Nani aliyemshauri Rais Magufuli amjibu Lowassa?

Nani aliyemshauri Rais Magufuli amjibu Lowassa?

mtu anakwambia usiongee hovyo alafu yeye anaongea hovyo kwa kuropoka eti usiangalie sura! Kwahiyo hata awe na "kichwa rungu" akamatwe tuu?
 
Siku zoote hizo alikuwa hafahamu kuhusu kuwekwa ndani hao anowatetea, juzi alipotamka ndo alifahamu au..kwa nini aseme wakati huu??? halafu yeye akisema sawa mnaziba midomo yenu, akisema Rais mnafunua mabakuli yenu..kwa hiyo hata ukisemwa uongo na Lowasa Rais anyamaze tu ndio hivyo..hata mtoto wa darasa la saba hahitaji kufundishwa kwamba Rais anapata taarifa za kina juu ya matukio yote yanayotokea nchini kwake kuliko wewe unayetegemea media! bara kukaa kimya kuliko kuleta ujinga huu ulioandika..
Ni kitu gani au sentensi gani mbaya mno inayovunja sheria ambayo aliitumia Lowasa alipofuturisha?
 
IPO siku mtamwelewa tu Raisi, kama ilivyochuwa muda kumwelewa kwenye makinikia, Leo hii hamna tena cha kuongea na ndiyo maana wanasiasa waliofilisika kisiasa wanaungaunga maneno ili wawagombanishe Watanzania. Ila watashindwa tu tena muda sio mrefu.
Wewe kwenye makinikia umemwelewa?
 
Lowassa angekuwa kipindi cha nyerere angekuwa ndani saa hizi, kuna statement kwa level ya lowasa hakutakiwa kuongea yale

wanaokufa ni ccm tu??

lowassa hana sapoti yeyote, unless unasema hao wauaji ndio wako nyuma ya lowassa??!!!

nyuma ya lowassa?? unamtisha nani??
Si mtekeni basi kama mnavyowateka wengine ! Hamna ushahidi mnaweka watu ndani mithili ya magunia ya mahindi .

Mmejaa uoga halafu mnajifanya mnapiga mkwara ! Poor ccm !
 
Awajumlishe kabisa Change na mtuhumiwa wa Richmond
Mkuu Change au Ngoyai sio wepesi hivyo wengi tunawachukulia...hawa niwajanja wemetembea nchi nyingi sana dili zinafanywa streets Kali abroad wanazijua....nivugumu kuwafunga watu hawa....sasa shida mkulu hajatembea amejaa hasira tu....thats why JK remains smart quite but sure!
 
Rais hajawai kua na akiba ya maneno jaribuni kumzoea ndivyo alivyo Serikali yangu hakutakua na Mpinzani sahau kesho kutwa akamteua mpinzani Sometime yes sometime No kwa hiyo nilishamzoea
 
Pole pole ndyo mshauri wake
Hahahahh ccm kuna makinikia ya uropokaji, akili kidogo nguvu nyingi, maadam ujue kusoma na kuandika, hata kama unaziro unasomeka kinara[emoji2] [emoji1] [emoji1]
 
Huyu jamaa alibidi awe katibu mwenezi wa chama chake maana achagui cha kusema
 
Hapo hata mimi Rais wangu mpendwa sijamuelewa.
Kuhusisha wale jamaa wa Zanzibar na kinachoendelea Kibiti ni makosa makubwa au hakupaswa kuyasema hadharani.

Hii maana yake Rais anatangaza kua kinachofanyika Kibiti ni ugaidi, maana yake ni kua sasa magaidi wote wataanza kumiminika Kibiti maana serikali ishasema kuna ugaidi.

Haikua sawa kabisa kusema yale hadharani kwa mtazamo wangu.
Kuna taarifa nimezipata, ambazo zimeongelewa na mtu mmoja mzito huko zanzibar, kuwa maalim seif na dk shein, wapo kwenye mazungumzo na kwamba dr shein atamkabidhi nchi maalim seif katika kipindi kisichozidi miezi 3 ijayo
Ving'ang'anizi waachie madaraka? Unafikiri hii nyimbo mpya imetungwa kwa bahati nasibu/mbaya? Link Nani aliemshauri rais Magufuli amjibu Lowassa?

Link2. Rais Magufuli atinga bandarini, ashangaa vichwa vya treni kushushwa na kukosa mwenyewe

NUKUU-"Niwaombe wanasiasa wanaoshindwa kucontroll midomo ya, wanaosema kuwa hawa watu wameshikwa kwa muda mrefu, tunashindwa kujua hata kuna watu kule Marekani walikaa Guantanamo muda nrefu, katika hali hiyk kwanini usifanye watu wafikiri na wewe ni mmoja wao. Msitufanye tukafika huko," Rais John Magufuli.

"Kwanini hata siku moja mtu asijitokeze kuulani watu wanaouawa bila hatia kule. Lakini kwa kuta sifa za kisiasa, mtu anatoka anasema hawa watu wako ndani muda mrefu, kuna ndugu zetu wanakufa kule...nataka polisi mfanye kazi yenu, hawa wanaoropoka waisaidie polisi, msiogope sura, awe na mwendo wa haraka, polepole au kukimbia, mkamateni ili kusudi aisaidie polisi akiwa kule ndani," Rais John Magufuli

"Juzi mtu amekamatwa na uniform 5000 za jeshi na inaonekana anahusika na hao walioko ndani, halafu unasema wamekaa muda mrefu, au na wewe ni miongoni mwa waliogiza hizo uniform za jeshi," Rais John Magufuli.

Link3. Lowassa ataka masheikh wa uamsho wafikiriwe..Adai ni fedhea kuwashikilia mahakamani kwa miaka minne - Mtembezi

 
Lowassa angekuwa kipindi cha nyerere angekuwa ndani saa hizi, kuna statement kwa level ya lowasa hakutakiwa kuongea yale

wanaokufa ni ccm tu??

lowassa hana sapoti yeyote, unless unasema hao wauaji ndio wako nyuma ya lowassa??!!!

nyuma ya lowassa?? unamtisha nani??


Wewe hujatafakari kwa undani, kauli ile siyo nzuri maana imehusisha imani ya dini ya kiislamu na mauji yanayofanyika Kibiti.
Kama mashehe wanauhusiano na wauaji kwanini wasipandishe mahakamani?
 
Kwani mamvi ni Rais...?kuna tofauti kubwa kati Sizonje na EL anachoongea Sizonje kina mapokeo mapana kuliko EL,tukiona muendelezo wa uropokaji wa Sizonje kwa nafasi yake tunashangaa ila sio tatizo kauli hizo zingekua zinatolewa na mzee Rungwe kweli kipaumbele kinatakiwa kibaki kua elimu maana hata wafuasi wake hamjui nafasi ya Sizonje.
Kulikuwa na haja ya kunishambulia mimi binafsi kwa mtazamo wangu? Mbona sijasema wote mnaomsapot mamvi akili zenu mbovu? Sababu I am smart how to deal with people. Tuongelee hao watu wawili (Mamvi na Magu). Habari ya mimi au wewe upoje ni mjinga tu au mtu asiyeelewa anaweza akafanya ni ishu. Ni mtazamo wangu una mtazamo wako. Jifunze jinsi ya kujadiliana ni skill nzuri hata kwenye maisha yako binafsi
 
Wachangia mada wengi humu wameshindwa kumuelewa mh. Rais kutokana na upeo wao mdogo au wapo kwa lengo la kumchafua rais.
Sijaona sehemu yoyote aliyohusisha viongozi wa uhamsho waliofungwa na wauaji wa kibiti..ukisikiliza kwa makini anayosema mh. Rais na ukaelewa maana yake hautokaa na kupiga porojo humu zisizo na msingi kwa lengo la kumchafua. Rais hakuna alipokosea, tutumie bongo zetu kutafsiri kwa umakini.
 
Kwenye red: Jitahidi siku nyingine usiandike jambo usilolifahamu kwa undani wake. Nani amekuwambia mashehe walio ndani hawana uhusiano na mauaji yanayoendelea? Furahia amani uliyonayo nyumbani kwake lakini kaa ukijua Rais anafanya kazi ambayo huna taarifa nazo ili uendelee kuishi kwa amani na kuandika hapa JF. Panua mawazo yako na fikiri kwa utashi zaidi. Rais hakukurupuka kusema aliyosema jana, na kinachoshangaza na pengine kusumbua akili ni wanasiasa kutetea upande unaoleta shida. Na wewe unaweza kuchagua upande.
Acha hizo Rais mara nyingi wasaidizi wake humdanganya sana mbona vyeti vya Bashite kaviamini hadi leo?
 
mtu anakwambia usiongee hovyo alafu yeye anaongea hovyo kwa kuropoka eti usiangalie sura! Kwahiyo hata awe na "kichwa rungu" akamatwe tuu?
Huo ndiyo Udikteta pia hujenga chuki kati ya polisi na wananchi
 
Lowassa angekuwa kipindi cha nyerere angekuwa ndani saa hizi, kuna statement kwa level ya lowasa hakutakiwa kuongea yale

wanaokufa ni ccm tu??

lowassa hana sapoti yeyote, unless unasema hao wauaji ndio wako nyuma ya lowassa??!!!

nyuma ya lowassa?? unamtisha nani??
Ana watu million sita nyuma yake?au ushajitoa ufahamu?
 
Back
Top Bottom