john achila mukumwa
Senior Member
- Jan 4, 2024
- 139
- 275
Wana wa manabii ni akina nani
Katika biblia tunasoma sehemu kadha wa kadha zikiwataja “wana wa manabii”.
Katika Agano la Kale, lilikuwepo kundi la watu waliojulikana kama Wana wa Manabii (1Wafalme 20:35, 2Wafalme 2:5, 2Wafalme 4:1, 2Wafalme 6:1).
Watu hawa walikuwa ni manabii wa Mungu, ambao walijitia katika kifungo cha kujifunza juu ya Nabii zilizotangulia kabla yao.
Hii haikuwa kujifunza jinsi manabii wanavyoishi, au wanavyokula, au wanavyoona maono. La hasha. Hakuna mwanadamu yeyote anayeweza kumfundisha mtu mwingine namna ya kuona maono. Hivyo ni vipawa vya Mungu ambavyo ni Mungu mwenyewe anaviweka ndani ya mtu, na hatujifunzi wala hatufundishwi.
Ni sawa na ndoto. Hakuna mtu anayeweza kumfundisha mwenzake jinsi ya kuota. Ndoto zinakuja zenyewe, kwa sababu ni vipawa vya asili ambavyo Mungu kaviweka kwetu wote.
Na nabii za Mungu, zinawajia watu maalum, ambao Bwana amewachagua, na siyo kupitia kujifunza.
Kwa hiyo hawa "wana wa manabii", au kwa lugha nyingine “wanafunzi wa manabii”, walikuwa ni watu waliojikita katika kujifunza nyakati na majira, pamoja na Nabii zilizotangulia kutolewa na manabii wengine waliowatangulia. Kumbuka kuwa walikuwa wanajulikana kama wana wa MANABII, na siyo wana wa NABII.
Lengo la kufanya hivyo, yaani kupokea maarifa hayo, ni ili wawe salama, na wawe na uhakika wa Nabii watakazozitoa isije wakapotoka na kutoa unabii wa uongo.
Kwa mfano, Nabii anaweza kuona maono au kupata ujumbe kuhusu Taifa la Israeli. ili authibitishe ujumbe ule au ono lile kama kweli ni kutoka kwa Bwana, ni sharti awe na Nabii nyingine za kutosha, za waliomtangulia, zinazoendana na ono lake hilo jipya. Na akija kugundua kuwa Nabii mwingine mkuu aliyetangulia, alishatabiri jambo kama hilo au linalokaribiana na hilo, ndipo ono lake hilo linathibitika.
Lakini akija kukuta ono lake linakinzana na maono ambayo manabii wakuu waliyatoa, ndipo analiacha, kwa sababu siyo kutoka kwa Bwana. Ni kwa sababu kamwe Bwana hawezi kujipinga katika maneno yake.
Hiyo ndiyo maana ilihitajika SHULE YA MANABII, ambayo lengo lake ni kujifunza kujua Nabii zilizotangulia juu ya watu, na mataifa.
Katika kuelewa vizuri kuhusu suala hili, utakumbuka kipindi cha Nabii Yeremia wakati anatabiri kwamba Israeli watachukuliwa utumwani kwenda Babeli. Yeremia alikuwa ni mtu mwenye elimu ya kutosha kuhusu nabii zilizotangulia, na alihakiki jumbe anazozipokea katika maono, kwa nabii za waliomtangulia kama wakina Isaya, na wengineo.
Jambo moja alilojifunza ni kuwa “Manabii karibu wote, hawakuwahi kutabiri juu ya Amani kwa mataifa, bali manabii wengi walikuwa wanatabiri juu ya Vita na Mabaya na Tauni”. Na Yeremia alijua Mungu hawezi kujipinga. Hivyo maono yake aliyahakiki kwa namna hiyo.
Lakini utaona alitokea mtu anaitwa Hanania, ambaye alijitokeza na kuanza kutabiri juu ya Amani kwa Israeli, kwamba hawataenda utumwani, watakuwa salama, ilihali taifa zima limemwacha Mungu, jambo ambalo lilikinzana na nabii Mungu alizozitoa kupitia manabii wakuu waliotangulia. Na Yeremia kuliona hilo akamwambia Hanania maneno yafuatayo:
Yeremia 28:7 “Lakini lisikilize sasa neno hili nilisemalo, masikioni mwako, na masikioni mwa watu wote, 8 MANABII WALIOKUWAKO KABLA YA ZAMANI ZANGU, NA ZAMANI ZAKO, WALITABIRI JUU YA NCHI NYINGI, NA JUU YA FALME KUBWA, HABARI YA VITA, NA YA MABAYA, NA YA TAUNI”.
Umeona jambo Yeremia alilomwambia Hanania?
Yeremia alikuwa ni mwana wa manabii, lakini Hanania alikuwa ni mtu tu aliyejizukia na kujiita Nabii. Hakuwa na elimu yoyote ya Nabii za Mungu. Akaanza kuwafariji watu kwa maneno ya uongo, jambo ambalo lilimchukiza sana Mungu, na hata kumwua Hanania.
Hebu tusome zaidi kuhusu Yeremia 28:
15 “Kisha nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, Sikia sasa, Ee Hanania; Bwana hakukutuma; lakini unawatumainisha watu hawa maneno ya uongo.
16 BASI BWANA ASEMA HIVI, TAZAMA, NAKUTUMA UENDE ZAKO TOKA JUU YA USO WA NCHI; MWAKA HUU UTAKUFA, KWA SABABU UMENENA MANENO YA UASI JUU YA BWANA. 17 BASI NABII HANANIA AKAFA, MWAKA UO HUO, MWEZI WA SABA”.
Leo hii shetani ameligeuza hili Neno Wana wa Manabii. Leo hii kuna watu wamefungua vyuo vyao, wakiwa wenyewe wanajiita Manabii wakuu, na vijana wao wanawaita “wana wao (yaani wana wa manabii)”. Lakini ukiingia katika madarasa yao na kusikia wanachofundishwa, ni huzuni tupu.
Utasikia wanachofundishwa ni jinsi ya kuona maono, jinsi ya kutumia na kutengeneza mafuta na chumvi, na mengineyo. Utaona wanafundishwa mtindo wa maisha na mtindo wa kuongea, na kuvaa kama nabii mkuu wao, na jinsi ya kumwogopa na kumtukuza baba yao, nabii mkuu. Na watasomea hata miaka 5 na wakitoka hapo wanapewa na vyeti, tayari wakufunzi. Huo ni uongo wa shetani.
Wana wa manabii katika Agano la kale, hawakufundishwa wala hawakuwa wanajifunza mitindo ya kuongea ya manabii waliowatangulia. Wala walikuwa hawajifunzi jinsi ya kuona maono, kwa sababu tayari walikuwa na hiyo karama, ndiyo maana wakaitwa manabii.
Walichokuwa wanajifunza ni nabii zilizotangulia zinazohusu wakati waliopo wao, na za mataifa mengine, kuanzia zilizoandikwa katika Torati ya Nabii Musa, mpaka wakati waliopo wao, ili kusudi wasije wakapotoka na maono waliyokuwa wanayapokea.
Na sisi leo hii, wote ni Wana wa Manabii, ambao manabii wetu si baba zetu wa kiroho. Wala si maaskofu wetu, bali ni MITUME WA KWENYE BIBLIA, na MANABII WA KWENYE BIBLIA.
Tunatembea katika nabii walizozitoa hao, wakina Musa, Isaya, Yeremia, Habakuki, na mitume wakina Petro, Yohana, Paulo nk. Na nabii zao hazijawahi kukinzana. Kwa sababu walikuwa na Roho mmoja.
Kwa mfano, Nabii Isaya alitoa unabii ufuatao, Isaya 13:6 “Pigeni kelele za hofu; maana siku ya Bwana i karibu; itanyesha kama maangamizi yatokayo kwa Mwenyezi Mungu”.
Nabii Yoeli naye alitoa unabii kama huo huo katika Yoeli 3:1. Na manabii wengine wote walitabiri hayo hayo.
Kwa leo, ili sisi tuhesabike kuwa “Wana wa Manabii", ni lazima maono yetu tunayoyaona katika ndoto, au kwa wazi, yapatane na huo unabii wa Isaya, na Yoeli na wengineo katika biblia. Usipopatana na huo unabii wa Isaya, basi hilo ono au huo unabii ni wa UONGO. Ni kutoka Kuzimu.
Tukiota au tukiona maono ambayo yanatuonyesha au kutuambia kuwa “Tufurahi, tupige kelele za shangwe, kwa sababu siku ya Bwana bado sana”, basi hilo ni ono kutoka kuzimu.
Kwa hitimisho ni kwamba, wana wa manabii, ni manabii ambao walikuwa wamejikita katika kusoma nabii za manabii wa Mungu waliowatangulia, ili wasifanye makosa katika kutoa nabii zao.
Hawakuwa watoto wa manabii, bali walikuwa ni manabii kamili wa Mungu, ambao walijitia katika kifungo cha kujifunza juu ya nabii zilizotangulia kabla yao.
Na sisi pia tukiwa wana wa manabii, ni lazima tuwe wanafunzi wa biblia, turejee biblia katika kuhakiki kila kitu, na hatupaswi kuamini tu kila jambo ambalo tunalipokea katika ndoto au maono.