Nani kama Mama Vs Nani kama Baba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani kama Mama Vs Nani kama Baba

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Asprin, May 6, 2011.

 1. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,062
  Likes Received: 24,061
  Trophy Points: 280
  Waungwana salamu,

  Kuna thread moja huko kuna mjadala umezuka na ndani ya thread yenye topic tofauti kabisa. Nimeona niuweke hapa mjadala ili ujadiliwe kwa kina kama itaonekana inafaa.

  Kuna huu msemo: Nani Kama mama? Au hakuna kama mama........Hakuna anayebishana na msemo huu. Mama acheni aendelee kuitwa mama. Anastahili. Ni msemo unaompa heshima mama.

  Shida imetokea pale babu nilipohoji: Hivi kuna aliye kama baba? Wajukuu zangu wamenishambulia na hoja yao ya msingi ni kuwa majukumu ya baba anaweza akapewa mtu yoyote yule na akayamudu. Hastahili kupewa heshima ya "NANI KAMA BABA" Sijajua ni majukumu gani wanayoyashikilia ambayo hata baba asipokuwepo haijalishi.....kulea? kujali? kusomesha? ku nini sasa?

  Eti ni kweli baba hana umuhimu huo na wala hastahili kupewa heshima ya "Nani kama baba"?

  Babu leo siendi ofu topic kabisa, niko kimaadili.....Kama Matesha wangu haoni sababu ya kunipa heshima ya "Nani kama ODM Asprin".......Mi ntakuwa simwelewi kwakuwa kwangu Mimi Hakuna kama baba yangu mmzee Ng'maryo.

  ODM anaomba msaada waungwana

  Babu anarudi kitandani.
   
 2. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Wapo kama baba ila hakuna kama mama.
   
 3. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  'Nani kama mama?' hili neno lina maana kubwa sana. Ngoja nijipange kisawa sawa nije nikujib kwa ufasaha mpaka uamini kuwa hakuna kama mama!Nafanya maombi kwanza.
   
 4. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,062
  Likes Received: 24,061
  Trophy Points: 280
  Kina nani hao ambao wako kama baba? Wajomba? Mababu? Mashemeji? Kina nani hasa?
   
 5. One and Only

  One and Only Senior Member

  #5
  May 6, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mama anaanzia kulea tumboni mpaka baada ya kuzaliwa, wapo kama baba ila hakuna kama mama
   
 6. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #6
  May 6, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,062
  Likes Received: 24,061
  Trophy Points: 280
  Hili la Nani kama baba halina maana kubwa?

  Kina baba tumewakosea nini mpaka hamtaki kutupa heshima hii?
   
 7. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #7
  May 6, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,062
  Likes Received: 24,061
  Trophy Points: 280
  Na huko tumboni ni nani aliyekuweka humo?
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  May 6, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,417
  Trophy Points: 280
  Hakuna aliyepo kama baba yangu. Baba yangu ndo shujaa wangu. Ingawa nampenda mama yangu lakini mapenzi yangu kwa baba yanayazidi yale ya mama. Msiniulize kwa nini. Ni jambo zito sana.

  Kwa hiyo hapo utaona kuwa inategemea na uhusiano mtu alionao na mzazi/ wazazi wake. Mimi binti yangu ananipenda kuliko maelezo. Ukimwuliza 'who is your hero?'.....anakujibu bila kusita 'my daddy is my hero'. Kwake ni 'nani kama baba'. Humwambii na humwelezi kitu kuhusu baba yake. She's a daddy's a girl and I savor every bit of it.
   
 9. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #9
  May 6, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,089
  Likes Received: 885
  Trophy Points: 280
  nani kama mama.........
   
 10. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #10
  May 6, 2011
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  kama wewe...hakuna kama mama.
   
 11. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #11
  May 6, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,062
  Likes Received: 24,061
  Trophy Points: 280
  Thats my boy!

  You can say that again and again and again!!
   
 12. One and Only

  One and Only Senior Member

  #12
  May 6, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Sperm peke yake ingekuwa inatunga mtoto basi akina baba wangekuwa wanazaa peke yao, huko tumboni ni mchango wa mbegu ya kiume na yai la mama na bado mama ndio amebeba kiumbe kwa miezi 9 tukiacha shida zingine wa mama wajawazito wanazopata na bado anakuja kunyonyesha, hakuna anaeweza kupinga umuhimu wa maziwa ya mama kwenye growth ya mtoto, hakuna kama mama
   
 13. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #13
  May 6, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,062
  Likes Received: 24,061
  Trophy Points: 280
  Yaani mimi kwa wanao naweza kuwa kama baba watoto wako?....You cant be serious!
   
 14. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #14
  May 6, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Wababa na Waheshimiwe sana tu. Kusema hakuna kama mama haimaanishi tumewadharau wababa! No. Kuna mambo kwenye hii dunia wamama wanayapitia, wanayavumilia, n.k wababa hawawezi kufanya hivyo. Jarb kuangalia kwnye familia mama akikosekana nini kinatokea, na hapo baba yupo. Wamama ni zaidi ya marafiki kwa watoto wao. Naishiwa na cha kusema ila kweli hakuna kama mama.
   
 15. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #15
  May 6, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Mama KWANZA halafu ndio Baba. Hata vitabu vya dini vimesema hivyo.
   
 16. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #16
  May 6, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Ukichukulia huo msemo literary kua hakuna kama mama na hivyo baba ana umuhimu utakua unakosea njia... Ni kwanini inasemekana hakuna kama mama?

  Mama ni kiumbe ambae katika viumbe woote tunamchukulia sana for granted. Huyu mama ndo kakubeba wewe tumboni kwako (hebu naomba u pause kidogo na tafakari hili suala - kua the whole of you, mwili wako huo wote ulitoka ndani ya tumbo lake). Mama ni Mwalimu, rafiki, dakitari, mtabiri, mpenzi wa kweli, dereva na vitu vingine viingi ambavyo naamini hata wewe pia unaelewa. Asprin niseme nini hapa... Nani kama mama ??? Mama anaamini wewe ndo wewe no matter your weakness (sometimes anapalilia hata hizo weakness), Mama anakuambia mwanangu Aprin mimi nakupenda na as long as am still there you will always be safe, sitakubali dunia ikusumbue... Niambie mwanangu; unasema unahitaji niwaongeze wewe na mkeo mtaji - usijali nitaongea na baba....

  Baba on the other hand ni nguza yako ya kuegemea, ni jeshi lako la kukimbilia iwapo kuna wasi wasi wowote wa mashambulizi, ni mtu akuoneshae kua hii dunia you can overcome anything ukitumia nguvu, determination, focus na akili. Ni mtu ambae anakusimamie but ikifika wakati wa wewe kusimama anakujulisha kua nawe sasa ni ngazi, anakwambia kabisa kama wewe huna hivi huna nafasi katika hii dunia hivyo jiandae kua defeated - na anakujulisha kua kama utashindwa kua mwanajeshi katika mambo yote yakuzungukayo na kukusumbua basi mi sio commander wako...

  Ni wachache saana wamepata bahati ya kupata committed Fathers hata kama wamelelewa nao, but kwa wale woote walojaliwa kulelewa na mama zao ilikua ni rahisi kupata a committed mom though ndio kuna exceptions..
   
 17. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #17
  May 6, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,062
  Likes Received: 24,061
  Trophy Points: 280
  Kwahiyo huu ujiko wa "Nani kama mama" ni kwa kuwa tu kabeba mimba kwa miezi tisa? Ni hicho tu? Mbona kuna wanaojifungua na kuua watoto wao? Mbona kuna wanaotesa watoto wao?....Hawa wanaowatesa watoto wao kama wanyama nao wanastahili kupata hii heshima ya "nani kama mama" kwakuwa walibeba mimba kwa miezi tisa?
   
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  May 6, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,417
  Trophy Points: 280
  Kwangu mama alikosekana na mambo hayakwenda mrama. Hakuna aliyepo kama baba yangu.
   
 19. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #19
  May 6, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hahahaha....babu naona hii kitu imekugusa sana!!
  Hamna kama mama ila wapo kama baba....ndio maana mzee yeyote anaweza kua baba yako ila sio mwanamke yeyote anaeweza kua mama yako.

  Kama unavyosemaga mwenyewe USIPINGANE NA NATURE!!!
   
 20. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #20
  May 6, 2011
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  Hivi hommie.....apa ulikuwa unamaanisha mama au baba?
   
Loading...