Naomba Majibu Tafadhali: 'Mfumo imara' ni nini?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
11,789
2,000
Unafikiri kwa nini serikali zinachora mistari, na zinaweka vibao vya speed limit na Zebra barabarani?? Kwa sababu zinafahamu kuna watu wajinga kama wewe wanaoajali kuwahi tu kama ndilo jambo la msingi kwenye safari.
KWA maelezo ya wadau hapo juu hasa kuhusu mfumo imara, kwa lugha nyepesi naomba nitoe mfano huu. Gari aina ya IST inamfumo ambao hautabadilika kwa dereva yoyote yule atakayeshika usukani kuongoza safari, mwendo utategemeana na ujuzi wa dereva katika kucheza na usukani sambamba na kukanyaga mafuta. Kutokana na hilo inakuwa rahisi kumpima dereva anayetuwahisha au anayetuchelewesha katika safari. Hivyo katika kuchagua mfumo pia kwa mfano huu umakini unahitajika vipi tukichagua mfumo wa IST badala ya FERRARI.? Kwa maana rahisi hata tukawa na mfumo bora bado hatua zetu zitamtegemea dereva wetu kufikia nchi ya ahadi.
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
6,561
2,000
Yaani nyie mnatoa mifano mizuri kabisa inayojenga hoja ya kwamba watu bora husaidia mifumo. Sasa unapotumia mfano wa 4-4-2 kwenye mpira wote tunafahamu kwamba ili huo mfumo ufanye kazi unahitaji wachezaji bora wenye talanta zao. Makocha hao hao husajiliwa na kutimuliwa mara kwa mara maana wenye timu zao hawaamini katika mifumo wanaamini katika kocha sahihi...
Lazima kuamini kwenye sheria na sio kuamini kwenye watu, watu wanapita sheria zinazoongoza institutions hazipiti, sijui unapata shida gani kuelewa hili?

Nyerere, Mkapa, na Kikwete hawakuyatumia vibaya madaraka yao kiasi cha kuitwa madikteta vipi mbona Magufuli aliyatumia vibaya? kuwanyima watu haki zao (mikutano ya vyama vya siasa), kupora uchaguzi, utekaji, utesaji, na mauaji yote yalifanywa wakati wake, huo ndio mfumo unaoutetea?!

Nakushangaa bado tu unakuwa mgumu kuelewa mfumo imara haujengwi na mtu bali hujengwa na misingi inayoainishwa kwenye sheria za nchi, na kila mtawala atatakiwa kuifuata, na wala sio mapenzi binafsi ya viongozi ndio yaitwe mfumo.

Bye.
 
zimmerman

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
1,027
2,000
Lazima kuamini kwenye sheria na sio kuamini kwenye watu, watu wanapita sheria zimazoongoza institutions hazipiti, sijui unapata shida gani kuelewa hili?...
Nikushangae wewe usiyeona umuhimu wa mtu sahihi katika taasisi, nchi au hata dunia. Kipi katika historia ya binadamu kilianza, mtu au mifumo? Hata kwenye vitabu vya dini tunaambiwa Mungu aliumba mtu baadaye akamwekea sheria, sheria aliyokuja kuivunja baadaye, na inasemekana ndiyo maana tunakufa. Si kwamba mifumo si kitu au haifai, ila mifumo inategemea sana watu.

Bye.
 
MtamaMchungu

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
6,355
2,000
Taasisi au mifumo imara

1. Haingiliwi na wanasiasa au siasa
2. Inafanya kazi kwa kufuata katiba na sheria sio matamko.
3. Ina watu imara wenye integrity , wanaoweza kukataa kuyumbishwa
4. Kuna mifumo ya kuulinda uhuru wake

Mifano midogo.

Netanyahu ametuhumiwa, amechunguzwa na ameshitakiwa kwa makosa ya rushwa. Taasisi imara ziko kazini, kwamba polisi wanauwezo wa kepeleka notice kwa kiongozi wa serikali, kumhoji na baadae prosecutors kupeleka mashitaka mahakamani bila woga.

Richard Nixon wakati anapambana kujinasua na Watergate scandal, alianza kumwambia CIA director aseme ilikuwa mission ya CIA, director akagoma, alivyombia am your president director akamwambia kesho nakuletea resignation letter, Nixon akaufyata. Baadae akaenda kumpa amri Attorney General asimamishe uchunguzi, jamaa akagoma na ku-resign, Nixon akaenda kwa deputy wake nae hivyo hivyo kagoma na kuondoka. Alienda mpaka kwa mtu wa 4 kwenye Department of Justice, wote wanagoma na ku-resign. Akaja kumpata jamaa mmoja akasimamisha uchunguzi, lakini mpaka kufika hapo; Nixon alikuwa damaged beyond repair, watu wa chama chake wakamwambia meli inazama, you have to go.

Taasisi gani hapa kwetu ina watu jasiri namna hiyo? Hata Trump pamoja na ukichaa wake, systems zilikuwa zinambana. Tunaweza tukaanza na teuzi, watu wawe vetted na kamati za Bunge. Hata kama watapitishwa, tayari mnajua ni vilaza.

Kuna jamaa Trump alimteua kuwa judge, alipoenda Senate, alipigwa maswali na watu wa chama chake mwenyewe. Alichemka mpaka akasema, na ujaji siutaki.

PANAFRICA

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
201
250
Yaani nyie mnatoa mifano mizuri kabisa inayojenga hoja ya kwamba watu bora husaidia mifumo. Sasa unapotumia mfano wa 4-4-2 kwenye mpira wote tunafahamu kwamba ili huo mfumo ufanye kazi unahitaji wachezaji bora wenye talanta zao...
Rais wa awamu ya NNE Mhe.Jakaya Kikwete alitambua umuhimu wa kujenga misingi imara ya kiutawala kwa maslahi mapana ya nchi, akaanzisha mchakato wa katiba mpya ambayo ndiyo sheria mama ambayo ingejenga misingi imara ya kitaasisi.

Aliishia kupiga u-turn kwa sababu anazozijua yeye, bunge la katiba likatumia pesa nyingi za walipa kodi bila matokeo tarajiwa.
Naamini kabisa kuwa atakuwa anajutia maamuzi yake na washauri wake kwani angeteneza legacy ambayo ingeenda vizazi hadi vizazi, hii inaitwa lost opportunity.

Naamini alishauriwa vibaya na wahafidhina wasioamini kwenye taasisi imara kwa maslahi yao binafsi na vizazi vyao. Mhe. Rais mama yetu Samia Suruhu Hassan anayo nafasi ya kuacha legacy,tumuunge mkono mwanzo wake unaonesha kuwa ana nia njema kabisa ya kuwatumikia na kuwavusha watanzania kuelekea kwenye nchi yenye maziwa na Asali.
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
6,561
2,000
Rais wa awamu ya NNE Mhe.Jakaya Kikwete alitambua umuhimu wa kujenga misingi imara ya kiutawala kwa maslahi mapana ya nchi, akaanzisha mchakato wa katiba mpya ambayo ndiyo sheria mama ambayo ingejenga misingi imara ya kitaasisi....
Jamaa mgumu sana kuelewa, labda ataelewa kesho.
 
MtamaMchungu

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
6,355
2,000
Yaani nyie mnatoa mifano mizuri kabisa inayojenga hoja ya kwamba watu bora husaidia mifumo. Sasa unapotumia mfano wa 4-4-2 kwenye mpira wote tunafahamu kwamba ili huo mfumo ufanye kazi unahitaji wachezaji bora wenye talanta zao. Makocha hao hao husajiliwa na kutimuliwa mara kwa mara maana wenye timu zao hawaamini katika mifumo wanaamini katika kocha sahihi...
Ukitegemea busara za mtu nayo ni tatizo. Unadhani CAG Assad bila mfumo imara wa kumlinda angeweza kupona wakati wa Magufuli? Pamoja na hasira zake zote, Magufuli alisubiri mpaka mkataba ukaisha, akagoma ku-renew.

Huo ndio mfumo imara, kwamba utafanya kazi yako bila kuogopa hata kama rais hakupendi
 
Mpatuka

JF-Expert Member
Nov 15, 2015
703
1,000
Unafikiri kwa nini serikali zinachora mistari, na zinaweka vibao vya speed limit na Zebra barabarani?? Kwa sababu zinafahamu kuna watu wajinga kama wewe wanaoajali kuwahi tu kama ndilo jambo la msingi kwenye safari.
hakukua na haja ya kuniita mjinga kiongozi katika familia yako lakini. Mfano wangu ni mtambuka sana kiasi kwamba hata mimi najua sijaweka nyama za kutosha ili mwelevu Kama wewe unielewe. Ila jambo la msingi ni tumepigwa sana mpaka sasa tulitakiwa kuwa donor country. Nukuu hiyo ndiyo kuchelewa kwenyewe huko.
 
Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
15,611
2,000
Wafuasi wa hicho kitu kiitwacho "mfumo imara" ni wale watu wavivu na dhaifu kiutendaji. Wasioamini katika uongozi. Watu kaliba ya yule CAG mstaafu aliyezinduka juzi akasema angalau asilimia 60 ya watumishi wa umma hawana uwezo stahiki...
Hata hujui unachokitetea,contradictions kibao,anyway unamsemea Kakoko yupi huyo aliefanya vizuri bandari na huo uzuri gani alioufanya au kwa zile data za kupika bila kusahau ufisadi walioifanya wakishirikiana na mwendazake?
 
Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
15,611
2,000
Kuna commenter mmoja hapo juu aliyejibu ( na nashawishika) kwamba huwezi kuwa na mfumo imara bila kuwa na watu imara, ila inawezekana kuwa na watu imara bila kuwa na mifumo imara. Hili si swali la kuku na yai kipi kilianza. Hili lipo wazi kabisa kwamba kiongozi imara anahitajika awepo kwanza ili kuwepo mfumo imara.
Yaani nyie Jiwe alivyokuwa anaipelekesha Nchi kama familia yake na kuifilisi kabisa ndio mnataka Strong leaders wa kariba yake?
 
Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
15,611
2,000
Nyerere alirithi nchi kutoka kwa mkoloni (mwingereza) ikiwa chini ya mifumo ya matabaka "caste" na "tribal" systems. Kulikuwepo tabaka la wazungu, wahindi na waarabu na wazawa weusi. Kazi ya kwanza ilihitaji kiongozi imara atakayevunja hayo matabaka na kuweka mfumo wake mwingine, na ndicho alichokifanya Nyerere..
Eeh embu tuambie after Jiwe era nini kitafuata,au tumsubiri tena azaliwe Jiwe mwingine mwenye roho mbaya? Mfumo imara unatakiwa uongozwe na kusimamiwa na Katiba na Sheria zenye nguvu zisizompa favor au kumuonea haya mtu yeyote yule awe Rais, Waziri,Mwanajeshi.
 
Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
15,611
2,000
Unajichanganya, huwezi kusema mfumo unawekwa na mtu kama ulivyotumia mfano wa Magufuli, mfumo imara unawekwa na sheria itakayotoa miongozo ya hao watakaokuwa wanaongoza hizo taasisi waweze kuziendesha bila kuingiliwa na yeyote wakitimiza majukumu yao, na hivyo hivyo wakiharibu washtakiwe bila kuangalia wao ni wakina nani toka chama gani...
Hao ni Mataga wanajua kila kitu ila ujinga na uzuzu wa kuamini katika Mtu ndio umewapofusha.
 
zimmerman

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
1,027
2,000
Ukitegemea busara za mtu nayo ni tatizo. Unadhani CAG Assad bila mfumo imara wa kumlinda angeweza kupona wakati wa Magufuli? Pamoja na hasira zake zote, Magufuli alisubiri mpaka mkataba ukaisha, akagoma ku-renew.

Huo ndio mfumo imara, kwamba utafanya kazi yako bila kuogopa hata kama rais hakupendi
Naona kwenye mfumo mnajikita kwenye mifumo inayolinda taasisi za chini zisiingiliwe na rais. Hamtaki kujishughulisha kwamba hizo taasisi za chini zinaweza kutumia hiyo mifumo inayowakingia kifua kufanya mambo ya ovyo kwa kisingizio cha kwamba ni wao ni mihimili inayojitegemea wasiingiliwe.

Kama mnaogopa kwamba katiba inampa rais madaraka makubwa sana na kwa udhaifu wa kibinadamu anaweza akayatumia vibaya, kwa nini msiogope pia kwamba uhuru wa mihimili mingine nao unaweza kutumika vibaya?

Kama inshu ni kuweka sheria kwamba yeyote atakayetumia vibaya ashtakiwe bila kujali yeye ni mhimili gani, swali litabaki nani atamfunga paka mwenzake kengele. Na ikumbukwe sisi raia hatujui kinachoendelea jikoni, tunalishwa tu matango pori na hayo mamihimili. CAG anapokuletea mareport kwamba shirika hili na lile limepata hasara, hatuwezi kujua uhalisia wa kile kilichoendelea nyuma ya pazia wakati akifanya hayo mahesabu.

Wape watu heshima wanayostahili, nayo ni kwamba mifumo inategemea watu.
 
zimmerman

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
1,027
2,000
Yaani nyie Jiwe alivyokuwa anaipelekesha Nchi kama familia yake na kuifilisi kabisa ndio mnataka Strong leaders wa kariba yake?
JPM hakuifilisi nchi, JPM hakuipelekesha nchi. Mnapenda kurudia rudia sana uongo na inabidi tuwajibu tu kila mara kadri mnavyourejea uongo huo.

JPM alikuwa aina ya kiongozi ambaye hakwenda ikulu kucheza na kula bata. Alienda pale kufanya kitu, kurekebisha mambo, kuvunja, kungoa na kubomoa, ili atengeneze, apande na kujenga. Katika mchakato kuna walioumia. Katika mchakato kuna mambo makubwa yalifanyika.

Mlizoea vibaya sana kuwa na rais easy-going.
 
zimmerman

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
1,027
2,000
Eeh embu tuambie after Jiwe era nini kitafuata,au tumsubiri tena azaliwe Jiwe mwingine mwenye roho mbaya? Mfumo imara unatakiwa uongozwe na kusimamiwa na Katiba na Sheria zenye nguvu zisizompa favor au kumuonea haya mtu yeyote yule awe Rais, Waziri,Mwanajeshi.
After JPM ndo hivyo taifa limepata hasara kumpoteza kiongozi wa aina yake! Mfumo gani utakupatia JPM mwingine?

"Mfumo imara unatakiwa uongozwe na kusimamiwa na Katiba na Sheria zenye nguvu zisizompa favor au kumuonea haya mtu yeyote yule awe Rais, Waziri,Mwanajeshi."

Kana kwamba hatuna Katiba na Sheria zenye nguvu tayari! We kwa akili yako unahisi hatuna Katiba yenye nguvu? Au Sheria zenye nguvu? Ulichosema na nikubaliane na wewe ni kwamba kinachotakiwa ni usimamizi wenye nguvu. Na hapo ndipo maana ya mtu kwa maana ya "viongozi bora" inapokuja.
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
11,789
2,000
Peace
hakukua na haja ya kuniita mjinga kiongozi katika familia yako lakini. Mfano wangu ni mtambuka sana kiasi kwamba hata mimi najua sijaweka nyama za kutosha ili mwelevu Kama wewe unielewe. Ila jambo la msingi ni tumepigwa sana mpaka sasa tulitakiwa kuwa donor country. Nukuu hiyo ndiyo kuchelewa kwenyewe huko.
 
PANAFRICA

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
201
250
After JPM ndo hivyo taifa limepata hasara kumpoteza kiongozi wa aina yake! Mfumo gani utakupatia JPM mwingine?

"Mfumo imara unatakiwa uongozwe na kusimamiwa na Katiba na Sheria zenye nguvu zisizompa favor au kumuonea haya mtu yeyote yule awe Rais, Waziri,Mwanajeshi."

Kana kwamba hatuna Katiba na Sheria zenye nguvu tayari! We kwa akili yako unahisi hatuna Katiba yenye nguvu? Au Sheria zenye nguvu? Ulichosema na nikubaliane na wewe ni kwamba kinachotakiwa ni usimamizi wenye nguvu. Na hapo ndipo maana ya mtu kwa maana ya "viongozi bora" inapokuja.
Taifa halijawahi na haliwezi kupata hasara kwa kumpoteza kiongozi wa aina yoyote mkuu,
no one is indispensable under the sun.(JFK)
Na ndiyo maana Mama anasema "Kazi iendelee.
 
gigabyte

JF-Expert Member
May 27, 2015
2,044
2,000
Yaani nyie mnatoa mifano mizuri kabisa inayojenga hoja ya kwamba watu bora husaidia mifumo. Sasa unapotumia mfano wa 4-4-2 kwenye mpira wote tunafahamu kwamba ili huo mfumo ufanye kazi unahitaji wachezaji bora wenye talanta zao. Makocha hao hao husajiliwa na kutimuliwa mara kwa mara maana wenye timu zao hawaamini katika mifumo wanaamini katika kocha sahihi.

Turudi kwenye mada. Usiamini sana katika sheria, amini katika watu wanaosimamia hizo sheria. Nyerere aliposema katiba imempa Rais wa Tamzania madaraka makubwa kiasi kwamba ningeyatumia kikamilifu ningekuwa dikteta. Kwa nini hakuyatumia? Kwa sababu hakuwa dikteta. Tanzania haijawahi kuwa na rais dikteta hata kama katiba inawapa madaraka makubwa kuwa dikteta. Kwa nini hawajawa madikteta? Kwa sababu kwa asili zao hawakuwa madikteta. Hata JPM anayetuhumiwa kuwa alikuwa na tendency za udikteta bado hakuwa dikteta in a real sense ya udikteta.

Kwa nini mfumo unawapa nguvu ya kuwa madikteta na hawawi? Ni kwa vile mfumo si inshu sana. Inshu ni mtu. Mtu ana uwezo wa kugeuza mfumo mzuri on paper ukawa mbaya sana, na mtu ana uwezo wa kugeuza mfumo mbaya sana on paper ukawa mzuri.
Kwani hii nchi imeshakua na marais wangapi ili utolee mfano.subiri nchi ifikishe ata maraisi 10 tuone.Instakiwa ujue hiyo katiba kama ina mapungufu yakiachwa yalivyo inaweza kuja kutumika vibaya miaka 100 ijayo.sasa wewe unaangalia hapa karibu unaacha kujua kua katiba ni andiko na muongozo unaoishi zaidi kuliko sisi binadamu.
 
gigabyte

JF-Expert Member
May 27, 2015
2,044
2,000
Mfumo imara ni kinyume cha kumtegemea mtu mmoja au kikundi cha watu kiamue kipi kifanyike wapi na lini.Maana yake ni kutengeneza sheria,kanuni na taratibu zitakazozifanya taasisi zote za serikali lazima zifanye kazi kwa uhuru na taratibu zilizopitishwa na ikiwa kinyume chake adhabu ni lazima.Na kukiwa na mifumo imara kwasababu kila mtu atawajibika ipasavyo sehemu yake ata kukiwa na ubadhirifu mahali popote ni rahisi kujulikana na hatua zikachukuliwa na vyombo stahiki,tofauti na ilivyokua uko nyuma vitu vingine vya wazi kujulikana na hatua kuchukuliwa ni hadi raisi wa nchi afanye ziara ndo akagundue uozo.Kwahiyo mifumo ikiwa imara ni kama ulivyo mwili wa binadamu,pamoja kwamba ni wako bado kuna viungo vinajiendesha vyenyewe bila wewe kuvipangia au kuamua na ikitokea vimepata itilafu lazima uvitibu ukiviacha utendaji wako utakua duni na matokeo yake unayajua.Sasa kwako wewe kipi bora kati ya kumtegemea mtu au kikundi cha watu ambao kimsingi wanaweza kubadilika au kupita kwenye hizo nafasi au kua na mifumo imara itakayomfanya yoyote atakayepata nafasi kuhudumu atahudumu sawasawa na taratibu zilizopo na hata akifa au kupita yoyote atakayekuja atapita kwenye misingi ile ile.
 
MtamaMchungu

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
6,355
2,000
Naona kwenye mfumo mnajikita kwenye mifumo inayolinda taasisi za chini zisiingiliwe na rais. Hamtaki kujishughulisha kwamba hizo taasisi za chini zinaweza kutumia hiyo mifumo inayowakingia kifua kufanya mambo ya ovyo kwa kisingizio cha kwamba ni wao ni mihimili inayojitegemea wasiingiliwe.

Kama mnaogopa kwamba katiba inampa rais madaraka makubwa sana na kwa udhaifu wa kibinadamu anaweza akayatumia vibaya, kwa nini msiogope pia kwamba uhuru wa mihimili mingine nao unaweza kutumika vibaya?

Kama inshu ni kuweka sheria kwamba yeyote atakayetumia vibaya ashtakiwe bila kujali yeye ni mhimili gani, swali litabaki nani atamfunga paka mwenzake kengele. Na ikumbukwe sisi raia hatujui kinachoendelea jikoni, tunalishwa tu matango pori na hayo mamihimili. CAG anapokuletea mareport kwamba shirika hili na lile limepata hasara, hatuwezi kujua uhalisia wa kile kilichoendelea nyuma ya pazia wakati akifanya hayo mahesabu.

Wape watu heshima wanayostahili, nayo ni kwamba mifumo inategemea watu.
Watu ni muhimu katika mfumo. Bila wao hakuna mfumo imara. Shida ni pale anapopewa mtu mmoja madaraka makubwa sana. Hata CAG office sio perfect, lakini tunaweza kuongeza uimara wake kwa mfano kutafuta kampuni ya nje nayo iwe inafanya random audits za kule alikopita CAG. Ndio mfumo wenyewe unavyojengwa, kwamba wewe kama ni mkaguzi kutoka CAG office unajua kabisa kuna mfumo wa watu kuja kujiridhisha kuhusu kazi yangu.

Ila kuwa na mtu mmoja anaamua nani achunguzwe nani aachwe sio sawa. Angalia hata hili la Mama Samia kuagiza special audit BOT, mamlaka zilikuwa wapi kuona shida? Ina maana kila siku tutahitaji rais ambaye anashida kuzunguka kila kona, no wonder hearts zao zinapata shida.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom