Nani kama Mama Vs Nani kama Baba

Babu naona leo umetuamkia lakini ukweli utabaki pale pale hakuna kama MAMA ukielewa neno mama vizuri utaelewa na msemo una maana gani ingawaje sikatai na baba naye ana umuhimu wake ushawahi kuona watu wakijikwaa huwa wanaita nani/??
 
Ah ha! Kwa hiyo hii blanket generalization ya nani kama mama haihuuuu. Ni vyema kuangalia kila situation on a case by case basis.

Kuna wengine tumefanya yote ukiondoa kunyonyesha kwa nyonyo. Tumenyonyesha kwa vyupa. Kuna kina mama wengine siku hawanyonyeshi kwa nyonyo. Ni chupa tu.

Tumebadilisha dirty diapers. Doctor visits hatukukosa. Tumekesha sana usiku. Si unajua watoto walivyo? Wengine usiku hawalali. Some of us have done it all and we still don't get appreciated by some people. I'm glad my Princess appreciates me and knows for a fact I'm irreplaceable.

Kamanda hii sredi unaitendea haki.... yaani unanikonga moyo.

Nimekuvulia kofia.
 
hilo sio tatizo. Kwenye isue ya vichanga kutupwa hovyo wote baba na mama mnahusika, ukifuatilia sana wababa mnasababsha vichanga vitupwe kwa kuzikataa hizo mimba zenu. Hebu umtie binti mimba afu usimkatae uone kama kuna vichanga vitatupwa M/nyamala. ( sijasema wadada mbebe mimba hovyo then mtupe vichanga. Ni dhambi )
Muda si mrefu ulopita pale Mwananyamala kama sikosei miili ya maiti za vichanga ilikutwa imetupwa. Nani kama mama?
 
Babu naona leo umetuamkia lakini ukweli utabaki pale pale hakuna kama MAMA ukielewa neno mama vizuri utaelewa na msemo una maana gani ingawaje sikatai na baba naye ana umuhimu wake ushawahi kuona watu wakijikwaa huwa wanaita nani/??

Na hawa kina mama wanaotelekeza watoto nao bado wana sifa ya "NANI KAMA MAMA"?
 
Ukichukulia huo msemo literary kua hakuna kama mama na hivyo baba ana umuhimu utakua unakosea njia... Ni kwanini inasemekana hakuna kama mama?

Mama ni kiumbe ambae katika viumbe woote tunamchukulia sana for granted. Huyu mama ndo kakubeba wewe tumboni kwako (hebu naomba u pause kidogo na tafakari hili suala - kua the whole of you, mwili wako huo wote ulitoka ndani ya tumbo lake). Mama ni Mwalimu, rafiki, dakitari, mtabiri, mpenzi wa kweli, dereva na vitu vingine viingi ambavyo naamini hata wewe pia unaelewa. Asprin niseme nini hapa... Nani kama mama ??? Mama anaamini wewe ndo wewe no matter your weakness (sometimes anapalilia hata hizo weakness), Mama anakuambia mwanangu Aprin mimi nakupenda na as long as am still there you will always be safe, sitakubali dunia ikusumbue... Niambie mwanangu; unasema unahitaji niwaongeze wewe na mkeo mtaji - usijali nitaongea na baba....

Baba on the other hand ni nguza yako ya kuegemea, ni jeshi lako la kukimbilia iwapo kuna wasi wasi wowote wa mashambulizi, ni mtu akuoneshae kua hii dunia you can overcome anything ukitumia nguvu, determination, focus na akili. Ni mtu ambae anakusimamie but ikifika wakati wa wewe kusimama anakujulisha kua nawe sasa ni ngazi, anakwambia kabisa kama wewe huna hivi huna nafasi katika hii dunia hivyo jiandae kua defeated - na anakujulisha kua kama utashindwa kua mwanajeshi katika mambo yote yakuzungukayo na kukusumbua basi mi sio commander wako...

Ni wachache saana wamepata bahati ya kupata committed Fathers hata kama wamelelewa nao, but kwa wale woote walojaliwa kulelewa na mama zao ilikua ni rahisi kupata a committed mom though ndio kuna exceptions..


Asha D,
Nimependa sana jinsi ulivyomwaga utetezi wako hapa,
lakini kikubwa nachogundua hapa kwa mawazo yako,
na ya akina dada wengine hapa JF,
NI KATIKA UZAZI, yaani kubeba mimba, kunyonyesha nk.
ndipo ambapo mama anaonekana yeye ndo yeye na hakuna mwingine,
lakini hebu tujiulize, maisha yanajidhihirisha katika phase hiyo tu?
mbona mnasahau hatua zingine za maisha baada ya kuwepo tumboni kwa miezi 9,
kunyonya n.k.?

Pili, kama ndo hivyo, je wale akina dada wanaotupa watoto chooni, vichakani nao tuwaite NANI KAMA MAMA?
Je, wale akina mama wanaokaa na watoto wa kufikia na kila kutwa wanawatesa kwa mateso ambayo hata JEHANAMU unaweza usiyakute, je nao tuwaite NANI KAMA MAMA?

ASANTE,
NANI KAMA MUNGU?
 
Babu naona leo umetuamkia lakini ukweli utabaki pale pale hakuna kama MAMA ukielewa neno mama vizuri utaelewa na msemo una maana gani ingawaje sikatai na baba naye ana umuhimu wake ushawahi kuona watu wakijikwaa huwa wanaita nani/??

Wanaita "YESUUU" ama JESUS
 
Teh teh mpaka kieleweke leo mkuu nani kama baba?

Hakuna kama baba. Huu ndo msimamo wangu na ndo ukweli mtupu.

Hakuna wa kumlinganisha na baba yangu asee. Acheni utani kabisaaaa!

Kama hoja ni kuzaa, siku hizi chupa nazo zinazaa!....NANI KAMA CHUPA?
 
Kamanda hii sredi unaitendea haki.... yaani unanikonga moyo.

Nimekuvulia kofia.

Unajua nini kamanda? Hii nyuzi yako imenigusa sana. Kuna baba wengi sana ambao hawatendewi haki yao. Wababa tunajipinda na wakati mwingine kujinyima ili tuweze kuwapa wanetu misingi bora ya maisha lakini bado tu hatuthaminiwi kama inavyostahili.

Wengine tunafanya mengi kuliko hata hao mama zao waliowazaa lakini wapi. Hatupewi haki yetu. Inasikitisha sana mkuu. Laiti watu wangejua jinsi wengine tunavyowahangaikia wanetu labda wangeweza kututhamini.
 
Nadhani hapa unaangalia zaidi uchakachuzi wa maisha lakini in real sense ukitazama neno mama na majukumu yake ndo maana huu msemo unasimama na tukianza kutazama majukumu ya mama yaliyochakachuliwa unakosea kwa sababu hao hawasimami kwenye nafasi ya mama.

Huu msemo unasimama kwa maana ya mama na uwezo,hekima,uvumilivu pamoja na majukumu yake yote aliyotunukiwa na Muumba na ndio ilivo babu na itakavokuwa siku zote.



Nadhani hujanielewa. Huyu binti naekaa naye, mama yake alimtelekea. Na mai waifu wangu ndo anamlea.

Huyu aliyemtelekea naye ndo "NANI KAMA MAMA" kwa kuwa tu alibeba mimba kwa miezi tisa?
 
Ntake radhi babu. Niko ofcn bana kwenye laptop nafanya kazi ya ofisi then mdogo mdogo naingia Jf bosi akpita hanishitukii.

Hahahaha....JF adikshen!

Nakutaka radhi............Nani kama baba?
 
Hao sio kina mama sababu hawajui wala hawako tayari kuwa mama,hapa anatazamwa mama aliye mama na amabaye amevaa uhusika wa kimama.
TUSICHANGANYE MADESA SASA HATA TUNAPOSEMA HAKUNA KAMA BABA SIO WOTE NI KINA BABA WENGINE NI WAMWAGA MBEGU TU.


Na hawa kina mama wanaotelekeza watoto nao bado wana sifa ya "NANI KAMA MAMA"?
 
Kama baba wapo. Kama mama hakuna.

Wakina nani kama baba? maana kwenye kubeba mimba siku hizi mama analinganishwa na chupa na kwenye kunyonyesha mama ana linganishwa na maziwa ya unga kibao yamejaa kwenye ma super market kwa hiyo walio kama mama wapo
 
Back
Top Bottom