Kudai uthibitisho wa kitu ni kudai definition ya hicho kitu?!!
Ina maana mwenye kutaka uthibitisho wa kitu ni kwamba hakijui hicho kitu ni nini?
1. Inawezekana hakijui, na hapo definition ni sehemu ya uthibitisho, maana unaweza kuanza kuelezea kitu bila kuki define ikawa huja make sense.
2. Inawezekana anakijua, lakini anavyokijua yeye na unavyokijua wewe ni tofauti. Na hapo ni muhimu definition iwekwe vizuri ili kuondoa mapishano. Mfano, kama wote mnajua rangi nyekundu na blu ni ipi, lakini unayoita wewe nyekundu, mwenzako anaita bluu, na unayoita wewe bluu, mwenzako anaita nyekundu, mnaweza kuwa mnataja kitu kile kile, lakini kwa majina tofauti, au mnaweza kuwa mnataja vitu tofauti, kwa jina lile lile.
Hapo definition ni muhimu.
Chukulia mfano, mnafanya litmus paper test kuangalia acidity na alkalinity. Halafu wewe unachoita nyekundu, mimi naita bluu, na mimi ninachoita bluu, wewe unaita nyekundu.
Hapo tutabishana hata kama tunaona rangi ile ile. Wewe utaiita nyekundu, mimi nitaiita bluu.
Kwa nini? Kwa sababu hatuja define na kukubaliana nyekundu ni nini na bluu ni nini.
define Mungu ni nini, kisha, thibitisha Mungu yupo.
Unaweza kum define Mungu wako ni ng'ombe kama wahindi, au ni gravity.
Ukimdefine Mungu wako hivyo, siwezi kukubishia kwamba yupo, katika muktadha huo.
Kwa sababu ng'ombe yupo, na gravity ipo.
Ili mjadala uwe na maana, inabidi u define Mungu ni nini kwanza. Halafu uthibitishe yupo.
Bila hayo, utakuwa unaendekeza ubishi usio msingi.