba kibali cha kukubalika mbele za watu na omba ulinzi dhidi ya mabaya yote juu yako..niamini ninachokwambia Mungu anasikia.
All the best, I advised all of that from my personal experience.
Mkuu nimekuuliza wewe ni wangapi kuzaliwa?Kondoa
Pambana aiseeee, usiwe mwenye kuchagua kazi yoyote inayokuja piga, hakuna mwanamke atampenda mwanaume asiye na kitu kabisa, wanahitaji mwanaume mwenye kitu kiwe kikubwa au kidogo Ili mradi unakitu utapata mwanamke atakuzalia na mtoto kabisa maana atakuwa na uhakika, lakin kama huna anaogopa kuja kulea peke yake, kwahiyo pambana, hiyo miaka isikutishe kikubwa uzima unao pambana tu!Mimi ni kijana wa miaka 33 sina mke wala mtoto mpaka dakika hii na kila jambo ninalopanga linayeyuka na sio kwa mahusiano tu hadi mipango yote ya kimaisha.
Kwa kweli naumia sana tafadhali naombeni ushauri wenu wa aina yoyote ule.
Watoto wa kwanza na wa mwisho wanapitia changamoto nyingi mno. Jipe moyo utayashinda.Wa 6 na ndio wa mwisho
Mkuu mshukuru sana MUNGU umefika hapo narudia tena mshukuru sana MUNGU,Ibada jamani Anko Jei inakusaidiaje kukujenga kiuchumi Mkuu wangu? Mbona watu wangu mnakosea sana katika hilo? Afya njema. Kuchapa kazi na mipango mizuri ndio kunakujenga kiuchumi mkuu wangu.
Mkuu uko sahihi saana ,nimemwambia kama hajapitia huko hawezi kuelewa hili,,yeye amshukuru MUNGU TU inatoshaSijaongelea interm of mali mkuu, thats more spiritual kwa namna flani tuna background tunayofanana kimalezi ila...nilikua km wewe onve upon a time ila kuna yaliyonikuta na nashukuru kwa uwezo wa Mungu nilipita so ninavyosema kuhusu Mungu na kibali naelewa nini namaanisha mkuu.
Juhudi, mipango mizuri, na afya nzuri inayotoka kwa Mungu peke yake. Mungu anatupa afya, mengine yote ni sisi wenyewe. Fuatilia posts zote za mjadala huu labda utaelewa.Mkuu mshukuru sana MUNGU umefika hapo narudia tena mshukuru sana MUNGU,
sio juhudi na mipango yako mizuri pekee vilivyokufikisha hapo,
Kuwa na Mipango sahihi,,kufanya kazi kwa bidii saana pekee hakumfanyi mtu afanikiwe .
Kufanikiwa ni KIBALI,
Na sio kila mtu ana KIBALI,
Watu wana mipango mizuri saana,watu wanajituma saana ,usiku na mchana,
Huwezi kuelewa hili la mtoa mada kama haujapitia ,,utaishia kumlaumu tu mtoa mada.
Japo sikatai uvivu na mipango mibay vinaweza kuchangia,,lakini sio kiasi hicho,
Kwaayo wakuu wanapomshauri mtoa mada amrudie MUNGU wanajua kuwa juhudi na mipango mizuri pekee havitoshi kufanikiwa.
Mimi nimepitia sana. Kuzaliwa maskini na kutokuwa na Baba ni mchezo sasa? Na ndugu wanasema ww ni mvuta bangi na kwamba umeacha shule kizembe... kumbe nilikuwa nashughulikia USA visa. Ndugu wakanitenga hadi nikalala chini ya mti au kulala club wakati napambania USA visa sababu sikuwa na ndugu hata mmoja wa kwenda kwake? Au kwenda USA miaka kibao mambo yanavurugika HADI MTU UNATAKA KUJIUA. Japo ndio unakumbuka ulikotoka unasema nitatoboa tu.Mkuu uko sahihi saana ,nimemwambia kama hajapitia huko hawezi kuelewa hili,,yeye amshukuru MUNGU TU inatosha
Ni kweli kabisa mkuu yaani inafikia hatua mpaka unasema hivi mungu ananijua kweli. Japokuwa ni kama namkufuruMimi nimepitia sana. Kuzaliwa maskini na kutokuwa na Baba ni mchezo sasa? Na ndugu wanasema ww ni mvuta bangi na kwamba umeacha shule kizembe... kumbe nilikuwa nashughulikia USA visa. Ndugu wakanitenga hadi nikalala chini ya mti au kulala club wakati napambania USA visa sababu sikuwa na ndugu hata mmoja wa kwenda kwake? Au kwenda USA miaka kibao mambo yanavurugika HADI MTU UNATAKA KUJIUA. Japo ndio unakumbuka ulikotoka unasema nitatoboa tu.
Msione sababu mtu amefanikiwa eti hajapitia changamoto. Mambo ya kufukuzwa kwa kufunguliwa mbwa wakati namfuatilia sponsor wangu wa Ubalozini?
Namshukuru Mungu sana sababu hela yangu ni HALALI 100% . Ni matokeo ya kuchapa kazi na mipango mizuri.. na afya nzuri kutoka kwa Mungu. Majumba kibao. Magari kibao. Investments kadhaa Tanzania na nje. Na nina makazi Tanzania na nje ya Tz pia. Na bado Mungu anaendelea kunibariki. Ila nimevipata vyote kwa kupambana. Najua kabisa formula, kwa hio ninavyosikia mtu mnasema hivyo.. NAJUA MNAKOSEA.. sababu najua barabara niliyoipitia hadi nikafanikiwa.