Mlinganishe Prof Kabudi vs Profesa J, nitakuambia (kwa mtazamo wangu) Profesa J ana akili nyingi kuliko Profesa Kabudi (ni kwa sababu elimu ya mtu hupimwa pia kupitia matendo yake, mchango wake kwenye jamii, nk). Na ukija kwa huyo mwingine, tulishakubaliana kitambo!
Udaktari unaotambulika rasmi ni wa aina mbili tu; wa kusomea shahada ya kutibu binadamu, wanyama, nk. Na ule wa PhD unaohusiana na ukufunzi kwenye vyuo, nk! Nyerere alipewa hizo PhD za heshima zaidi ya 20 kutoka vyuo tofauti duniani kote! Na bado hakuwa kujiita Daktari! Vivyo hivyo kwa Mkapa!
Ni vizuri kama huna sifa nilizozitaja hapo juu, usikubali kuitwa Daktari! Kwa sababu utakuwa umekubali kudhalilishwa mbele za watu mchana kweupe.