DocJayGroup
JF-Expert Member
- Jan 17, 2020
- 1,654
- 3,328
Nimeona sio mbaya kuingia kwa JF kupata information zaidi sababu kuna watu wana knowledge nyingi sana na mbalimbali hapa.
Katika saiti yangu moja ya kazi, kuna nyumba za wafanyakazi. Kijana mmoja mwangalizi mkuu wa saiti hio, amekuwa akitunza hela kwenye ndoo sababu wazazi wake walipitia tatizo la Greenland bank wakapoteza hela zao zote enzi hizo. Kwa hio na yeye haamini kabisa kuweka hela banks. Sasa hivi karibuni ndio machungu yametokea na nafikiri anajuta na kutamani angeweka benki.
Katika ndoo hio ametunza akiba ya miaka mitano. Kila akipata hela amekuwa anatunza akiba laki mbili au zaidi. Kwa hio kwa hesabu za haraka haraka ni zaidi ya 10 million for 5 years. Hakugundua hadi juzi, ila wizi huo, kuna uwezekano kuwa ulitokea hata mwezi umepita sababu anaenda kwa ndoo mara moja kwa mwezi akipata mshahara kuweka akiba yake. Juzi ndio anaenda kuweka akiba anakuta ndoo hakuna. Tarehe kamili ya wizi haijulikani. Ndoo hio hata mimi niliwahi kumwona zamani sana anaifanyia welding, ila sikujua kabisa habari zake kwamba ni ya kutunzia hela. Mimi ndio mwajiri wake. Ila kuna mtu au watu itakuwa walijua sababu ilikuwa kwa room ya store ya nyumba ya huyo kijana na hawajaiba kingine zaidi ya hio ndoo tu. Ndoo ni ya chuma, mfuniko chuma, na ilikuwa imefungwa bolti kwa sakafu.
Kuna wafanyakazi wawili ndio tunawahisi, inaonekana walipanga njama sababu wamekuwa na hela sana hivi karibuni zaidi ya kawaida. Pia baada ya wote kukataa nili-arrange kwa polygraph test. Wote wakaja kasoro hao wawili waliogopa. Napenda kupata messages zao kuona kama kuna information za kupata kutoka kwa hizo text messages.
Utaratibu wa kupata messages ni upi? Kwa wasiojua, ukituma message kama simu ni ya halotel kwa mfano, halotel wanatunza messages hizo kwa computer database yao kwa muda fulani. Kwa hio hata mtu ukifuta messages kwa simu, uwezekano wa kuzipata upo. Sijui process yake na ndio naomba information. Namba za hao wawili ni halotel, na ndio nataka kuanza nao. Polisi wameshahusika, na wamewadadisi wafanyakazi wote kazini pasipo kupata jibu la maana. Kama kuna ushauri mwingine pia nisaidieni.
Tatizo hakuna ushahidi kamili na hawajakiri. Ila dalili zote zinalenga kwa hao vijana wawili. Pia walikubali kufanya adhabu ya kazi miezi miwili mizima bila malipo nilipowatishia kuwapeleka jela au else kwamba wafanye adhabu. Ila hawakukiri wakasema tu afadhali kufanya adhabu ila hawajahusika. Miezi miwili ita-recuperate 2 million only, sababu kila mmoja anapata around 500k kwa mwezi. Ila nilisema tu hivyo kuwatega, na wakakubali mtego. Naombeni ushauri zaidi. Pia naomba habari za polygraph test ya uhakika Tz. Niliyoifanya mtu huyo alitumia home-kit tu na sio high quality sana. Police depts tanzania wanafanya polygraph testing? Shida hata hio nayo haitumiki mahakamani. Ni njia tu ya ku-eliminate au ku-include suspects.