Nani ameweka hizi bei elekezi za taxi pale Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere?

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,016
9,885
Mbali na uwepo wa taxi mtandao kama Uber, bolt nk, bado Watanzania tuko nyuma ya muda.

Karne ya 21. bado tunakomaa na namna ya zamani ya kufanya biashara. Sisemi kwamba watu wafanye taxi kizamani, kwa kuwa kuna maeneo madereva wa taxi mtandao hawataki kwenda.

Hata hivyo, walioweka bei hizi za taxi wametumia vigezo gani kuweka bei kubwa kiasi hiki. Aidha mbona maeneo mengine hayapo?

1706104284866.png
 
Nimeangalia tax mtandao hapa nilipo Mikocheni hadi uwanja wa ndege gharama ni Tsh 24,000 kwa gari, lakini bei za hao zinasema Tsh 60,000. Bei zao hazina uhalisia nadhani zitakuwa zimewalenga foreigners. Wabongo wachache wanaweza kukubaliana na hizo nauli.

Hao jamaa wapunguze ubinafsi, watanzania siyo matajiri.
 
Sasa wewe una hela ya kupanda ndege halafu huna hela ndogo ya taxi?
Any way hii ni kawaida hata mambele huko, na ukiita uber au taxi binafsi, kuingia au kushusha wanachajiwa.
Hao Taxi wamesajiliwa kufanya kazi hapo tu airport, kwa hiyo lazima wajilinde kimaslahi.

Mna bahati ka airport kadogo unaweza kutembea mpaka nje barabarani, Airport kama Heathrow au Schiphol ni unatembea maili kadhaa ndio utaona nje.
 
Back
Top Bottom