Umemuacha SHESHE KALONDA msikilie kwenye ile ABISINA YA PEPE KALE
Kakuruvi,
Ni extra Ball(sio Boy)..lol... ngoja niilete hapa...
http://www.youtube.com/watch?v=y7hkcm7sV9Y
Kakuruvi,
Line up hapa(toka kushoto) Djo Mpoyi,Pape Ndombe Opetum,Madilu(kalikuwa katooto,just joined) na mtu wangu 'Josky' Kiambukuta Londa
http://www.youtube.com/watch?v=OAQuXaO7nCw&feature=related
Hapana...just happened to like music na historia yake pia....lakini nyaisanga ni mmoja wa resource people wangu...sadly hayupoten R1 maana ijumaa nilikuwa sikosi HIZI NAZO a program from 9 to midday...hawa alowaachia wanavurunda tu...
Nawasalimu Great Thinkers,
Kama kuna watu waliojaliwa vipaji na wamevitumia ni hawa jamaa wawili Diblo Dibala na Dally Kimoko, hawana utani wanapokamata mpini, mfano Diblo Dibala (Extra Boy), Dally Kimoko (Liza), si mchezo achilia mbali bendi zao za kazi ila wamekuwa wakitumiwa na bendi nyingine kurecord, kama kuna mwenye nyimbo walizopiga mpini leteni humu tusikie mambo, nani zaidi kati ya hawa magwiji wa mpini?
Nawasalimu Great Thinkers,
Kama kuna watu waliojaliwa vipaji na wamevitumia ni hawa jamaa wawili Diblo Dibala na Dally Kimoko, hawana utani wanapokamata mpini, mfano Diblo Dibala (Extra Boy), Dally Kimoko (Liza), si mchezo achilia mbali bendi zao za kazi ila wamekuwa wakitumiwa na bendi nyingine kurecord, kama kuna mwenye nyimbo walizopiga mpini leteni humu tusikie mambo, nani zaidi kati ya hawa magwiji wa mpini?
Tuko pamoja mkuu wangu hawa jamaa walikuwa wanatupa vitu adimu sana lakini hata hapa nyumba kulikuwa na wakali wa mpini wa mpini wa solo enzi hizo ambao kwa uchache naomba niwataje. Mose sengo Fan Fan,Nguza Viking [Babu seya],Supreme Ndala Kasheba na gita lake la nyuzi kumi na mbili,Kawale Motimwana na Mbaraka Mwinshee Mwaruka.
muziki wa kizazi kipya hauna fursa za kuwa na wakali wa ala mbali mbali za muziki kazi zote zinafanywa na computer badala ya utundu wa wasanii.Hali ikiachwa iendelee kwa muda mrefu uenda tutakuja kuwa na kizazi cha wanamuziki wasiojua kutumia ala za muziki.
Wadau,
Kwanza nianze kusema kuwa LOKETO haikuwa BENDI gorup.
Hawa jamaa walikuwa na bendi zao za kila siku na time to time wanaamua kukutana na kula good time pamoja. Ndiyo maana safu zao siku zote zilikuwa zinabadilika ingawa kuna jamaa siku zote walikuwa hapo.
Loketo ama KIUNO walipata sifa kubwa sana kwa muda mfupi kwani walikuwa ni watu wanafahamu nini wanataka na kukifanya kwa umahiri mkubwa na hamna eti MTU WA KUJAZIA. Mwanzo walianza na Diblo Dibala aliyetoka kwa Kanda Bongo Man na kuanzisha kundi lake mwenyewe baadaye. Baadaye wakawa na Dally Kimoko. Moja ya watu mashuhuri aliyekuwa kwenye kundi hili ila siku hizo hafahamiki ni Awilo Longomba.
http://www.youtube.com/watch?v=QBCCcH-QJWY
(Ukianzia 4:00 utamsikia Awilo akiimba/Rap na mbele kidogo mama anasema Dally Kimoko).
http://www.youtube.com/watch?v=UNXVIXcpbUo
(Ukianzia 3:15 utasikia wakitaja jina la Awilo Longomba ambaye siku hizo ni Mpiga drums unazosikia kwenye wimbo hapo juu).
Ki ufundi, Diblo Dibala alikuwa akipiga gitaa ki-Afrika zaidi yaani nyuzi moja moja. Dally Kimoko alianza kweka zile sauti za gitaa kama za Rock Musics yaani ufundi wa akina Slash wa Gun N' Roses au Mzee Jimmy Hendrix. Ila wengine pia walianza baadaye kuiga kama akina Zaiko langa langa na Waafrika tuliipenda maana walikuwa wakiweka sauti tu ila upigani unabaki ule ule.