Nani amewahi kuziona Torati na Injili halisi?

Nani amewahi kuziona Torati na Injili halisi?

Tunazungumzia uhalisia siyo udini mkuu. Njoo na hoja ili tuzichambua kwa manufaa ya wote.
Shida mmemezeshwa uongo, halafu hamuufanyii utafiti, wapinzani wote wa biblia au wanaosema biblia imebadilishwa hakuna hata mmoja anayejibu hoja ,Huwa ni propaganda tu kama hizi unazoleta hapa

Wengi wawanaosema Biblia imebadilishwa wanapobaini ushahidi wa manuscripts za Dead Sea Scrolls na Papyrus 52, hawawezi kutoa hoja ya kisayansi inayothibitisha Biblia iliharibiwa au ilibadilishwa kwa makusudi maana manuscripts hizi zimebaki kuwa na maandiko ya kale sana ambayo yanathibitisha usahihi wa Biblia ya leo.

Mfano nimeona unasema eti zilichomwa Alexandria 😂😂

Mimi nitakuuliza maswali machache

Alexandria Unajua ulijengwa lini?

Halafu nitakuletea hapa manuscripts za kabla ya hiyo Alexandria zipo Hadi Leo na zimethibitishwa kisayansi kabisa ni za miaka karibu 250 kabla ya Yesu

Na Yesu alizinukuu ,

Na uhakika ttukiijadili hii mada na nikakuweka kwenye CROSS EXAMINATION lazima uchochore
 
Vitabu 14 havipo kwenye Biblia ya sasa wakati ile ya Mwanzo Vilikuwepo hiyo ni moja ya sababu ya kutokuwa OG zipo na zingine kibao.
Inaonekana wewe umelishwa propaganda ila kujitetea huwezi

Hoja kwamba Biblia ya sasa si OG kwa sababu vitabu 14 havipo inachekesha,Kuna vitabu vingi ambayo ni apokrifa vipo na watu wanavisoma kama Hadith , historia tu,

Kuna sababu kwanini Jews walikusanya biblia hii agano la kale ,ndio maana nimekwambia Dead sea scrolls ya mwaka 250BC , Ina vitabu vyote vya agano la kale kwenye biblia ya Sasa kwa 99.999%

Kitabu cha Esta tu ndio hakipo

Huu ugunduzi wa Dead sea scrolls uliwafanya wenye hii propaganda yako mpaka kesho waingie mitini ,maana iliwaumbua

Manuscripts za Biblia zilizopatikana, kama Dead Sea Scrolls (karibu 250 BCE – 68 CE) na Papyrus 52 (~100–150 CE), zinathibitisha kuwa maandiko ya kale yalikuwepo mapema sana, ndani ya karne zilizotangulia Biblia ya sasa.

Hata Yesu alizinukuu hayo maandiko haya ya kale, akayahubiri na moja ya kanuni ya kuacha vitabu vya apokrifa kwanza havipo kwenye manuscript za awali, Mitume na Yesu hawakuvinukuu,

Sasa wewe unasema viliondolewa, Kuondolewa kwa baadhi ya vitabu siyo kuharibu Biblia; ni matokeo ya historia ya kuchagua vitabu vilivyoendana na mafundisho.

Manuscripts hizi nyingi za mapema zinaonyesha Biblia ya leo inalingana sana na maandiko ya asili, hivyo hoja kwamba si OG ni propaganda isiyo na msingi.

Na hivo vitabu vipo ukitaka unavipata ,
 
Msiwe mnaokoteza habari zisizo na uthibitisho. Nani alikuambia kuwa Injiliniliandikwa Kirumi na Kiebrania?

Vitabu vya agano la kale viliandikwa kwa lugha mbili. Na hiyo iliitwa Tora. Hiyo Tora iliyoandikwa kwa Kiebrania ilikuwa na vitabu 36. Tora iliyoandikwa kwa Kigiriki ilikuwa na vitabu 46. Lakini kama ya kuandikwa, Tora kwa miaka mingi iliishi kwenye kumbukumbu za watu na kusimliwa toka kizazi kimoja hadi kingine, mpaka ilipokuja elimu ya kuandika.

Agano Jipya, Waandishi wale wote wanne, ni injiliya Mathayo pekee ndiyo iliandika kwa Kiebrania, wengine wote waliandika kwa Kigiriki, na zote, zilitafsiriwa kwenda kwenye lugha zote kubwa za wakati huo, na hasa kilatini.

Maandiko ya Agano la kale, ya zamani kabisa ni ya kitabu cha Hesabu na walawi. Maandiko haya yaliyopo ni ya tangu miaka 600 kabla ya Kristo.
ambavyo bado vipo
Huyo jamaa anaookota propaganda za kina mazinge analeta hapa

Nimemwambia kama anajiweza aje hapa tumfanyie cross examination kuhusu hii mada
 
Ukisoma kwenye vitabu vya paulo (aka agano jipya) utaona wazi kuwa wanafunzi halisi wa Yesu walikuwa wakiwindwa na kuuawa. Huku kiongozi wa mauaji akiwa ni Paulo mwenyewe.

Imani halisi aliyofundisha Yesu ilikuwa ikionekana ni Haramu mbele ya Warumi na vibaraka wao wa kiyahudi.
Hivi mnaona wote humu ni wajinga ?

Paulo alikuwa muuaji mwanzoni, na baadae alibadilika na alishirikiana sana na wanafunzi WA Yesu kueneza injili

Hoja kwamba Paulo alikuwa kiongozi wa mauaji au alikuwa kinyume na wanafunzi wa Yesu ni si sahihi.

Biblia inathibitisha kwamba Paulo alikuwa mtumishi wa imani ya Yesu na aliwasaidia wanafunzi wengine kueneza Injili.

Kwa mfano, Waefeso 2:20 inasema:

20 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.

Paulo aliandika barua zake akishirikiana na Petro, Yohana, na wanafunzi wengine wa Yesu, si dhidi yao.

Aidha, Matendo 9:15-16 inafafanua kwamba Paulo aliteuliwa na Mungu kueneza injili kwa mataifa yote, si kuwaua wanafunzi wa Yesu. Wanafunzi walioshuhudia maisha ya Yesu waliendelea kushirikiana na Paulo, na hata wakubwa wa Kanisa walimkubali, ikionyesha wazi kwamba Paulo hakuwa kiongozi wa mauaji bali mtumishi wa kweli wa Injili.
 
sawa kobazi tunaomba uiweke hapa iyo injili halisi na sisi tujisomee kama ww ulivosoma ukajua kuwa ayo hayakuwemo..............tuwekee hapa hapa

afu inaonekana hujui hata maana ya injili ngoja ni kusaidie

injili n habari njema za kuzaliwa kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo.
kwa mujibu wa Quran haipo kutokana na mikono ya uongo ya waandishi wenu.

Pia soma Yeremia 8:8
 
Nakala halisi za vitabu hivi vitatu...Taurati, Zabur na Injili zipo kwa Mungu.

Ndani ya Agano la kale na hili Jipya yapo maneno ya Mungu, maneno ya waandishi, tafasiri za wanazuoni, maneno ya manabii wa uongo Paulo na genge lake n.k ndio maana unakuta contradictions nyingi, upotoshaji mkubwa n.k
 
Kitabu pekee kilichobaki katika uhalisia wake kwa miaka 1400 ni Quran tu
 
allah ni dhaifu sana anajitunzia nakala za zaburi injili na torati za nn wakat duniani hazipo original..............

alafu allah uyo uyo ameweza tunza quruan isiharibiwe
 
kwa mujibu wa Quran haipo kutokana na mikono ya uongo ya waandishi wenu.

Pia soma Yeremia 8:8
sasa hii quruan ya juz mbona inasema tukawaulize wakristo na mayahud waliopewa vtabu......??

inamaana haikujua hvo vitabu vishakuwa corrupted?

kobaz mu 1 anamfundisha aliyepewa kitabu kuwa kitabu chake ni kitabu feki

ivi ukiachana na mohamed nani mwingne alikuwa nabii wa kiarabu?
 
Kwanza ulitakiwa ujue jambo moja, ishara ya kutokuwepo kwa matini ya Injili ni kutokuwepo Injili katika lugha ya Yesu.

Injili kusemwa au ujumbe wa Yesu kusemwa umeandikwa au kutafsiriwa kwa lugha ya Kiebrania, mlitakiwa mtu ambie hao wakipata wapi hayo maandiko na walijuaje kama ni ujumbe wa Yesu.

Yawezekana hujui mambo mengi kuhusiana na historia ya dini.
Kwa uelewa wako, Yesu alikuwa anajua lugha ngapi?

Ufahamu kuwa nyakati za Kristo Bwana, katika Israel ya kale, yaani ile Israel na Judah Kingdoms, kulikuwa na lugha 4 zilizokuwa zikitumika:
1. Kigiriki, lugha rasmi ya wasomi. Yesu Kristo mara kadhaa aliingia kwenye mijadala mizito na wasomi wa nyakati hizo, kiasi cha kuwashangaza wasomi wakuu. Aliongea na wasomi kama msomi kwa lugha ya wasomi.

2. Kiebrania.
Kiebrania ilikuwa lugha ya asili ya wayahudi lakini ilipotea na kubakia lugha ya dini wakati wayahudi walipochukuliwa utumwani Babylon, na huko walikaa miaka 70. Watoto waliozaliwa utumwani Babylon waliporudi hawakuitambua lugha hii, badala yake waliongea lugha ya huko Babylon walikozaliwa, yaani lugha ya Aramaic. Lakini wataalam wote wa dini waliitumia lugha hii kwa masuala ya dini kwani maandiko yote ya dini yalikuwa katika lugha hii.

3. Aramaic
Ilikuwa lugha ya watu wa kawaida, japo haikuwa lugha yao asilia. Yesu aliongea ligha hii kwani mara nyingi aliwahubiria na kuwafundisha watu wa kawaida.

4. Kilatini
Kilatini ilikuwa lugha ya mtawala, na ilitumika na kuzungumzwa kwenye makoloni ya Mrumi, japo si wengi walipiongea, isipokuwa wale waliokuwa na maingiliano na watawala. Hakuna ushahidi wa moja kwa moja, lakini inaaminika kuwa Kristo Bwana pia aliiongea lugha hii.

Waandishi wa injili waliitumia lugha ya Kigiriki kwa sababu lugha hiyo ndiyo ionekana kuwa ni lugha rasmi na universal kwa maana ilizungumzwa katika mataifa mengi.
 
Kama siyo lugha aliyoizungumza Yesu maana yake kuwa siyo kweli?
Kwa uzito wa ujumbe wa bwana Yesu ilitakiwa uwe kama alivyousema, na mara nyingi alikuwa akizungumza kwa kutumia mifano "parables", hao wanafunzi wake walikuwa hawamfahamu vizuri sasa usiniambie ujumbe wake utafisiriwe kwenda lugha nyingine na kwa watu wengine, unafikiri utafahamika vizuri?
Na mfumo ya lugha ya kiaramia ni tofauti na lugha ya kigiriki, kwani lugha ya kiaramia ni lugha ya vitendo (picha) wakati lugha ya kigiriki ni lugha ya dhana (kifalsafa).

Ukisoma Matayo 5:17-18

​

17“Do not think that I have come to abolish the Law or the Prophets; I have not come to abolish them but to fulfill them. 18For truly, I say to you, until heaven and earth pass away, not an iota, not a dot, will pass from the Law until all is accomplished. 19Therefore whoever relaxes one of the least of these commandments and teaches others to do the same will be called least in the kingdom of heaven, but whoever does them and teaches them will be called great in the kingdom of heaven. 20For I tell you, unless your righteousness exceeds that of the scribes and Pharisees, you will never enter the kingdom of heaven.

17“Msidhani kwamba nimekuja kufuta sheria ya Musa na mafundisho ya manabii. kwamba mpaka mbingu na dunia zitakapo toweka, hakuna hata herufi moja ya sheria itakayopotea mpaka shabaha yake ikamilike. 19Kwa hiyo ye yote atakayelegeza hata mojawapo ya amri ndogo kuliko amri zote na akawafundisha wengine kufanya hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika Ufalme wa mbinguni. Sikuja kuzifuta bali kuzitimiza. 18Kwa maana ninawaambia hakika Lakini atakayetii amri hizi na kuwafundisha wengine kuzitii ataitwa mkuu katika Ufalme wa mbinguni. 20Kwa maana nawaambieni, ikiwa haki yenu haitazidi haki ya waandishi wa sheria na Mafari sayo, hamtaingia katika Ufalme wa mbinguni kamwe.”

Hivyo kwenye maneno ya Mungu hutakiwi kuongeza wala kupunguza hata herufi moja, sembuse kubadilisha maana kabisa.
 
Kitabu pekee kilichobaki katika uhalisia wake kwa miaka 1400 ni Quran tu
Unajua kuwa Quran Haina hata manuscript moja tu ya karne ya 7 au 8

ili Hali biblia Ina Manuscript za kabla ya Yesu

Inakuwaje Quran ya juzi tu hapa INAKOSA angalau manuscript za Uthman

Wakati vitabu vya Aristotle vina manuscript
 
kwa mujibu wa Quran haipo kutokana na mikono ya uongo ya waandishi wenu.

Pia soma Yeremia 8:8
Kwanini Quran inasema mkaulize kwa waliopewa kitabu?

Je haikujua kuwa vimeharibiwa?

Halafu hiyo Yeremia 8:8 context yake sio hiyo unayosema

Kingine unawezaje kutoa ushahidi Kwenye kitabu unachodai kimeharibiwa ?
 
Nakala halisi za vitabu hivi vitatu...Taurati, Zabur na Injili zipo kwa Mungu.

Ndani ya Agano la kale na hili Jipya yapo maneno ya Mungu, maneno ya waandishi, tafasiri za wanazuoni, maneno ya manabii wa uongo Paulo na genge lake n.k ndio maana unakuta contradictions nyingi, upotoshaji mkubwa n.k
Mungu alivichukua lini na mwaka gani ?
 
Kwa uzito wa ujumbe wa bwana Yesu ilitakiwa uwe kama alivyousema, na mara nyingi alikuwa akizungumza kwa kutumia mifano "parables", hao wanafunzi wake walikuwa hawamfahamu vizuri sasa usiniambie ujumbe wake utafisiriwe kwenda lugha nyingine na kwa watu wengine, unafikiri utafahamika vizuri?
Na mfumo ya lugha ya kiaramia ni tofauti na lugha ya kigiriki, kwani lugha ya kiaramia ni lugha ya vitendo (picha) wakati lugha ya kigiriki ni lugha ya dhana (kifalsafa).

Ukisoma Matayo 5:17-18

​

17“Do not think that I have come to abolish the Law or the Prophets; I have not come to abolish them but to fulfill them. 18For truly, I say to you, until heaven and earth pass away, not an iota, not a dot, will pass from the Law until all is accomplished. 19Therefore whoever relaxes one of the least of these commandments and teaches others to do the same will be called least in the kingdom of heaven, but whoever does them and teaches them will be called great in the kingdom of heaven. 20For I tell you, unless your righteousness exceeds that of the scribes and Pharisees, you will never enter the kingdom of heaven.

17“Msidhani kwamba nimekuja kufuta sheria ya Musa na mafundisho ya manabii. kwamba mpaka mbingu na dunia zitakapo toweka, hakuna hata herufi moja ya sheria itakayopotea mpaka shabaha yake ikamilike. 19Kwa hiyo ye yote atakayelegeza hata mojawapo ya amri ndogo kuliko amri zote na akawafundisha wengine kufanya hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika Ufalme wa mbinguni. Sikuja kuzifuta bali kuzitimiza. 18Kwa maana ninawaambia hakika Lakini atakayetii amri hizi na kuwafundisha wengine kuzitii ataitwa mkuu katika Ufalme wa mbinguni. 20Kwa maana nawaambieni, ikiwa haki yenu haitazidi haki ya waandishi wa sheria na Mafari sayo, hamtaingia katika Ufalme wa mbinguni kamwe.”

Hivyo kwenye maneno ya Mungu hutakiwi kuongeza wala kupunguza hata herufi moja, sembuse kubadilisha maana kabisa.
Kwahiyo injili original ipo wapi?
 
Back
Top Bottom