Naomba kupata ufafanuzi kuhusu ufundishaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalumu (VI, HI, II) pamoja na wale wa kawaida katika darasa moja

Lanlady

JF-Expert Member
Feb 27, 2019
1,421
4,729
Kumekuwepo na sera ya ufundishaji wa wanafunzi kwa kujuimuisha wenye mahitaji maalum na wale wa kawaida katika shule/ darasa moja.

Wanafunzi hawa katika baadhi ya shule wanafundishwa na walimu waliosomea ualimu wa kawaida. Tatizo linakuwa ni namna ya kuwasiliana na wanafunzi hao hasa wenye ulemavu wa kuona au kusikia.

Na kwa sasa (tofauti na hapo kabla) hata wale wenye ulemavu wa akili, nao pia huchanganywa darasa moja na wanafunzi wa kawaida.

Kwa baadhi ya shule, wanafunzi wenye ulemavu hupewa chakula bali wale wa kawaida huishia kuwatazama tu wenzao.
Inawezekana kusiwe na athari za moja kwa moja kwa sasa, lakini inaweza kuwaathiri wanafunzi kisaikolojia kwa hapo baadae.

Nadhani ni vema wanafunzi hawa wakawa na madarasa maalum pamoja na walimu maalum kama ilivyokuwa hapo kabla. Kwasababu namna ya ufundishaji na ujifunzaji wao ni tofauti na wanafunzi wa kawaida (normal learners).

Ni vema Wadau walitazame upya suala hili
 
Back
Top Bottom