Naomba kujua kosa langu Wana jamvi

Naomba kujua kosa langu Wana jamvi

Aiseee, pole sana kijana!

Binafsi sijaona kosa lako, na umefanya vizuri tu kusema. Nadhani walioharibu huu uzi ni wachangiaji badala ya ku stick kwenye kutoa ushauri wame-base kwenye ubashiri na kufukunyua mengine.

Kwa kuongea na kusema yalio moyoni mwako umejipa uhuru wa akili na kuondoa hasira zako kifuani, ushayatoa ya moyoni relax endelea na maisha yako tu. Usiangalie ulipotoaka, angalia unapo elekea ndio iko na umuhimu kwa sasa.

Insinuation na speculation zetu sisi wachangiaji tuziache. Sidhani kama kuna faida sana kumjua mhusika wa pili. Japo najua alipo sasa atakuwa kajawa na hasira manake kwa mleta mada kusema ya moyoni kajiondolea tatizo, sasa huyo binti atakuwa na hasira za kuletwa hapa nae atafute pa kusemea ya moyoni awe huru kiakili na kuondoa hizi stress.

Kucheza na hisia ni mbaya sana, seriously na hivi inakuwaje kutongozana mitandaoni? Mbona social na public centre ziko mob tu mnafanya meeting na ku-date! Hizi cheap relationship za mitandaoni ndio cost yake hii.

Ma phyico na serial killer wanatengenezwa hivi hivi kwa visa vya ki.pu.mbavu kuumizana kwenye mapenzi bila sababu za msingi. Hata kama mtu haja meet yo standard au hajafikia criteria zako kuna better way ya kum-push back!

Poleni sana...wote msichana na mvulana. Wote mko kwenye majanga ya kimapenzi. Tafuteni pa kusemea muondoe hasira na muwe na akili huru za kuweza kupenda na kuamini kwenye mapenzi ya kweli.

Sent from my WhiteBerry using JamiiForums

Safi sana kwa mchango wako
 
:becky::becky::becky::becky:

Ivi hii becky becky becky ni kitu gani?naomba nijue ina maana gani.nliipotezea mwanzoni ila bado naziona tuu.becky::becky::becky:: 😂 lol
 
........hii inaweza kuwa kweli, mdada kaona gari mkweche akaamua kutoka ndukii!! Betri ya gari ni laki 2 tu......akaona hapa wallet hoi.

Ila nafuu mdada kauchuna kujitokeza hapa, kafanya la maana sana.

kwani alikuwa anaenda kuwa kwenye mahusiano na gari?
 
Paka shume tu huyo...na hakua na nia na hiyo siku alikua analiwa..
 
........hii inaweza kuwa kweli, mdada kaona gari mkweche akaamua kutoka ndukii!! Betri ya gari ni laki 2 tu......akaona hapa wallet hoi.

Ila nafuu mdada kauchuna kujitokeza hapa, kafanya la maana sana.

Ndiyo maana vijana wangu wa leo hwapendi shida, wakidate mdada aidha waazime gari au wakodishe kwa siku ili mradi papuchi iliwe tu. Ikishaliwa demu akiulizia gari ataambiwa lipo service. Hahahaaaaaaaa...
Baadaye warembo mnarudi humuhumu mkilia mmetendwa, wakati mwanaume sahihi alikuja lakini kwa kuwa hakuwa na gari au gari lake kimeo ukamtema.
 
Mkuu pole sana bana ndo changamoto za maisha ya mausiano.
Habari wana jamvi

Naomba ushauri wa kutambua Kosa langu katika hili labda naweza jifunza na kuomba msamaha

Nilipendezewa kiukweli sana na binti mmoja mwana jamvi humu nikaanza kumtokea lakini alinieleza kuwa ana yupo likizo ktk mahusiano ya kimapenzi kwa sasa.

Niliendelea kumshawishi ili aweze kumaliza hiyo likizo na kumuahidi sita mpa majonzi ya kumfanya achukue likizo tena.

Hakukubali direct ila tuliendelea kuchati kwa muda mrefu tu na tulikuwa tukiwasiliana hadi muda wa kulala tunaagana ndo kila mtu ana lala,nilipenda kumuandikia sms nikiishia na neno Mpz lakini alisema mimi sio mpz wako bado.Mimi nilimwambia sawa japo halidhuru chochote basi nitakuwa nikiandika sms siliandiki na badala yake nikifika sehemu ya kuandika nitaja kimoyoni tu halafu naendelea.

Tuliwasiliana kwa muda lakini hakuwa Daresalaam alikuwa ameenda Mkoani bt siku moja alianza kucharuka na kusema mbona siku hizi nimebadilika na simuiti mpz tena hata simu sipigi.

Nilijitetea kuwa nilikupigia mbona Mara moja akasema mwanzo ulikuwa unapiga Mara tatu sasa umepunguza Mimi nikaona isiwe mada nikaomba radhi akakubali tukaendelea na mawasiliano.

Siku moja aliniambia ujue Mimi nina mtoto nikamuuliza baba yake yupo wapi akasema amenitelekeza nikamwambia pole but maisha yanawezekana pia bila huyo baba yake.akasema ni kweli hadi sasa mtoto ana miaka 3 ana mlea mwenyewe nikasema hongera kwa uvumilivu na kuamua.

Tuliendelea na mazungumzo ila siku moja tarehe kama 30/12/2014 tukiwa tunachati ghafla niliona kaniblock watsapp nikamwandikia sms kawaida nikamuuliza kulikoni hakujibu!!nilikuja kumpigia saa tano usiku akawa ana kata na baadae alituma sms na kusema hawezi pokea Simu amelala na mtoto ataamka nikakubali na kesho yake akaendelea kuwa kimya.

Aliniambia ana taraji kurudi tarehe 1/1/2015 kwa kuwa ni mwalimu wa shule moja hivi lakini kwa kuwa hakuwa anawasiliana nami tena niliamua kupotezea tu,Leo majira ya saa nne asb nikaona sms yake on my way!!nikamwambia umeanza safari ya kuja akasema ndio basi nikamwambia karibu sikutaka kukumbusha yale .


Tuliendelea kuwasiliana hadi alipofika nikaenda kumpokea baadae nilimuambia vipi ulisema unakuja na mwanao mbona hujaja nae akasema hana dada wa kazi ameamua kumuacha na mama yake baadae aliniuliza una mtoto nikamwambia ndio akasema hawezi olewa na mwanaume mwenye mtoto nilimuambia kwa nini aksema huwa mna kumbushia nikasema Jf Leo kulikuwa na Uzi wa hii mada na ulikuwa unachangia kuonesha inawezekana Leo vipi akasema hayo ni mamabo ya mtandaoni siwezi kuzungumzia

Tukaendelea na safari nikawa nimepigiwa Simu na dada yangu mmoja nikaongea nae na baadae niliongea na Mama wa mwanangu ambaye alinipigia Simu akaanza kuniuliza mwanao ana itwa nani? Nikamwambia akasema na huyo mama yake nikasema ndio akasema mbona mna active communication nikamwambia ni active communication na sio active mapenzi.

Akaanza kuwa mkali na kusema nimshushe njiani kwani hapendi kudanganywa nikamwambia hapo uongo upo wapi?akasema unawezaje kuwa na mpz na ukaongea na ex Wako nikamwambia inawezekana akasema Mimi nilikudanga sina mtoto nilitaka kukupima!!!!???

Najiuliza

1. lengo la kusema ana mtoto ndo kumpima mwanaume?
2. Mbona aliniomba nimtafutie dada wa kazi kwa ajili ya mwanae au alikuwa ana nipima back
3.Mbona nilipopiga simu usiku alisema amelala na mtoto au ndo alikuwa ana nipima?

Najiuliza maswali mengi zaidi ya hayo ?na baadae aliomba nimushushe njiani ila nilimtoa ubungo hadi Mbagala maji matitu kwa umbali huo na alikuwa naelekea chamazi akadai ana boreka na uongo wangu na pretending na ndo maana hawapendi wanaume akaomba kushuka na ikabidi nimshushe japo nilimwambia Leo Luna panya road umewaona nakuonea huruma just nikufikishe karibu na kwako alikataa na nikabidi nishushe na sijui amefika au LA


Nawasilisha naweza mtaja akiridhia na sheria za Jf kama zina ruhusu kwani nimeumia na kuwaza sana which kind of woman is this

Naomba radhi kwa kuwachosha japo lengo langu muelewe kwa kiasi pa kuanzia kunishauri


Regards,
Superbrand
 
Back
Top Bottom