Nani kama Magufuli?

Nani kama Magufuli?

Mayor Quimby

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2021
Posts
6,750
Reaction score
14,491
IMG_8106.jpeg

Just because I feel

My hero, mwamba
 
kwa mtu anayetazama mpangilio wa matukio, basi ni wazi CCM haina muda mrefu madarakani, Kifo cha JPM kimeonesha wazalendo hawana nafasi kwenye hiki chama, mauaji ya Oct 29 ndo kimekizika rasmi hiki chama, mitandao ya kijamii imefungua minyororo kwa watanzania wengi waliyofungwa na CCM kwa muda mrefu kifikra, yaani elimu ya hali halisi ya Tanzania inazidi kushika kasi ndani ya vichwa vya watanzania kupitia mitandao.
 
Nilichojifunza na ambacho naushauri moyo wangu, Mtu mweusi aliye na mapenzi mema na ya dhati kwa mwenzake, nchi yake na jamii yake, hawa watu ni wa kutafuta sana na ikitokea bahati watu hao wakae kwenye nafasi ya juu ya uongozi, hufanya kazi kama wanajifanyia wao na familia zao

Mtu kama huyu akitokea na akaonyesha dalili zote za uzalendo, nasemaje, mtu huyo alindwe kimwili na kiroho tena kwa nguvu zote, na watu wawe tayari kuwadhuru wote wanaomwinda yeye

Watu aina hiyo siyo lazima watokee chama tawala au upinzani

Watu hawa mara nyingi huwa kama zawadi tu na hutokea tu kama muujiza na kupotea kwao ni hivyohivyo
 
kwa mtu anayetazama mpangilio wa matukio, basi ni wazi CCM haina muda mrefu madarakani, Kifo cha JPM kimeonesha wazalendo hawana nafasi kwenye hiki chama, mauaji ya Oct 29 ndo kimekizika rasmi hiki chama, mitandao ya kijamii imefungua minyororo kwa watanzania wengi waliyofungwa na CCM kwa muda mrefu kifikra, yaani elimu ya hali halisi ya Tanzania inazidi kushika kasi ndani ya vichwa vya watanzania kupitia mitandao.
NI MWANADAMU GANI ALIWAHI KUISHI MILELE ? KWAKUWA MALKIA ELIZABETH ALIFARIKI WAKATI WA KITI CHAKE INAMAANISHA KUWA DOLA YA UFALME ILIKUWA INAKUFA MWISHONI ? WANADAMU HUFA , VIONGOZI HUFA. KIFO NI IBADA , SO AS YOU AND I , SOTE NJIA YETU NI MOJA . MUNGU ATUREHEMU SOTE . MWENYEZI MUNGU AMPUMZISHE MAHALI PEMA PEPONI KIONGOZI WETU. ILA HIZI PROPAGANDA ZENU HAZINA WAKATI KWA DUNIA YA SASA.
 
kwa mtu anayetazama mpangilio wa matukio, basi ni wazi CCM haina muda mrefu madarakani, Kifo cha JPM kimeonesha wazalendo hawana nafasi kwenye hiki chama, mauaji ya Oct 29 ndo kimekizika rasmi hiki chama, mitandao ya kijamii imefungua minyororo kwa watanzania wengi waliyofungwa na CCM kwa muda mrefu kifikra, yaani elimu ya hali halisi ya Tanzania inazidi kushika kasi ndani ya vichwa vya watanzania kupitia mitandao.
Ukiniuliza mimi kwa muda mchache nilio ishi hapa Duniani, nitakujibu maendeleo au mabadiliko hayaletwi na Chama bali mtu mmoja na utashi wake. Angalia mambo mengi mazuri tuliyo nayo kwa sasa Duniani hayakuletwa na vyama isipokuwa mtu. Hivyo haya mambo ya mavyama vyama ni upuuzi kinaweza kuja chama kingine chochote kile na bado mambo ya hovyo yakawa mara mbili zaidi.

ushauri wangu tuheshimu vichwa vya watu (talented figures) na sio mavyama.
 
Hana utakatifu huo, huyu ndio chanzo cha bunge la hovyo la kijani tupu..!!

Sheria nyingi mbovu zilipitishwa kwake, uchawa na kuziba wananchi midomo.

Ni vile Samuya karuhusu utekaji uendelee toka kwa mtangulizi wake na mauaji Dec 29 ndio yamefanya chuki izidi kwake.

Nina uhakika naye angekuwepo tungekuwa na M7 wetu sasa hivi..!!

Tatizo watanzania tunajifanya wasahurifu ila hiko chuma kilikuwa ni chanzo cha haya yote.
 
Ni mambo ya ajabu sana tatizo la watanzania wengi ni wasahaulifu na huu ndo mtaji wa ccm

Magufuli ni architect wa mambo mengi sana ya hovyo ambayo mpaka leo yapo yes ana mazuri yake ila mabaya ni mengi kuliko mazuri
 
Nilichojifunza na ambacho naushauri moyo wangu, Mtu mweusi aliye na mapenzi mema na ya dhati kwa mwenzake, nchi yake na jamii yake, hawa watu ni wa kutafuta sana na ikitokea bahati watu hao wamekaa kwenye nafasi ya juu ya uongozi, hufanya kazi kama wanajifanyia wao na familia yao

Mtu kama huyu akitokea na akaonyesha dalili zote za uzalendo, nasemaje, mtu huyo alindwe kimwili na kiroho tena kwa nguvu zote, na watu wawe tayari kuwadhuru wote wanaomwinda yeye

Watu aina hiyo siyo lazima wawe watokee chama tawala au upinzani

Watu hawa mara nyingi huwa kama zawadi tu na haitajarisha kule watatoka
Shida ni kwamba hatuna utaratibu huo chama kwanza nchi baadae sisi ni waajabu kuliko hayo maajabu yenyewe
 
Back
Top Bottom