Nani kama Mama Vs Nani kama Baba

Ana umri gani huyo binti yako? Manake kuna umri mtoto hajaweza kuwa na akili vzr, ukmwulza baba na mama unampenda nani? Atakujb baba! U know why? Zawadi na outings zinamzuzua, akikua akaujua ulimwengu vizuri atabadili maneno yake. Atagundua mama ni muhimu kwake kuliko mtu yeyote huku duniani.
Hakuna aliyepo kama baba yangu. Baba yangu ndo shujaa wangu. Ingawa nampenda mama yangu lakini mapenzi yangu kwa baba yanayazidi yale ya mama. Msiniulize kwa nini. Ni jambo zito sana.

Kwa hiyo hapo utaona kuwa inategemea na uhusiano mtu alionao na mzazi/ wazazi wake. Mimi binti yangu ananipenda kuliko maelezo. Ukimwuliza 'who is your hero?'.....anakujibu bila kusita 'my daddy is my hero'. Kwake ni 'nani kama baba'. Humwambii na humwelezi kitu kuhusu baba yake. She's a daddy's a girl and I savor every bit of it.
 
am happy because i will be ranked higher than my boy by mtoto wetu.

Hamna kama mama.
 
Ukichukulia huo msemo literary kua hakuna kama mama na hivyo baba ana umuhimu utakua unakosea njia... Ni kwanini inasemekana hakuna kama mama?

Mama ni kiumbe ambae katika viumbe woote tunamchukulia sana for granted. Huyu mama ndo kakubeba wewe tumboni kwako (hebu naomba u pause kidogo na tafakari hili suala - kua the whole of you, mwili wako huo wote ulitoka ndani ya tumbo lake). Mama ni Mwalimu, rafiki, dakitari, mtabiri, mpenzi wa kweli, dereva na vitu vingine viingi ambavyo naamini hata wewe pia unaelewa. Asprin niseme nini hapa... Nani kama mama ??? Mama anaamini wewe ndo wewe no matter your weakness (sometimes anapalilia hata hizo weakness), Mama anakuambia mwanangu Aprin mimi nakupenda na as long as am still there you will always be safe, sitakubali dunia ikusumbue... Niambie mwanangu; unasema unahitaji niwaongeze wewe na mkeo mtaji - usijali nitaongea na baba....

Baba on the other hand ni nguza yako ya kuegemea, ni jeshi lako la kukimbilia iwapo kuna wasi wasi wowote wa mashambulizi, ni mtu akuoneshae kua hii dunia you can overcome anything ukitumia nguvu, determination, focus na akili. Ni mtu ambae anakusimamie but ikifika wakati wa wewe kusimama anakujulisha kua nawe sasa ni ngazi, anakwambia kabisa kama wewe huna hivi huna nafasi katika hii dunia hivyo jiandae kua defeated - na anakujulisha kua kama utashindwa kua mwanajeshi katika mambo yote yakuzungukayo na kukusumbua basi mi sio commander wako...

Ni wachache saana wamepata bahati ya kupata committed Fathers hata kama wamelelewa nao, but kwa wale woote walojaliwa kulelewa na mama zao ilikua ni rahisi kupata a committed mom though ndio kuna exceptions..
Thanks Asha kwenye hii useful post.
Hapo kwenye red.........Haimpasi baba kupewa heshima hiyo ya NANI KAMA BABA?
 
Muda si mrefu ulopita pale Mwananyamala kama sikosei miili ya maiti za vichanga ilikutwa imetupwa. Nani kama mama?
 
Hahahaha....babu naona hii kitu imekugusa sana!!
Hamna kama mama ila wapo kama baba....ndio maana mzee yeyote anaweza kua baba yako ila sio mwanamke yeyote anaeweza kua mama yako.

Kama unavyosemaga mwenyewe USIPINGANE NA NATURE!!!

Mnatunyanyapaa sana bana.

Kama nlivyokwambia, wakati wa ujana wangu nilifanikiwa kumkabidhi binti mmoja mimba ya kujitolea. Mtoto aliyezaliwa, niko naye hapa home akilelewa na mai waifu wangu. Mtoto wala hajui kama huyu si mama yake....Je mai waifu wangu hajawa kama mama wa huyu binti?....
 
Muda si mrefu ulopita pale Mwananyamala kama sikosei miili ya maiti za vichanga ilikutwa imetupwa. Nani kama mama?

Kubeba mimba hakumfanyi mtu mama...kua na hisia na kichanga alichobeba ndo kunamfanya mtu mama!!
Ndo maana hao watupa vichanga hawaitwi wala hawajiiti mama....
 
Ana umri gani huyo binti yako? Manake kuna umri mtoto hajaweza kuwa na akili vzr, ukmwulza baba na mama unampenda nani? Atakujb baba! U know why? Zawadi na outings zinamzuzua, akikua akaujua ulimwengu vizuri atabadili maneno yake. Atagundua mama ni muhimu kwake kuliko mtu yeyote huku duniani.

Ni mkubwa kiasi kuelewa nini kinachoendelea. Huwezi kumtendea vibaya halafu asijue umemtendea vibaya. Na wala sijawahi kumwuliza anampenda nani zaidi kati ya mama na baba. Kufanya hivyo ni vibaya. Mapenzi yangu kwake ni ya dhati na sifanyi mashindano ya nani anapendwa zaidi.

Anajua baba yake anampenda kwa dhati na yeye najua ananipenda. Kama mapenzi yangu kwake ni ya dhati sijui kwa nini baadaye aje abadili mtazamo wake. Haingii akilini.
 
Mnatunyanyapaa sana bana.

Kama nlivyokwambia, wakati wa ujana wangu nilifanikiwa kumkabidhi binti mmoja mimba ya kujitolea. Mtoto aliyezaliwa, niko naye hapa home akilelewa na mai waifu wangu. Mtoto wala hajui kama huyu si mama yake....Je mai waifu wangu hajawa kama mama wa huyu binti?....

Babu kama nilivyokujibu kule.....hamna anaeweza kuchukua nafasi ya mama mzazi (mwenye uchungu na mtoto wake that is) akaitendea haki asilimia mia moja!!!Kumpenda atampenda na mkumlea atamlea ila bado!!!Naongea kwasababu najua!!!
 
Hapa mtazunguka saana lakini point ni moja tu ambayo imeweka uzito wa hili la nani kama mama nayo ni kubeba mimba basi. Hayo mambo mengine kila mtu aweza fanya.
 
Muda si mrefu ulopita pale Mwananyamala kama sikosei miili ya maiti za vichanga ilikutwa imetupwa. Nani kama mama?

Mi kazi yangu ni kukugongea MaLIKE kwenye haya mayuziful posts yako mkuu.
 
Baba na Mama wote tunawapenda ila tukirudi kwenye nani kama mama jibu linabaki pale pale hakuna kama mama.
Ni mkubwa kiasi kuelewa nini kinachoendelea. Huwezi kumtendea vibaya halafu asijue umemtendea vibaya. Na wala sijawahi kumwuliza anampenda nani zaidi kati ya mama na baba. Kufanya hivyo ni vibaya. Mapenzi yangu kwake ni ya dhati na sifanyi mashindano ya nani anapendwa zaidi.

Anajua baba yake anampenda kwa dhati na yeye najua ananipenda. Kama mapenzi yangu kwake ni ya dhati sijui kwa nini baadaye aje abadili mtazamo wake. Haingii akilini.
 
Hapa mtazunguka saana lakini point ni moja tu ambayo imeweka uzito wa hili la nani kama mama nayo ni kubeba mimba basi. Hayo mambo mengine kila mtu aweza fanya.

na mimba zinazotungwa kwenye chupa ? chupa si inakuwa kama mama au?
 
Hakuna aliyepo kama baba yangu. Baba yangu ndo shujaa wangu. Ingawa nampenda mama yangu lakini mapenzi yangu kwa baba yanayazidi yale ya mama. Msiniulize kwa nini. Ni jambo zito sana.

Kwa hiyo hapo utaona kuwa inategemea na uhusiano mtu alionao na mzazi/ wazazi wake. Mimi binti yangu ananipenda kuliko maelezo. Ukimwuliza 'who is your hero?'.....anakujibu bila kusita 'my daddy is my hero'. Kwake ni 'nani kama baba'. Humwambii na humwelezi kitu kuhusu baba yake. She's a daddy's a girl and I savor every bit of it.

Hapo penye rangi, ndo umenena mkuu!

Kutokana na ule upendo mkubwa wa mama kwa watoto wake (kuanzia tumboni hata malezi), ndo maana jamii imesema hakuna kama mama! Na kwa uzoefu wangu mdogo, wababa wengi huwa hawana muda na watoto kabisa, kwahiyo unakuta watoto hawako karibu kabisa na baba yao. Baba anakuwa yeye ni wa kuhakikisha mahitaji muhimu yanapatikana nyumbani., basi. Lakini muda wa kucheza na watoto na kutengeneza mahusiano ya karibu hakuna! Baba anakuwa anaogopwa kweli...mhhhh!!!!!

Lakini najua kabisa wapo wababa wachache ambao watoto wao, watasema...hakuna kama baba, kwasababu wametengeza mahusiano ya karibu na watoto wao. Mtoto anapoumwa, sio kazi ya mama peke yake kukesha au kumwangalia mtoto!

Hayo ni mawazo yangu mimi!
 
Babu kama nilivyokujibu kule.....hamna anaeweza kuchukua nafasi ya mama mzazi (mwenye uchungu na mtoto wake that is) akaitendea haki asilimia mia moja!!!Kumpenda atampenda na mkumlea atamlea ila bado!!!Naongea kwasababu najua!!!

Nadhani hujanielewa. Huyu binti naekaa naye, mama yake alimtelekea. Na mai waifu wangu ndo anamlea.

Huyu aliyemtelekea naye ndo "NANI KAMA MAMA" kwa kuwa tu alibeba mimba kwa miezi tisa?
 
Kubeba mimba hakumfanyi mtu mama...kua na hisia na kichanga alichobeba ndo kunamfanya mtu mama!!
Ndo maana hao watupa vichanga hawaitwi wala hawajiiti mama....

Ah ha! Kwa hiyo hii blanket generalization ya nani kama mama haihusu. Ni vyema kuangalia kila situation on a case by case basis.

Kuna wengine tumefanya yote ukiondoa kunyonyesha kwa nyonyo. Tumenyonyesha kwa vyupa. Kuna kina mama wengine siku hawanyonyeshi kwa nyonyo. Ni chupa tu.

Tumebadilisha dirty diapers. Doctor visits hatukukosa. Tumekesha sana usiku. Si unajua watoto walivyo? Wengine usiku hawalali. Some of us have done it all and we still don't get appreciated by some people. I'm glad my Princess appreciates me and knows for a fact I'm irreplaceable.
 
Back
Top Bottom