Nani huchukua mirabaha ya wasanii waliofariki?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,307
33,925
Punde nilikuwa nasikiliza Wimbo wa Sam Wa ukweli uitwao "Sina Raha" kama njia ya utafiti niliokuwa nafanya.

Kwenye "YouTube" wote waliouweka Wimbo huo, kulikuwa na matangazo mbalimbali kwenye channel hizo za YouTube.

Likanijia wazo kuwa wasanii waliokufa kazi zao zinapotumiwa na watu mbalimbali jee hupata mirabaha?

Msanii akifa haki za kazi zake husimamiwaje?
 
Punde nilikuwa nasikiliza Wimbo wa Sam Wa ukweli uitwao "Sina Raha" kama njia ya utafiti niliokuwa nafanya...
Kuna warithi mkuu,
Msanii anapo enda kusajili kazi zake Cosota moja wapo ya requirements ni warithi wa kazi zako endapo umefariki,
Warithi watanufaika na kazi za mbunifu huyo hadi miaka 50 tokea kifo cha huyo mbunifu
 
Yale matangazo makubaliano yakoje. Maana inawezekana "Youtuber" analipwa na YouTube Sasa Hadi warithi wapate gawiwo lao inakuwaje!!??

Mfilisiti
Hao youtuber wanafanya makosa, na hairuhusiwi kisheria kuuchukua wimbo wa msanii na kuuweka kwenye chanel yako, Msanii ananufaika moja kwa moja kwenye digital platform kama YouTube kwamaana ya idadi ya streaming&download,so ni kazi ya msanii kuhakikisha wimbo wake unakaa kwenye chanel yake
 
Safi.

Maana channel Moja nikaona watu zaidi ya Milioni 2.5 waliuangalia ule Wimbo.

Hizi familia zetu mtu akifa anakuwa amekufa sijui kama huwa zinafuatilia.
 
Hao youtuber wanafanya makosa, na hairuhusiwi kisheria kuuchukua wimbo wa msanii na kuuweka kwenye chanel yako, Msanii ananufaika moja kwa moja kwenye digital platform kama YouTube kwamaana ya idadi ya streaming&download,so ni kazi ya msanii kuhakikisha wimbo wake unakaa kwenye chanel yake
Na pia cha kuongezea Allen Kilewella youtube wana mfumo wa kugundua maudhui yenye hati miliki, unaitwa Content ID.

Ukipost kitu chenye hati miliki bila leseni kinafutwa, ama kinaendelea kubaki hewani ila mapato yanaenda kwa mmiliki, inategemea mmiliki ameamuaje.

Sasa wasanii wengi wanakuaga na licensing partners wa kuhakikisha kazi zao hazisambazwi hovyo. Hawa licensing partners ndo wanasajili vitu kwenye Content ID.

Kwahiyo hao wanaopost miziki ya watu unaweza kuta hawaingizi chochote.
 
Dunia ya ubepari haina huruma na wewe au Familia yako.
Swali alikuwa ana haki miliki za hizo nyimbo? Kuimba nyimbo au kutunga haikupi haki miliki kwa 100%.
Je hizo nyimbo cosota zimesajiliwa kwa jina la Nani? Je mirathi ya MAREHEMU walitambua hizo nyimbo kama sehemu ya mali za MAREHEMU? Kifupi hili ni funzo kwa wasanii watumie wanasheria kuweka mambo Yao Sawa kwa maana kwenye burudani dhuluma ni kitu cha kawaida Sana.

Sent from my SM-A035F using JamiiForums mobile app
 
Punde nilikuwa nasikiliza Wimbo wa Sam Wa ukweli uitwao "Sina Raha" kama njia ya utafiti niliokuwa nafanya.

Kwenye "YouTube" wote waliouweka Wimbo huo, kulikuwa na matangazo mbalimbali kwenye channel hizo za YouTube.

Likanijia wazo kuwa wasanii waliokufa kazi zao zinapotumiwa na watu mbalimbali jee hupata mirabaha?

Msanii akifa haki za kazi zake husimamiwaje?
Mirabaha ya wasanii waliotangulia mbele za haki ni sehemu ya mirathi kwa warithi wake kwa muda wa miaka 50 tangu kifo kitokee kwa msanii.

Kibongobongo watu kuleee jikoni wanapita nayo
 
Punde nilikuwa nasikiliza Wimbo wa Sam Wa ukweli uitwao "Sina Raha" kama njia ya utafiti niliokuwa nafanya.

Kwenye "YouTube" wote waliouweka Wimbo huo, kulikuwa na matangazo mbalimbali kwenye channel hizo za YouTube.

Likanijia wazo kuwa wasanii waliokufa kazi zao zinapotumiwa na watu mbalimbali jee hupata mirabaha?

Msanii akifa haki za kazi zake husimamiwaje?
Wasanii hawalipwi moja kwa moja bali wenye hatimiliki ndio wanalipwa ili wawalipe wasanii. Na hapo ndipo mziki na biashara yake ulipo.
 
Punde nilikuwa nasikiliza Wimbo wa Sam Wa ukweli uitwao "Sina Raha" kama njia ya utafiti niliokuwa nafanya.

Kwenye "YouTube" wote waliouweka Wimbo huo, kulikuwa na matangazo mbalimbali kwenye channel hizo za YouTube.

Likanijia wazo kuwa wasanii waliokufa kazi zao zinapotumiwa na watu mbalimbali jee hupata mirabaha?

Msanii akifa haki za kazi zake husimamiwaje?
Msanii akifa kazi zake za Sanaa zote zinarithiwa kama Mali za marehemu nyingine tu ,mfano ni Bob Marley watoto wake sa hivi ndo wanasimamia kazi zake na Hadi Wana account za social media za bob Marley na Twitter na kwenye list ya wasanii marehemu wanaopiga pesa nyingi kwenye mauzo ya kazi zao uwa Bob na Michael Jackson lazima wawepo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom