Nani ndo GOAT wa rhumba?

Nani ndo GOAT wa rhumba?

Samahani; hiyo post uliyokwoti niliiandika kwenye iphone, na hao jamaa wa iphone huwa wana tabia ya kubadilisha maneno ninayoandika kwa kiswahili. Nimeshairekebisha.

Tukirudi kwenye mada, ukweli ni kuwa hakuna mtu anayejidai kuwa ni mwazilishi wa Mziki wa Rhumba huko Congo kwa sababu kadhaa, Muziki wa rhumba uliletwa eneo letu hili na Salim Abdallah Yazidu aliyekuwa na Bendi ya Morogoro Jazz baadaye akaanzisha ya kwake iliyoitwa Cuban Marimba. Hapo alivuta muziki wa Cuba na kuuweka katika marimba za kiafrika, na hiyo ilikuwa ni mwaka 1948. Muziki wa rhumba ya Salimu Abdallah ulimvutia sana Kabasele naye akaanzisha bendi yake ya African Jazz mwaka 1953, yaani miaka mitano baada ya Salim Abdallah kutangulia. Franco alianza muziki kama muajiliwa wa bendi ndogo ilyokuwa ikishandana na ile ya Kabasele; bendi hiyo ilikuwa inajulikana kama Bandidu. Mwaka 1956 ndipo alipoanzisha bendi iliyokuja kujulikana ka TP OK Jazz. Huyu Kabasele nadhani ndiye babawa Pepe Kalle, ila baadaye walishirikiana na Francko kwenye Muziki wao.

Kwa mtililiko huo, utagundua kuwa Franco alikuwa ni late comer sana kwenye muziki wa Rhumba. Isingekuwa kifo kumchukua Salimu Abdallah, labda Franco asingekuwa jina kubwa sana kama lilivyo leo.

View: https://www.youtube.com/watch?v=xAEDihQDV-I&list=RDxAEDihQDV-I&start_radio=1

some usefull info, naomba source ya hii taarifa
 
some usefull info, naomba source ya hii taarifa
Source ni mimi mwenyewe; hujui kuwa mimi ni kichuguu? Hayo yanataokea mimi nilikuwa toddler tukifundishwa AEIOU kwenye mwembe. Ndiyo maana nilichukizwa na lugha yako kuse,ma kuwa mimi ni mwongo. Ni afadhali kusema kuwa hii siyo kweli kulikuo kusema kuwa huo ni uwongo. Najua vijana wengi wa siku hizi hawana skills za mawasiliano lakini kuna haja ya kuwa kuwa msikivu wakati unawasliana na watu wengine.
 
samahani kwa hili, nimechunguza online apa however naona anapewa credit mtu anaitwa Antoine “Papa Wendo” Kolosoy
 
Sikiliza: Rhumba unalolijua wewe leo hii lililetwa kwetu Afrika na Salim Abdallah; mengine yote ni hadithi tu. In fact Salimu alikwenda Cuba kujifunza muziki huo na kuuleta kwetu. Unaweza kufikiria miaka hiypo ya 1945 mtu kutoka Tanganyika hadi kufika Cuba na kurudi.
 
Back
Top Bottom