Mirabaha itumike kuwawekea wasanii Bima ya Maisha

gim

Senior Member
Jan 28, 2022
131
239
Natumaini wote mu wazima.

Wiki mbili zilizopita tumeshuhudia historia ikiwekwa kwenye muziki wa Tanzania na wasanii wake.

Wasanii katika makundi mbalimbali wameanza kupokea matunda ya jasho zao kutoka serikalini kupitia kwa washirika wake, imekua ni faraja kubwa sana kuona makundi hayo yakipokea haki zao ambazo kwa miaka mingi zimekua ni kama kama ndoto kwao.

Kongole kwa wasanii waliosimama kidete katika kupigania wasanii wenzao ili waweze kupata haki zao wapo wengi sana ila hapa nitatambua mchango wa dada yangu witness kibonge mwepesi, huyu amekua mstari wa mbele kupigania haki za wasanii ili serikali kupitia cosota na washirika wake itoe mirabaha kwa wasanii na kitu ambacho kimetekelezeka katika kipindi hiki.

Serikali kupitia cosota wameweza kugawa stahiki kwa wasanii wa makundi ya bongo fleva, mziki wa injiri, mziki wa dansi n.k.
Japokua serikali imeanza kugawa mirabaha hiyo kwa wasanii lakini inaonekana ni haba kulingana na ukubwa wa kazi walizofanya, kiasi cha shilingi milioni 7 kwa msanii kama Ali Kiba ni ndogo sana kulinganisha na kazi kubwa ambayo ameifanya kwa miaka mingi ndani ya bongo fleva.

Lakini pia kumekua na malalamiko kutoka kwa washirika wa kutengeneza hizo kazi kukosa asilimia katika mirabaha hiyo, hali hii imeweka doa katika jambo hilo kwa kuonekana limefanyika bila kufanyika utafiti wa kutosha.

Tumeshuhudia kwa kiasi kikubwa wasanii mbalimbali wengi wakipitia misukosuko ya kimaisha pindi muda wao unapokwisha, wengi wamekuwa hawana tena uwezo wa kujiingizia kipato kupitia muziki wao hivyo kuingia katika matumizi ya madawa ya kulevya.

Mifano iko mingi ya wasanii hao waloingia kwenye matumizi ya madawa baada ya maisha yao ya kimuziki kwenda mlama.

NINI KIFANYIKE
Serikali iangalie namna itakavyoweza ili kuwawekea bima ya maisha wasanii wote kupitia mirabaha yao kwani kusema umkabidhi msanii laki tatu au mbili kwa mwaka hii si sawa na ni kushusha hadhi zao, hivyo mirabaha ielekezwe moja kwa moja kwenye bima ya maisha ya wasanii hao ili matatizo yakitokea msanii anaweza kuhudumiwa na si kusubiri michango ya wananchi.

N:b Tujifunze kwa hili lililotokea kwa msanii nguli kabisa wa muziki Tanzania
 
BIMA ya maisha inakatwa kwa mwaka...ukiisha mwaka hujafa au kuipata majanga imeenda...next year unapaswa kuikata tena..sasa kwa idea yako unamaanisha serikali isiwalipe kabisa wasanii mirahaba Yao itumike kuwakatia BIMA ya maisha?
 
Natumaini wote mu wazima.

Wiki mbili zilizopita tumeshuhudia historia ikiwekwa kwenye muziki wa Tanzania na wasanii wake.

Wasanii katika makundi mbalimbali wameanza kupokea matunda ya jasho zao kutoka serikalini kupitia kwa washirika wake, imekua ni faraja kubwa sana kuona makundi hayo yakipokea haki zao ambazo kwa miaka mingi zimekua ni kama kama ndoto kwao.

Kongole kwa wasanii waliosimama kidete katika kupigania wasanii wenzao ili waweze kupata haki zao wapo wengi sana ila hapa nitatambua mchango wa dada yangu witness kibonge mwepesi, huyu amekua mstari wa mbele kupigania haki za wasanii ili serikali kupitia cosota na washirika wake itoe mirabaha kwa wasanii na kitu ambacho kimetekelezeka katika kipindi hiki.

Serikali kupitia cosota wameweza kugawa stahiki kwa wasanii wa makundi ya bongo fleva, mziki wa injiri, mziki wa dansi n.k.
Japokua serikali imeanza kugawa mirabaha hiyo kwa wasanii lakini inaonekana ni haba kulingana na ukubwa wa kazi walizofanya, kiasi cha shilingi milioni 7 kwa msanii kama Ali Kiba ni ndogo sana kulinganisha na kazi kubwa ambayo ameifanya kwa miaka mingi ndani ya bongo fleva.

Lakini pia kumekua na malalamiko kutoka kwa washirika wa kutengeneza hizo kazi kukosa asilimia katika mirabaha hiyo, hali hii imeweka doa katika jambo hilo kwa kuonekana limefanyika bila kufanyika utafiti wa kutosha.

Tumeshuhudia kwa kiasi kikubwa wasanii mbalimbali wengi wakipitia misukosuko ya kimaisha pindi muda wao unapokwisha, wengi wamekuwa hawana tena uwezo wa kujiingizia kipato kupitia muziki wao hivyo kuingia katika matumizi ya madawa ya kulevya.

Mifano iko mingi ya wasanii hao waloingia kwenye matumizi ya madawa baada ya maisha yao ya kimuziki kwenda mlama.

NINI KIFANYIKE
Serikali iangalie namna itakavyoweza ili kuwawekea bima ya maisha wasanii wote kupitia mirabaha yao kwani kusema umkabidhi msanii laki tatu au mbili kwa mwaka hii si sawa na ni kushusha hadhi zao, hivyo mirabaha ielekezwe moja kwa moja kwenye bima ya maisha ya wasanii hao ili matatizo yakitokea msanii anaweza kuhudumiwa na si kusubiri michango ya wananchi.

N:b Tujifunze kwa hili lililotokea kwa msanii nguli kabisa wa muziki Tanzania
Shusho alipokea 4m TZS? Seriously?
 
Attachments

  • mchengerwa2.jpg
    mchengerwa2.jpg
    126.4 KB · Views: 6
Back
Top Bottom