Nani amewahi kuziona Torati na Injili halisi?

Nani amewahi kuziona Torati na Injili halisi?

Una uelewa wowote kuhusu Hypocrypha/pseudepigrapha books?
Umewahi kuiona Biblia ya Kiorthodox?
Unajuwa tofauti ya (Canon) ya Biblia ya Kikatoliki na Kiprotestant?
Badala ya kuuliza maswali ulipashwa kutoa somo ili wana JF wajifunze kutoka kwako acha kufikiria kutoa maswali tu kama Mwalimu au Prof.
 
Copy halisi?.

Ina maana OG ilikuwa duplicate.
Na duplicate ilibaki?.
Je Ndio hizi tunazoziona? au walianza tena kutafuta wale waandish wa vitabu wasimulie tena upya na watu waandike?.

Je OG ilikuwa na nn cha ziada ambacho za sasa hivi hamna?.
Kwanza ulitakiwa ujue jambo moja, ishara ya kutokuwepo kwa matini ya Injili ni kutokuwepo Injili katika lugha ya Yesu.

Injili kusemwa au ujumbe wa Yesu kusemwa umeandikwa au kutafsiriwa kwa lugha ya Kiebrania, mlitakiwa mtu ambie hao wakipata wapi hayo maandiko na walijuaje kama ni ujumbe wa Yesu.
 
Badala ya kuuliza maswali ulipashwa kutoa somo ili wana JF wajifunze kutoka kwako acha kufikiria kutoa maswali tu kama Mwalimu au Prof.
Umekuja na ujuwaji hukuja kujifunza, sasa lazima kwanza nione bible knoledge yako ni level ipi.

Msingi wa Biblia ni Canon, vitabu ambavyo havikuingizwa vipo lakini siyo canon books ni Aphocrypha books, ni mafunzo na reference, havipo katika msingi wa imani ya Kikriso.

Kanisa inavitambuwa vitabu hivyo., huoni copy zake mitaani kwa sababu si vitabu vya kiimani kwa mujibu wa Church Fathers.
 
Vitabu 14 havipo kwenye Biblia ya sasa wakati ile ya Mwanzo Vilikuwepo hiyo ni moja ya sababu ya kutokuwa OG zipo na zingine kibao.
Hapa hatuzungumzii Biblia bali Torati na Injili. Au mada hujaielewa?
 
Neno Injili ni neno lenye asili ya kiarabu ambalo shina lake linatokana na neno "euangelion" lenye asili ya kigiriki lenye kumaanisha "habari njema" ambalo liliingizwa kwenye lugha ya Kiarabu toka kwa wakristo wa Syria.

Na Torati ni neno linalotokana na neno la Kiyahudi "Torah" ambalo linahusisha vitabu vitano vya Sheria vya mussa vilivyoandikwa kwa lugha ya Kiebrania.

Lakini kumekuwa na shutuma kwamba Torati na Injili zilizopo Sasa zimechakachuliwa na siyo zile halisi za zama hizo.

Jee ni nani amewahi kuziona Torati na Injili halisi ili tufanye ulinganisho tujue hizi Torati na Injili zilizopo sasa zilipunguzwa ama kuongezwa nini?
Tuanze na kulinganisha Lugha aliyozungumza Yesu na Injili ya mwanzo iliyoandikwa kwa kigiriki zinafanana?
 
Mkuu na Genesis?

Hapo nilimaanisha vitabu ambavyo kuna maandiko ya kale kabisa. Kitabu cha mwanzo, Genesis ni cha mwanzo kama kinavyojieleza, lakini katika zile manuscripts za zamani kabisa miongoni mwa zile zilizohifadhiwa, za zamani kabisa ni Kitabu cha Hesabu na Walawi. Manuscripts ya zamani kabisa za Genesis zilizohifadhiwa ni za mwanzoni mwa karne ya 2 Baada ya Kristo.
 
Nikafikiri unaweza kutembea kilomita 85 ndani ya library,kumbe ni urefu wa shelf zilizopangwa kama ukijulimsha kwa pamoja.
Yes, huo ni jumla ya urefu wa shelves zote zilizopo kwenye vyumba na majengo mbalimbali humo Vatican
Vatican City yenyewe kwa ujumla wake ni 440000 square metres, ekari 120
Kwa Dar ni eneo kama Tanganyika Packer pale kwa Mwamposa, kama urefu wa Clock tower mpaka Askari Monument ushuke mpka posta mpya urudi tena usawa wa mnazi mmoja na humo kuna Kanisa, uwanja wa St Peter, museum na sehemu za makazi za kuishi Papa na raia wake
Kaeneo kadogo sana kuwa na urefu wa 83km za library
 
Asante hapo nimeelewa, hata hivyo hio library kubwa sana, hivi Israel wao kama kitovu cha ukristo hawana library za mambo ya Kibiblia au ndio document zote zilikobwa na Warumi?
 
Neno Injili ni neno lenye asili ya kiarabu ambalo shina lake linatokana na neno "euangelion" lenye asili ya kigiriki lenye kumaanisha "habari njema" ambalo liliingizwa kwenye lugha ya Kiarabu toka kwa wakristo wa Syria.

Na Torati ni neno linalotokana na neno la Kiyahudi "Torah" ambalo linahusisha vitabu vitano vya Sheria vya mussa vilivyoandikwa kwa lugha ya Kiebrania.

Lakini kumekuwa na shutuma kwamba Torati na Injili zilizopo Sasa zimechakachuliwa na siyo zile halisi za zama hizo.

Jee ni nani amewahi kuziona Torati na Injili halisi ili tufanye ulinganisho tujue hizi Torati na Injili zilizopo sasa zilipunguzwa ama kuongezwa nini?
wewe akili huna...yaani injili wateremshiwe wana wa Israel halafu uje kusema neno hilo limetokana na lugha ya kigiriki!!!
 
Kuna scipts za bible .
Zilipatikana karibu na mapango .
na bahar ya chumvi.
dead sea scrolls .
Ni mabaki ya Biblia kwa Lugha ya kiebrania na kiajemi.

Na wanasayansi walibaini kuwa ni maandish ya kale sana yapata miaka 2000 iliyopita.

Na yale maandishi hayakuwa na utofaut sana na maandishi ya sasahivi.

Ndio utuambie sasa kama injili na torat imebadilishwa. Nn kilikuwepo na nini hakikuwepo.

Ule ni Ushahidi wa Kisayansi tena sio wa wakristo. Na umethibitisha hakukuwa na mabadiliko makubwa zaid ya kutafsiri kwenda Lugha nyingne.
IMANI YA UTATU MTAKATIFU HAIKUWEPO KWENYE INJILI HALISI.

KUFA NA KUFUFUKA KWA YESU HAKUKUWEPO KWENYE INJILI HALISI.

UOKOVU KWA DAMU YA YESU HAKUKUWEPO KWENYE INJILI HALISI.

UTABIRI WA UJIO WA MTUME MUHAMMAD BAADA YA KUONDOKA KWA YESU ULIKUWEMO KWENYE INJILI ILA BAADAE WAANDISHI WALIFICHA/ WALIPINDUA MANENO YALIYOHUSU UJIO WA MTUME MUHAMMAD (pbuh).
 
acha uongo unakanusha hii iliyopo sio original kwasababu inakupinga au??....................yan waarabu wa misri wawe na torati original ichomwe moto ipotee yote afu wayahud na wakristo wasiwe nazo orginal?

unaikataa ii iliyopo kwa kusema nifake na unadaì kuna original na hujawah ioma wala kuisoma na wala hauna et unasema imechomwa moto

na aliyskwambia imwzcjomwa moto naez hajui vilivyoandikwa ndani....kobazi bhn
Ukisoma kwenye vitabu vya paulo (aka agano jipya) utaona wazi kuwa wanafunzi halisi wa Yesu walikuwa wakiwindwa na kuuawa. Huku kiongozi wa mauaji akiwa ni Paulo mwenyewe.

Imani halisi aliyofundisha Yesu ilikuwa ikionekana ni Haramu mbele ya Warumi na vibaraka wao wa kiyahudi.
 
Neno Injili ni neno lenye asili ya kiarabu ambalo shina lake linatokana na neno "euangelion" lenye asili ya kigiriki lenye kumaanisha "habari njema" ambalo liliingizwa kwenye lugha ya Kiarabu toka kwa wakristo wa Syria.

Na Torati ni neno linalotokana na neno la Kiyahudi "Torah" ambalo linahusisha vitabu vitano vya Sheria vya mussa vilivyoandikwa kwa lugha ya Kiebrania.

Lakini kumekuwa na shutuma kwamba Torati na Injili zilizopo Sasa zimechakachuliwa na siyo zile halisi za zama hizo.

Jee ni nani amewahi kuziona Torati na Injili halisi ili tufanye ulinganisho tujue hizi Torati na Injili zilizopo sasa zilipunguzwa ama kuongezwa nini?
DR Mambo Jambo hakosi cha kusema.

Walichochakachua ni nini?...kwamba wameongeza mambo yao Ili kupindisha ukweli au ?..
 
IMANI YA UTATU MTAKATIFU HAIKUWEPO KWENYE INJILI HALISI.

KUFA NA KUFUFUKA KWA YESU HAKUKUWEPO KWENYE INJILI HALISI.

UOKOVU KWA DAMU YA YESU HAKUKUWEPO KWENYE INJILI HALISI.

UTABIRI WA UJIO WA MTUME MUHAMMAD BAADA YA KUONDOKA KWA YESU ULIKUWEMO KWENYE INJILI ILA BAADAE WAANDISHI WALIFICHA/ WALIPINDUA MANENO YALIYOHUSU UJIO WA MTUME MUHAMMAD (pbuh).
sawa kobazi tunaomba uiweke hapa iyo injili halisi na sisi tujisomee kama ww ulivosoma ukajua kuwa ayo hayakuwemo..............tuwekee hapa hapa

afu inaonekana hujui hata maana ya injili ngoja ni kusaidie

injili n habari njema za kuzaliwa kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo.
 
Zilichomwa moto kwenye maktaba ya Alexandria, Misri. Hivyo copy halisi huwezi kuziona

Baada ya hapo ndio wakaanza kubadirisha mambo kidogo kidogo. Angalia hizi Sanamu zinazosemwa za Yesu ambazo waumini wakikristu wanauziwa na kuaminishwa ni za Yesu wakati ni za Mwigizaji zilizotengenezwa miaka ya 1970 tu hapo. Cha ajabu waumini hawaambiwi kuwa ni za Mwigizaji na wanauziwa kwa pesa kubwa ni sawa tu na kuuziwa Maji na Mafuta kwa Mchungaji Mwamposa. 🤣
MNAPENDA sana propaganda

Dead sea scrolls zipo hata kabla ya Yesu na hiyo makataba ya Alexandria

Zinahifadhiwa Qumran Israel

Zinafanana kwa 99.9999% na biblia hii agano la kale ,kitabu ambacho hakipo ni cha Esta tu

Waislamu mtaacha lini uongo, uzushi KWNEYE zama hizi za teknolojia ,hamuoni aibu ?
 
Kwenye Bible ya sasa kuna vitabu 14 viliondolewa ambavyo vilikuwa kwenye Bible ya kwanza ambqyo ndio tunasema ni OG. Hicho ni kimojawapo cha kusema hii ya sasa siyo OG.
Viliondolewa na nani ?

Hakuna kitabu kiliondolewa ,hivo vitabu vya apokrifa vipo na vinavyosomwa kama Hadith tu au historia

Acheni cheap propaganda
 
Kwenye Bible ya sasa kuna vitabu 14 viliondolewa ambavyo vilikuwa kwenye Bible ya kwanza ambqyo ndio tunasema ni OG. Hicho ni kimojawapo cha kusema hii ya sasa siyo OG.
Maandiko ya Biblia yamehifadhiwa kwa vizazi vingi, na ushahidi wa kihistoria unaonyesha maandiko haya yalikuwepo mapema kabla ya Yesu Kristo.

Kwa mfano, Dead Sea Scrolls yaliyopatikana karne nyingi zilizopita yanathibitisha maandiko ya Agano la Kale kama yalivyoandikwa, huku baadhi yake ikiwa karibu mamia ya miaka kabla ya Yesu.

Aidha, Papyrus 52, ambalo ni kipande kidogo cha Injili ya Yohana, kinathibitisha kwamba maandiko ya Agano Jipya yalikuwa yameandikwa tayari karne ya kwanza, ndani ya maisha au mara baada ya maisha ya Yesu.

Hii inathibitisha kwamba maandiko ya Biblia ya leo yanatokana na maandiko halisi ya kale. Zaidi, Yesu Kristo mwenyewe alitabiri na kunukuu maandiko haya ya Agano la Kale, akithibitisha umuhimu na uhalisi wake.

Kwa hivyo, kuondolewa kwa baadhi ya vitabu hakuharibu Biblia, kwani maandiko yaliyohifadhiwa ni sahihi, yaliyoandikwa mapema, na yamepitishwa kihistoria na kithibitisho cha wazi
 
Nami niketi hapa kukiona hicho kitabu
 
Fanya research mkuu.
Shida waislamu wengi hamtumii akili ,hamfatilii mambo ,mnadanganywa na nyie mnabeba hizo propaganda bila kufanya research

Hoja kwamba Biblia imeharibika au imebadilishwa haiwezi kuthibitishwa kwa ushahidi wa kihistoria.

Kuna mamia ya manuscripts za Biblia yaliyoandikwa mapema sana, kama Dead Sea Scrolls yaliyochimbwa Karne ya 20, ambayo yanathibitisha maandiko ya Agano la Kale yaliyoandikwa karibu mamia ya miaka kabla ya Yesu.

Sasa anapokuja mtu anasema biblia iliharibiwa wenye akili wanamuona ni mpumbavu tu .

Aidha, kipande kidogo cha Papyrus 52, kilichopatikana karne ya kwanza, ni uthibitisho kwamba maandiko ya Agano Jipya yalikuwa yameandikwa ndani ya maisha ya au karibu na maisha ya Yesu.

Ushahidi huu unaonyesha kuwa maandiko ya Biblia ya leo yameakisi maandiko ya kale kwa usahihi mkubwa.

Biblia imehifadhiwa kwa makini na waandishi na makanisa wa kihistoria, hivyo kubadilishwa kwa maana ya kupoteza maana au maandiko sahihi ni ngumu sana.

Hata wale wanaosema Biblia imebadilishwa wanapotafiti kwa kina wanajikuta kuwa hawawezi kutoa ushahidi wa kweli, na propaganda hiyo haina msingi wa kihistoria au kisayansi.

Hata wewe hapa nikikuweka kikaangano na uhakika lazima utokomee kusikojulikana ,

Biblia ya leo ni matokeo ya maandiko ya kale yaliyohifadhiwa kwa makini na kuthibitishwa na manuscripts nyingi za kihistoria.
 
Back
Top Bottom