ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,279
- 7,681
Kuna swala la kuupenda muziki, halafu kuna swala la umaarufu. Hivi ni vitu viwili tofauti. Zamani kulikuwa na rekodi ya mizoki gani inauzwa zaidi na inakaa kwenye chat. Joseph Kabasele amekuwa kwenye chat kwa miaka mingi na nyimbo nyingi ukimfananisha na Pepe Kalle. Pia Pepe Kalle ni generation tofauti na kina Franco, kwahiyo nyimbo zake pia ni tofauti.Muziki kila mtu anaupokea kwa ladha yake , mimi binafsi nasikiliza nyimbo za Pepe kalle mpaka leo.
Tukumbuke kuwa huku East Africa nyimbo za Congo zilianza kupata umaarufu miaka ya 70 baada ya serikali ya Mobutu kuyumbisha uchumi. Kwahiyo wanamuziki waliokuwa maarufu kabla ya miaka ya 70 hawana umaarufu sana East Africa.