Nani kama Mama Vs Nani kama Baba

Nani kama Mama Vs Nani kama Baba

Mpaka sasa hakuna aliyeweza kutetea hii hoja ya Hakuna kama mama, maana wote waliochangia wamishia kusema tu bila kutolea maelezo. Babu wameshindwa kujenga hoja pale ishu ya kutupa watoto na kuwatesa kwa hiyo babu upo sahihi kabisa kama hakuna kama baba pia
 
Unajua nini kamanda? Hii nyuzi yako imenigusa sana. Kuna baba wengi sana ambao hawatendewi haki yao. Wababa tunajipinda na wakati mwingine kujinyima ili tuweze kuwapa wanetu misingi bora ya maisha lakini bado tu hatuthaminiwi kama inavyostahili.

Wengine tunafanya mengi kuliko hata hao mama zao waliowazaa lakini wapi. Hatupewi haki yetu. Inasikitisha sana mkuu. Laiti watu wangejua jinsi wengine tunavyowahangaikia wanetu labda wangeweza kututhamini.

Nakusomasana kamanda....hawa kina mama wanakwepa kuwasemea kina mama wanaotupa vichanga, wanaotelekeza watoto wao (akiwemo binti mmoja niliyezaa naye..........huyu sijui ukimwambia nani kama mama atakuelewaje), kuna wanaowatesa watoto wao kama wanyama..............hayo yote hawayasemi.

Kina baba hata tujipinde vipi, bado tunaonekana kama samadi tu.
 
Kuzaa sio kazi kazi ni kulea. Na ujue kulea sio kulipa school fees.

Baba yangu alifanya na bado anafanya mengi ambayo hayapimiki. Kwangu HAKUNA KAMA BABA! Na kwa mwanangu navyo vivyo hivyo. Kwake hakuna kama mimi. Nimefanya yote na naendelea kufanya mengi na nitaendelea kufanya mengi zaidi hadi nitakapovuta pumzi yangu ya mwisho hapa duniani.
 
Hao sio kina mama sababu hawajui wala hawako tayari kuwa mama,hapa anatazamwa mama aliye mama na amabaye amevaa uhusika wa kimama.
TUSICHANGANYE MADESA SASA HATA TUNAPOSEMA HAKUNA KAMA BABA SIO WOTE NI KINA BABA WENGINE NI WAMWAGA MBEGU TU.

Kwahiyo ishu hapa ni kutojenerolaiz siyo?

Kwama si kina mama wote wana sifa ya NANI KAMA MAMA
Na siyo wanaume wote hawana sifa NANI KAMA BABA.

Sawa si sawa?
 
nina wasi wasi na wewe !!! nini maana ya kulea? kulea siyo kubeba mtoto mgongoni!!!!

Comeback yao mara huwa kulea sio kutoa ada za shule. Wanasahau kuwa kina baba nao hufanya kila kitu. Mimi hakuna ambacho sijakifanya kwa mwanangu katika malezi yake. You name it, I have done it.
 
Mkeo hafanyi unayofanya kwa bintiyo?? Usizungumzie majukumu ya baba, majukumu ni lazima, hayakufanyi uwe zaidi ya mama. Hapa tunazungumzia mioyo ya wamama, hawalipi school fees, lakin wana UPENDO wa kipekee kwenye familia zao. Hongera kwa kuwa baba bora, sio wote wako kama wewe.
Baba yangu alifanya na anafanya mengi ambayo hayapimiki. Kwangu HAKUNA KAMA BABA! Na kwa mwanangu navyo vivyo hivyo. Kwake hakuna kama mimi. Nimefanya yote na naendelea kufanya mengi na nitaendelea kufanya hadi nitakapovuta pumzi yangu ya mwisho hapa duniani.
 
Kwahiyo ishu hapa ni kutojenerolaiz siyo?

Kwama si kina mama wote wana sifa ya NANI KAMA MAMA
Na siyo wanaume wote hawana sifa NANI KAMA BABA.

Sawa si sawa?
Hili ndo hitimisho Babu watake wasitake. Huwezi kutupa mtoto then ukastahili hi heshima
 
Hapa tunaanza kwenda sawa sawa.
Kwahiyo ishu hapa ni kutojenerolaiz siyo?

Kwama si kina mama wote wana sifa ya NANI KAMA MAMA
Na siyo wanaume wote hawana sifa NANI KAMA BABA.

Sawa si sawa?
 
Mkeo hafanyi unayofanya kwa bintiyo?? Usizungumzie majukumu ya baba, majukumu ni lazima, hayakufanyi uwe zaidi ya mama. Hapa tunazungumzia mioyo ya wamama, hawalipi school fees, lakin wana UPENDO wa kipekee kwenye familia zao. Hongera kwa kuwa baba bora, sio wote wako kama wewe.

Kwani sisi (mimi) hatuna upendo wa kipekee kwa wanetu? Acha hizo bana. Acha kabisa. Nampenda sana mwanangu. Nikipigiwa tu simu sasa hivi nikaambiwa anaumwa mafua naacha kazi narudi nyumbani kumuuguza. Hakuna mwingine anayeweza kunifanya niache shughuli zangu zaidi yake yeye. Upendo wangu kwake haufananishwi wala kulinganishwa. Ni wa kipekee.
 
Hili ndo hitimisho Babu watake wasitake. Huwezi kutupa mtoto then ukastahili hi heshima
Sisi hatujatupwa na ndiyo mana tuko hapa kuwasemea mama zetu. Ukitupa mtoto huna maana.
 
Hongera kwa mara nyingine tena! Mkeo je hana hayo mapenzi uliyo nayo wewe kwa huyo mtoto wenu?
Kwani sisi (mimi) hatuna upendo wa kipekee kwa wanetu? Acha hizo bana. Acha kabisa. Nampenda sana mwanangu. Nikipigiwa tu simu sasa hivi nikaambiwa anaumwa mafua naacha kazi narudi nyumbani kumuuguza. Hakuna mwingine anayeweza kunifanya niache shughuli zangu zaidi yake yeye. Upendo wangu kwake haufananishwi wala kulinganishwa. Ni wa kipekee.
 
Tuko pamoja na hilo ndo jibu.

Kwahiyo ishu hapa ni kutojenerolaiz siyo?

Kwama si kina mama wote wana sifa ya NANI KAMA MAMA
Na siyo wanaume wote hawana sifa NANI KAMA BABA.

Sawa si sawa?
 
Back
Top Bottom