Naomba Majibu Tafadhali: 'Mfumo imara' ni nini?

kabyemela95

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
791
1,000
Mfumo Imara katika nchi ni mfumo wenye "Checks and Balances" ambazo zinazuia mtu mmoja mwenye mamlaka kufanya anavyojisikia yeye tu badala ya vile katiba, sheria na miongozo ya nchi inavyoelekeza. Lakini pia ni mfumo ambao unahakikisha kuwajibika kwa kiongozi endapo ataweza kuwa kichwa ngumu au jiwe kuzivuka checks and balances zinazopaswa kumdhibiti...
And also kuhusu Trump, ule uchaguzi umeibiwa live bila chenga,bahati yake mbaya kwasababu chama alichokuemo na wapinzani wake walikua hawamtaki...Usiwe unachungulia headline tu za CNN ,JARIBU KUFUATILIA kidogo..
 
Mpatuka

JF-Expert Member
Nov 15, 2015
650
1,000
KWA maelezo ya wadau hapo juu hasa kuhusu mfumo imara, kwa lugha nyepesi naomba nitoe mfano huu. Gari aina ya IST inamfumo ambao hautabadilika kwa dereva yoyote yule atakayeshika usukani kuongoza safari, mwendo utategemeana na ujuzi wa dereva katika kucheza na usukani sambamba na kukanyaga mafuta.

Kutokana na hilo inakuwa rahisi kumpima dereva anayetuwahisha au anayetuchelewesha katika safari. Hivyo katika kuchagua mfumo pia kwa mfano huu umakini unahitajika vipi tukichagua mfumo wa IST badala ya FERRARI?

Kwa maana rahisi hata tukawa na mfumo bora bado hatua zetu zitamtegemea dereva wetu kufikia nchi ya ahadi.
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
5,697
2,000
Si kuna sheria ya kodi? Mbona watu wanakwepa kodi kama unafikiri maana ya mfumo ni sheria?

Sheria bila uwepo wa watu makini wa kuhakikisha sheria ifuatwe sheria itabaki kuwa maandishi kwenye karatasi. Kinyume chake unaweza kuwa na kiongozi imara akaweka taratibu zake na baada ya muda wa kutosha hizo taratibu zinageuka utamaduni wa watu.
Mfumo ni sheria, nimeshakwambia hapo juu kama unadhani mfumo ni mtu vipi huyo mtu akiondoka huo mfumo wake utabaki? na huo mfumo wa kumtegemea mtu utakuwa ni mfumo dhaifu sana, haufai.

Kama sheria zipo lakini watu hawataki kulipa kodi wakamatwe washtakiwe, mbona simple, kama hawashtakiwi huo ni uzembe wa watu walioko kwenye huo mfumo kwasababu sheria zimeshaoanisha adhabu kwa wasiolipa kodi.
 
cool d

JF-Expert Member
Jan 20, 2015
993
1,000
Mfumo imara ni kufanya taasisi ziwe imara na zenye kutoa maamuzi kwa wakati, mfano mahakama mfumo wao wanajiendesha wenyewe na kuwekewa system au muundo wa kutatua kesi kwa haraka bila kutegemea maelekezo ya muhimili mwingine inakuwa na jopo lake labda la kukaa kila mwezi nakutatua kesi ngumu na kutoa maamuzi haraka bila kuingiliwa na ikitokea makosa ni wao wanawajibika hata kujiuzulu nafasi zao, na Bunge, Polisi hivyo hivyo wanakuwa na mifumo na ikitokea makosa wanawajibika kujiuzulu Ili kuonyesha imani yao kwa wananchi.
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
5,697
2,000
KWA maelezo ya wadau hapo juu hasa kuhusu mfumo imara, kwa lugha nyepesi naomba nitoe mfano huu. Gari aina ya IST inamfumo ambao hautabadilika kwa dereva yoyote yule atakayeshika usukani kuongoza safari, mwendo utategemeana na ujuzi wa dereva katika kucheza na usukani sambamba na kukanyaga mafuta...
Hapa wasipoelewa ndio basi tena, inshort lazima pawepo na instructions zitakazowaelekeza watu wanaoongoza hizo taasisi kuyajua majukumu yao na kuyatekeleza bila kujali nani anaongoza taasisi hizo kwa wakati husika, yeyote atakayekuja kuongoza majukumu yake atayakuta pale kisheria.
 
dolevaby

JF-Expert Member
Aug 25, 2013
12,110
2,000
Nafikiri humaanisha kwamba kiongozi awepo pale kama robot, afu nchi, taasisi na idara zake vijiendeshe automatic kulingana na sheria mama ya nchi na sheria zinginezo. Kazi ya rais iwe ni kupewa taarifa, kushauriwa na kutoa maamuzi kulingana na alivyoshauriwa...
Jiambie kuwa UMJINGA mfumo imara unaleta wezi umeshughulisha ubongo wako vzr! au ndio ujinga mlimezeshwa na jamaa yenu kumbe alikuwa anagawana na genge lake

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
zimmerman

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
905
1,000
Safi sana mkuu umetafsiri vema kabisa na mimi nimekuelewa vema,Welldone na kwa wale ambao sio wavivu wa kujisomea na kutafiti,someni na fanya utafiti kuona ni jinsi gani President Madiba alitengeneza serikali yake na kuacha legancy ya kuwa moja ya nchi zenye mifumo imara ya kusaidia utawala bora,aliifanya nchi iwe ya kikatiba na mahakama ya katiba ndio inayotafsiri sheria za nchi na hakuna aliyejuu ya sheria ,ndio maana sitting president au ex presidents wote wanaweza kushitakiwa mahakamani na elewa yeye mwenyewe(Madiba)alisimama kizimbani akiwa president na case ikamshinda!
Huo mfano wa South Africa ulioutoa ni mfano bora kabisa unaoonyesha kwamba watu wabovu hutumia mifumo kama kichaka cha kufanya uovu wao. Si unaifahamu state capture ya SA ambako wajanja wenye maslahi binafsi walitumia mifumo hiyo hiyo kufanya ufisadi wa kiwango cha juu kabisa. SA visa vya ufisadi haviishi pamoja na hizo unazoita strong institutions zao. Sababu ni nini? Sababu ni kwamba hata hiyo mifumo inaongozwa na wanadamu, kufanikiwa kumshtaki rais si mwarobaini wa matatizo yenu, hasa watu wakiwa wabovu tu.
 
zimmerman

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
905
1,000
Mfumo ni sheria, nimeshakwambia hapo juu kama unadhani mfumo ni mtu vipi huyo mtu akiondoka huo mfumo wake utabaki? na huo mfumo wa kumtegemea mtu utakuwa ni mfumo dhaifu sana, haufai.

Kama sheria zipo lakini watu hawataki kulipa kodi wakamatwe washtakiwe, mbona simple, kama hawashtakiwi huo ni uzembe wa watu walioko kwenye huo mfumo kwasababu sheria zimeshaoanisha adhabu kwa wasiolipa kodi.
Na mimi nimeshakwambia kwamba sheria ziwepo tu, na zipo tu. Hivi yule mzee aliyesema ili kuendelea tunahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora, kwa nini alianza na watu, na kwa nini hakuweka sheria? Aina ya watu na aina ya viongozi ni determinant kubwa ya ufanisi katika nyanja zote.

Kama mtu bora kafa kama nchi yetu ilivyompoteza kiongozi mahiri kuwahi kuwepo katika nchi yetu hilo ni bonge la hasara. Sometimes nchi au makampuni huyumba inapotokea kiongozi imara au CEO bora anapoondoka. Sheria za nchi ikiwemo mambo ya uchaguzi haviwezi kuguarantee kwamba replacement atafanya vizuri au zaidi. Umuhimu wa mtu hauwezi kuwa understated.
 
cool d

JF-Expert Member
Jan 20, 2015
993
1,000
Hapa wasipoelewa ndio basi tena, inshort lazima pawepo na instructions zitakazowaelekeza watu wanaoongoza hizo taasisi kuyajua majukumu yao na kuyatekeleza bila kujali nani anaongoza taasisi hizo kwa wakati husika, yeyote atakayekuja kuongoza majukumu yake atayakuta pale kisheria.
Ndiyo inavyokuwa yaani JOB description ndo mtu anakabidhiwa na siyo ilani ya Chama hizo zinakuwa kwa wanasiasa pekee, ikitokea tatizo kwenye taasisi yako hata Raisi hakusemei Kama sasa unawajibika tu kwa kujiuzulu unapisha wengine, hata haya matatizo ya uzembe tusingeyasikia maana wananchi wangekua wanapiga kelele Kama mtu hajawajibika.
 
zimmerman

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
905
1,000
Hapa wasipoelewa ndio basi tena, inshort lazima pawepo na instructions zitakazowaelekeza watu wanaoongoza hizo taasisi kuyajua majukumu yao na kuyatekeleza bila kujali nani anaongoza taasisi hizo kwa wakati husika, yeyote atakayekuja kuongoza majukumu yake atayakuta pale kisheria.
Kama ingekuwa job description inatosha hata wewe denooJ ungekuwa Rais wa nchi hii.
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
5,697
2,000
Na mimi nimeshakwambia kwamba sheria ziwepo tu, na zipo tu. Hivi yule mzee aliyesema ili kuendelea tunahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora, kwa nini alianza na watu, na kwa nini hakuweka sheria? Aina ya watu na aina ya viongozi ni determinant kubwa ya ufanisi katika nyanja zote.

Kama mtu bora kafa kama nchi yetu ilivyompoteza kiongozi mahiri kuwahi kuwepo katika nchi yetu hilo ni bonge la hasara. Sometimes nchi au makampuni huyumba inapotokea kiongozi imara au CEO bora anapoondoka. Sheria za nchi ikiwemo mambo ya uchaguzi haviwezi kuguarantee kwamba replacement atafanya vizuri au zaidi. Umuhimu wa mtu hauwezi kuwa understated.
Lazima aanze na watu kwasababu watu ndio wanaweka sheria za kuwaongoza, kama unadhani hayo maneno yake yalikuwa ndio mfumo wenyewe unakosea, coz Mkapa alikuja na yake, Mwinyi akaja na ruksa, Kikwete nae akaja na chake, sasa huo ni mfumo wa aina gani unaobadilika badilika hivyo?

Mfumo lazima sheria iwepo, na kama sheria zipo hazifuatwi huo ni uzembe wa watendaji, mfumo sio mtu mmoja kama unavyolazimisha ndio maana hata kwenye football kuna 4-4-2 au 4-3-3 na mingineyo, lakini hawa wachezaji hupokea maelekezo toka kwa kocha wao namna ya kufanya wakiwa uwanjani, kama ambavyo sheria na miongozo hutakiwa kutoa maelekezo kwa watendaji wa kwenye taasisi wanazoziongoza.
 
Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
2,145
2,000
Huo mfano wa South Africa ulioutoa ni mfano bora kabisa unaoonyesha kwamba watu wabovu hutumia mifumo kama kichaka cha kufanya uovu wao. Si unaifahamu state capture ya SA ambako wajanja wenye maslahi binafsi walitumia mifumo hiyo hiyo kufanya ufisadi wa kiwango cha juu kabisa. SA visa vya ufisadi haviishi pamoja na hizo unazoita strong institutions zao. Sababu ni nini? Sababu ni kwamba hata hiyo mifumo inaongozwa na wanadamu, kufanikiwa kumshtaki rais si mwarobaini wa matatizo yenu, hasa watu wakiwa wabovu tu.
Umetoa mfano mzuri wa state capture ila unasahau kuwa watu wameanza kupelekwa mahakamani kwa ufisadi huo na sitting president naye ataenda kutoa ushahidi wake,je hayo yanaweza kutokea hapa kwetu?kipindi cha awamu ya pili serikali yetu ilishikwa je kuna watu waliwajibika?kumbuka chavda,ladwa,Patel s etc etc hakuna aliyewajibika maana mfano imara w kusaidia utawala bora hatukuwa nao.
 
Sang'udi

JF-Expert Member
May 16, 2016
2,809
2,000
Mfumo imara ni muunganiko wa watu, rasilimali, sera na sheria tofautitofauti wanaofanya kazi kwa umoja na uhuru ili kufikia lengo la taasisi husika kwa ufanisi na weledi wa hali ya juu; kama tulivyoona katika kipindi cha Rais bora wa nchi yetu, Hayati Dr. JPM.
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
13,867
2,000
Mfumo upo tena mzuri,Tanzania kuna mamlaka za kudhibiti kila kitu, bodi za kila aina ya kitu, mahakama zinazosikiliza kila aina ya kosa,serikali iliyojaa wizara ya kila sekta...tulichokosa ni uadilifu tu, kila mtu angesimamia kazi yake kwa usahihi na bila kuogopana ,tungekua mbali...Kwahiyo unavoniambia hakuna mfumo sikuelewi, sema kuna watu dhaifu
Mnachekesha kweli kweli. Nimesoma comments nyingi lakini watu hawaelewi maana ya mfumo imara. Wewe unajichanganya kabisa. Mfumo imara unamfanya kila mtu kuwajibika kwenye majukumu yake.

Usipokuwa mwadilifu kwenye mfumo imara automatically unapata ''zawadi yako''. Mkitaka kujua maana ya mfumo imara angalia nchi kama USA.

Kwa mfano Trump aliposhindwa uchaguzi pamoja na kuwa rais na kutaka kubadilisha matokeo lakini alishindwa kwa sababu mfumo wa uchaguzi ni imara na hauwezi kuingiliwa. Kwa kifupi nchi inasemwa ina mfumo imara kama kila idara,taasisi na sekta za serikali zinafanya kazi zao kwa mujibu wa sheria na bila kuingiliwa na shinikizo la viongozi/idara/sekta nyingine.

Ukienda kwenye mhi,ili wa mahakama unakuta unafanya kazi kwa mujibu wa sheria na hauingiliwi na ushawishi kutoka nje. Bunge hivyo hivyo, taasisi ya rushwa, mashirika ya serikali n.k
 
slip way

Senior Member
Apr 11, 2021
166
250
Na mimi nimeshakwambia kwamba sheria ziwepo tu, na zipo tu. Hivi yule mzee aliyesema ili kuendelea tunahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora, kwa nini alianza na watu, na kwa nini hakuweka sheria? Aina ya watu na aina ya viongozi ni determinant kubwa ya ufanisi katika nyanja zote.

Kama mtu bora kafa kama nchi yetu ilivyompoteza kiongozi mahiri kuwahi kuwepo katika nchi yetu hilo ni bonge la hasara. Sometimes nchi au makampuni huyumba inapotokea kiongozi imara au CEO bora anapoondoka. Sheria za nchi ikiwemo mambo ya uchaguzi haviwezi kuguarantee kwamba replacement atafanya vizuri au zaidi. Umuhimu wa mtu hauwezi kuwa understated.
kiongozi imara gani anachakachua mpaka kura za wabunge wawe ccm peke yao.
 
zimmerman

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
905
1,000
Yaani nyie mnatoa mifano mizuri kabisa inayojenga hoja ya kwamba watu bora husaidia mifumo. Sasa unapotumia mfano wa 4-4-2 kwenye mpira wote tunafahamu kwamba ili huo mfumo ufanye kazi unahitaji wachezaji bora wenye talanta zao. Makocha hao hao husajiliwa na kutimuliwa mara kwa mara maana wenye timu zao hawaamini katika mifumo wanaamini katika kocha sahihi.

Turudi kwenye mada. Usiamini sana katika sheria, amini katika watu wanaosimamia hizo sheria. Nyerere aliposema katiba imempa Rais wa Tamzania madaraka makubwa kiasi kwamba ningeyatumia kikamilifu ningekuwa dikteta. Kwa nini hakuyatumia? Kwa sababu hakuwa dikteta. Tanzania haijawahi kuwa na rais dikteta hata kama katiba inawapa madaraka makubwa kuwa dikteta. Kwa nini hawajawa madikteta? Kwa sababu kwa asili zao hawakuwa madikteta. Hata JPM anayetuhumiwa kuwa alikuwa na tendency za udikteta bado hakuwa dikteta in a real sense ya udikteta.

Kwa nini mfumo unawapa nguvu ya kuwa madikteta na hawawi? Ni kwa vile mfumo si inshu sana. Inshu ni mtu. Mtu ana uwezo wa kugeuza mfumo mzuri on paper ukawa mbaya sana, na mtu ana uwezo wa kugeuza mfumo mbaya sana on paper ukawa mzuri.
 
mtolewa

JF-Expert Member
Jan 18, 2011
434
500
Nafikiri humaanisha kwamba kiongozi awepo pale kama robot, afu nchi, taasisi na idara zake vijiendeshe automatic kulingana na sheria mama ya nchi na sheria zinginezo. Kazi ya rais iwe ni kupewa taarifa, kushauriwa na kutoa maamuzi kulingana na alivyoshauriwa..
Hivi nyie CCM ufahamu huwa mnapeleka wapi? Au ndo ili uwe CCM lazima uwe mnafiki? Hivi kweli wewe hujui na huamini katika mfuko imara?
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
10,892
2,000
Kuna mahali nimekwambia hakuna mfumo?

Aliyeuliza swali ameuliza mfumo ni nini au Mfumo IMARA ni upi?

Kila nchi duniani ambazo zimekuwa na udikteta, vita,ukabila,double standards , rushwa ilyokithiri, kucheza na katiba na uovu mwingine zimekuwa na hivyo vitu yanaitwa bodi, tume, mahakama, bunge n.k. Suala sio uwepo wake tu, je mfumo uliopo unavifanya imara kwa kiwango gani ndio muhimu.

Mfumo upo tena mzuri,Tanzania kuna mamlaka za kudhibiti kila kitu, bodi za kila aina ya kitu, mahakama zinazosikiliza kila aina ya kosa,serikali iliyojaa wizara ya kila sekta...tulichokosa ni uadilifu tu, kila mtu angesimamia kazi yake kwa usahihi na bila kuogopana ,tungekua mbali...Kwahiyo unavoniambia hakuna mfumo sikuelewi, sema kuna watu dhaifu
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
10,892
2,000
Umeelewa kwanza maana ya mfumo imara ni nini kabla ya kurukia tawi lingine kama ngedere?
And also kuhusu Trump, ule uchaguzi umeibiwa live bila chenga,bahati yake mbaya kwasababu chama alichokuemo na wapinzani wake walikua hawamtaki...Usiwe unachungulia headline tu za CNN ,JARIBU KUFUATILIA kidogo..
 
zimmerman

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
905
1,000
Hivi nyie CCM ufahamu huwa mnapeleka wapi? Au ndo ili uwe CCM lazima uwe mnafiki? Hivi kweli wewe hujui na huamini katika mfuko imara?
Naamini zaidi katika kiongozi au mtu bora. Kiongozi bora anaweza hata kugundua wapi pana limitation za kimfumo ili zifanyiwe kazi. Kuongoza kwa kutumia "job description" tu nikitumia msemo wa commenter mmoja kuna undermine ubunifu wa kiongozi, na ndiyo chanzo cha utopolo wote. Nikupe mfumo bora, na wewe unipe mtu bora, bila shaka matokeo yetu yatakuwa tofauti sana.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom