Wadau,
Kwanza nianze kusema kuwa LOKETO haikuwa BENDI gorup.
Hawa jamaa walikuwa na bendi zao za kila siku na time to time wanaamua kukutana na kula good time pamoja. Ndiyo maana safu zao siku zote zilikuwa zinabadilika ingawa kuna jamaa siku zote walikuwa hapo.
Loketo ama KIUNO walipata sifa kubwa sana kwa muda mfupi kwani walikuwa ni watu wanafahamu nini wanataka na kukifanya kwa umahiri mkubwa na hamna eti MTU WA KUJAZIA. Mwanzo walianza na Diblo Dibala aliyetoka kwa Kanda Bongo Man na kuanzisha kundi lake mwenyewe baadaye. Baadaye wakawa na Dally Kimoko. Moja ya watu mashuhuri aliyekuwa kwenye kundi hili ila siku hizo hafahamiki ni Awilo Longomba.
http://www.youtube.com/watch?v=QBCCcH-QJWY
(Ukianzia 4:00 utamsikia Awilo akiimba/Rap na mbele kidogo mama anasema Dally Kimoko).
http://www.youtube.com/watch?v=UNXVIXcpbUo
(Ukianzia 3:15 utasikia wakitaja jina la
Awilo Longomba ambaye siku hizo ni Mpiga drums unazosikia kwenye wimbo hapo juu).
Ki ufundi, Diblo Dibala alikuwa akipiga gitaa ki-Afrika zaidi yaani nyuzi moja moja. Dally Kimoko alianza kuweka zile sauti za gitaa kama za Rock Musics yaani ufundi wa akina Slash wa Gun N' Roses au Mzee Jimmy Hendrix. Ila wengine pia walianza baadaye kuiga kama akina Zaiko langa langa na Waafrika tuliipenda maana walikuwa wakiweka sauti tu ila upigaji unabaki ule ule.