Album ya Mkuki Moyoni ya Afande Sele

Feb 6, 2024
40
50
AFANDE WA MOROGORO MFALME WA TANZANIA.

Toka mwaka 2002 mpaka sasa 2022 ni miaka 20 imepita toka album ya "mkuki moyoni" toka kwa Afande Sele izame sokoni. Mwaka 2004 hii album kwa uzito wa nyimo zake ilitosha kabisa kumtangaza mfalme wa rhymes ni Afande Sele.

Mkuki moyoni ni miongoni mwa album bora kwa mziki wa kizazi kipya mpaka Hip-hop kwa Tanzania kwa mda wote. Ubora wa hii album unabebwa na ubora wa tungo na washiriki ambao walipewa nafasi ya kutia mashairi kwenye nyimbo.

Wimbo wa "mayowe" aliyoshirikisha Jay Mo ndio wimbo wa kwanza kutoka kwenye hii album na ndio wimbo ambao ulimtambulisha kama msanii huru yote baada ya kua karibu sana na Sugu kwa mda mrefu kidogo.

Kumbukumbu zinaonesha hata wimbo wake wa kwanza "afande anasema" ulitoka akiwa kwa Sugu na ukawekwa katika album ya Sugu.

Fununu zilisema mwanzoni kabisa album ilitakiwa kupewa jina la "mtazamo" lakini mtu mzima Afande Sele akaona bora jina na kuipa jina la "mkuki moyoni" wimbo ambao ulibeba historia nzima ya maisha yake.

Uzinduzi wa hii album ulikua mkubwa sana yani raia walijaa sana yote kutokana na ukubwa wa Afande Sele. Pamoja na kujaza mashabiki inasemekana pia watu walimtapeli mfalme mpaka ikasababisha kitokuelewana na baadhi ya wasanii ambao walialikwa kwenye uzinduzi.

Mkuki moyoni ni album ilitoka chini ya P funk pale Bongo Record. Ukisikiliza hii album utagundua Afande toka mda mrefu anapenda ushurikiano na wasanii wenzake japo wasanii wenzake wanaogopa kumshirikisha kwa hofu ya kufunikwa kimashairi.

Album ilikua na nyimba 10.
1. Mkuki moyoni ft Daz Baba
2. Kama nitapata ukimwi ft K basil
3. Mayowe ft J Mo
4. Mayowe part 2 ft Papii Kocha
5. Mtu na Pesa ft Bwana Sam
6. Nikiwa Mbali ft Mc Koba
7. Habari kamili ft Ay & Black Rhyno
8. Mimi na wewe basi ft Mr Nice
9. Mtazamo ft Solo Thang & Prof J
10. Mpenzi njoo ft Bwana Sam.

Cover ya hii album ilisadifu kile kilichomo kwenye album hii. Tutagusia nyimbo chache kuona ilikuaje kuaje.

Mkuki moyoni ndio wimbo uliobeba album na ndio jina la Album. Huu wimbo unaelezea kisa ambacho kilimtokea Afande Sele miaka ya nyuma. Mwaka 2017 Afande sele alipost picha yake ya kwanza akiwa na mama ake mzazi. Mwaka 2022 Afande Sele ameondokewa na mama ake mzazi.

Wimbo unaanza kwa kiitikio toka kwa Daz Baba akisema

Mateso unayonipa mwilini
Ni vigumu we kuyatambua usoni
Umeshanichoma mkuki moyoni
Siwezi tena kuishi duniani na wewe
Nionyeshe huruma yako we mama (we mama)
Nionyeshe huruma yako we mama (we mama)
Nionyeshe huruma yako we mama (we mama)
Kabla mimi sijafa kiama

Ukisoma chorus unapata picha kubwa toka kwa Afande Sele kua kuna mda ambao alitaka apate upendo toka kwa mama ake mzazi pamoja na yote akamuomba mama ake amuonyeshe japo huruma kidogo aweze kuishi kwenye hii dunia lakini mama alikaza.

Baada ya chorus kupita ndipo beti ya kwanza inaanza toka kwa Afande Sele.

Aah! Kabla kifo cha baba nilipata nilichotaka
Na toka alipoanguka sioni hata pa kushika
Dingi alivyonipenda nashindwa hata kueleza
Ndugu zangu walinuna walisema ananidekeza
Ndo maana alipokufa wakapanga kuniangamiza
Visa vingi wanafanya ila mimi namuachia Mungu
Mkombozi uliye juu, na muumba nchi na mbingu
Kama kweli unayaona matendo ya walimwengu
Naamini utasimama na utalinda maisha yangu
Maana siko salama na kisa ni urithi wangu
Ndugu wameniandama waipoteze roho yangu
Nami sina pa kwenda, na sina mtetezi wangu
Mama alishakimbia na akaniacha peke yangu
Nateseka kivyangu, mchana jua ni langu
Usiku mvua ni yangu
Oh!

Ukisoma beti hii inaonesha labda mama alimkimbia Afande Sele baada ya kuona kuna uzinguaji kwenye mali za mumewe na mengine mengi akaona bora akimbie huku akimuacha mtoto ake sehemu ambayo sio nzuri kuishi japo marehemu baba ake aliacha vitu vingi.

Sasa, baada ya kifo cha baba
Mama aliniacha pekee, kasonga mbele kivyake
Miaka mingi ikapita sikupata salamu zake
Kwenye vyombo vya habari nikatuma ujumbe wake
Tena kuna gazeti nilitoa hadi picha zake
Waugwana walioziona walisema yupo Kigoma
Na zaidi wakanieleza kuhusu maisha yuko njema
Nikaenda kumtazama
Nipate kuhakikisha kama alipo ni salama
Mnajua uchungu wa mama, eh?
Hasa mkipotezana kwa muda usiojulikana
Kwa bahati njema nikampata
Bahati mbaya ikafata, najuta yalionikuta
Ni vigumu kuamini lakini ukweli nitakufa
Mama alinikataa, kwanza sikumuelewa nikabaki namshangaa
Kisha nikamuuliza, vipi mama una kichaa?
Mwenyewe umenizaa, hivi sasa unanikataa!
Jibu alilorudisha sikuamini kwa masaa
Alisema sikujui na geti akafunga pah!
Shoga zake jirani wakanieleza kwa ufasaha
Kumbe kaolewa tena na amesema hajazaa
Hivyo angenikubali mumewe angemkataa
Mwili ulikosa nguvu nikabaki nimeduaa

Hiyo beti ya pili ukisoma unaona wazi mama alipokimbia huku nyuma alimpa kazi kubwa mtoto wake kumtafuta kila kona. Alitumia kila njia mpaka akaja kufahamu mama ake alipo na akamfata cha ajabu mama nae akamtosa apo ndipo ukirudi kwenye chorus ndio unapata picha kwanini alitaka japo apate huruma ya mama kidogo.

Kweli nilishangaa
Mama ‘angu alionizaa kuniacha kwenye mataa
Takribani nusu saa sikuongea kama bubu
Watu walinizunguka, nikainama chini kwa aibu
Ntaishi vipi ugenini, akilini sikuwa na jibu
Kule sikuwa na ndugu, nkaishi maisha ya tabu
Sometimes ilinibidi nilale nje kama bawabu
Mbu, baridi kali, kwa kweli nilipata tabu
Maisha kwa kiumbe mimi yalionekana kama adhabu
Na kama unavyoelewa wenye pesa wengi waarabu
Wapo wenye ustaarabu, ila wengine hawana adabu
Nilipoomba msaada walitaka kwanza taarabu
Washenzi, hamna adabu
Ndivyo mimi nilivyo wajibu
Dhiki ukiendekeza haki ya Mungu watakuharibu
Hilo nililelewa nikaliweka kumbukumbu
Nilipokosa chakula ilibidi nilale njaa
Nikikosa pa kulala nazuga kwenye mitaa
Maisha kifo mkononi, kifupi mi niliishi kama mtoto wa mtaani
Ndo maana naona mbali, naona mbali
Kwa darubini kali!

Beti ya tatu ilimaliza kila kitu kuhusu safari yake ya kumsaka mama ake .

Kama nitapata ukimwi hui wimbo ulizungumzia kuhusu gonna hatari la ukimwi. Kama akipata ni jinsi gani ataweza kujilinda na kulinda wenzake.

Mayowe zote mbili zilitaka watu wasipige sana kelele kwa wale ambao kusikia na kuelewa kwao ni ngumu yani bora kuwaacha yawakute ndio wataelewa.

Watu na fedha ulizungumzia jinsi nguvu ya pesa ilivyo huku nguvu ya utu ikipotezwa vibaya mno na nguvu ya pesa.

Nikiwa mbali huu wimbo ulizungumzia mkoa wa Morogoro mpaka utunzaji wa mazingira katika mkoa wa Morogoro.

Habari kamili ulizungumzia mambo mbalimbali ya kwenye jamii yetu jinsi yalivyo.

Mimi na wewe ni wimbo wa mapenzi umezungumzia uvumilivu na upendo mpaka kuachana

Mpenzi njoo huu nao ulizungumzia kuhusu mapenzi na upendo wa dhati kabisa.

Mtazamo huu wimbo nitakupa mashairi yake na utajua ulikua mtazamo wa nini?

Solo Thang]
Yeah…
Yeah…
Hakuna S bila O
L bila O
Mwingine aitwe’ Thang bila Solo
Shupavu’ awajibike kama Apollo
Jay, Afande!
Ni ukuta’ wapi uchochoro?
Hakuna S bila O
L bila O
Mwingine aitwe’ Thang bila Solo
Shupavu’ awajibike kama Apollo
Jay, Afande!
Ni ukuta’ wapi uchochoro?
Yo Naghani’ ni mtazamo wa fani
Ile dhana ni uhuni wameleta hawa katuni
Kuna ku-rap na kumbwata
Ma-reaper na ma-rapper
Katuni, Tungo tata
Wapi ulipo we jaku?
Unakuwa mtumwa ili upewe promo kuuza
Au kama ni binti’ ukalale kwa prodyuza
Ma-Promoter wana uma tu’ hawajui na kupuliza
Na siku wakipuliza jua kidonda kishaoza
Natamani kuwa huru mnyonyaji asinidhuru
Wanaitwa “ma-Emcee” hawajui mitindo huru
Huu mtazamo wangu’ naona vingi vioja
Yaani watangazaji sasa’ ndo ma meneja
Vidato sita nlivyopitia
Ndivyo vinavyonisaidia
Mbunifu ukiizingatia
Hata wakinibania
Ni kipaji tu
Ni mtazamo tu
Msikasirike wash’kaji
Haya mawazo tu
Ulamaa…

Ukianza na beti ya Solo anakuonesha wazi kwenye huo wimbo hakuna mnyonge wa mashairi "Jay, Afande ni ukuta wapi uchochoro" kwa kupima kwako apo tu unaona kabisa hakuna mnyonge wa mashairi kwenye huu wimbo.

Ni mtazamo zamo emcee usiogope kivuli
Bora ukemee mabaya na usifie mazuri
Ni mtazamo zamo emcee usikwepe umande
Okoa sanaa ya Bongo ili uchumi upande
Ni mtazamo zamo emcee usiogope kivuli
Bora ukemee mabaya na usifie mazuri
Ni mtazamo zamo emcee usikwepe umande
Okoa sanaa ya Bongo ili uchumi upande
Kwi kwi, Ulamaa, Professor Jay, Afande

Chorus ndio imepita apo beti ya pili inafata

Ni mtazamo rap inakuwa ni mikingano
Sasa watoto wadogo wanajiita watu wa makamo
Wanakwenda hatua mbili, wanarudi kumi na kujipongeza
Bila kuzingatia hatua nane walizopoteza
Hao ni mafukara wa akili zao na uwezo wao
Wasiotambua nini na nini ni hatima zao
Magwiji vichwa chini nadhani wanatunga sheria
Lakini sheria msumeno isije ikawarudia
Yes, ma-underground wanafanya rap inang’ara
Lazima muwe vinara imara kwenye msafara
Rap na mazingaombwe abadani, haviendani
Msitegemee tawilee iwaokoe katika fani
Ni vyema ukafikiri kabla ya kufanya maamuzi
Tazama mbele usije ukanywa chai kwa mluzi
Naamini askari shupavu lazima upitie depo
Vinginevyo ndugu yangu utakuwa unapaka rangi upepo
Kama unapata moja kwanini usipate na mia
Hiyo inawezekana kwa wote mlio na nia
Sioni sababu za msingi kuomba kwenye mitaa
Kama una kipaji iweje ufe na njaa

Beti ya tatu
Asante Professor Jay
Majani na Ulamaa mmegusa n’napopataka
Nami kwenye mtazamo nina jambo nataka kuweka
Maana kila kukicha emcees wanaongezeka
Nasema very nice, yes rap kama dhehebu
Emcees kama wafuasi
Wingi wa wasanii unaonesha ni dini safi
Yaani imekubalika, waumini tuko wengi
Lakini bado nashaka
Sijapata uhakika, wote tumesadiki
Ama wengine ni fake mmetumwa kama mamluki
Maanake hamna maana
Mna-rap mnadi rap, mistari imekosa vina
Yenye vina haina maana
Na kila mnapokaa mnapenda kusengenyana
Mnapenda kutetana na mnapenda kurumbana
Mimi naogopa sana
Kwa jinsi navyoelewa mwishoni mtatukanana
Ama inawezekana mwishoni mkaja chinjana
Na wote tunao-rap tuonekane hatuna maana
Wapi ilipo Taarab
Ilikuja kwa kishindo, hata wagumu walishausudu
Kwa ajili ya marumbano mwishoni ikafa kibudu
Shabiki piga simu, changia mawazo yako
Nani tutamlaumu, kama rap ita-cease kwa kuendekeza upuuzi
Nani tumchune ngozi, producer aliyerekodi
Ama labda DJ anaepiga kwenye kipindi
Wengi wanapenda rap, ajabu rap haiwapendi
Waungwana wanaiacha, wapumbavu hawaambiliki
Hivi kwani lazima tuwe wote wanamuziki
Mi nadhani ingetosha wengine mbaki ushabiki
Huu ni wangu mtazamo masela msijenge chuki
Hata na Majani, yoh

Kwa kupimia tu huu wimbo ungetoka miaka hii unaona ni nani angeweza kufiti apo kimashairi?

Baada ya hii album na ushindi wa rhymes mtu mzima akatoka na album yake ya pili "DARUBINI KALI "
FB_IMG_1709979465347.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom