Namuonea huruma huyu dada, nilitaka urafiki wa kawaida na si mapenzi

50thebe

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
3,099
2,000
Nawasalimu kwa jina la JF, shuhuda ziendelee.

Wakuu imepita takribani miezi kadhaa hivi tangu ni fahamiane na huyu dada, nikiri kwa hii hali iliyofikia mie ndiye wa kulaumiwa.

Ilikuwa majira ya jioni nimetoka pindi nikechoka nikaona sio mbaya nitafute mtu stranger nipige naye story nimzingue tu. Nikaingia kwenye group la intake yetu mwaka huo, nikawa nachungulia dp za watoto wazuri then nawapa hi , wakirespond tunaendeleza kuchat.

Katika wadada watatu, wawili wakawa hawana response nzuri nikapotezea ,mmojawapo huyu ambaye ndio mwenye hii story akanasa kama mawimbi ga TBC huko mpakani mwa Kenya na Tz.

Dp yake alikuwa ni ustadhat mzuri sana kavalia ushungi rangi ya chocolate na dimpoz kwa umbali. Wakati tunaendelea kufahamiana akaniambia kuwa ni mgonjwa na kweli alikuwa anaumwa, KUMBUKA sijaonana nae face to face IDIBIA, nikamuahidi nitaenda kumpa salamu na kumjulia vizuri hali.

Imefika jioni nikamuahidi naenda kumuona nkitoka kwenye private study, mishale ya saa 4 usiku ,mzee mzito Sina hela Nina mia 7 tu mfukoni, sijala tangu mchana ,boom hakuna pesa zimekuwa hadimu sana mikononi mwangu, nkacheki wallet yangu lakini haioneshi ushirikiano kabisa, kung'uta wapi zinatoka receipts za bank wakati na withdrawal pesa etc

Nkapiga simu, hello vp unatumia juic mtoto akajibu ndio, chap nkashuka PECAM, nafika pale kwa ile mida juic fresh take away zilikuwa zimeisha ,kumbka ilikuwa ni mishale ya saa4 usiku. Nkachukua embe ndogo nikawa narud zangu.

Nimefika umbali kidogo nika mu alert atoke nje tuonane siwez ingia hostel za kike, basi sijafika hatua kadhaa nakuta simu inaita sikutaka kupokea nikaweka silence then mfukoni ili niweze kumuona alienipigia.

Wakati naenda kwenye ngazi zilizopo nje ya hostel nikapishana na mdada ameshika simu lakini yeye hakuvaa the way nimemuona kwa dp nikampotezea sikumpa salamu then nikakaa kitako nikisubiri huyu stranger atokee.

Akapiga tena simu nikapokea lakini sikuongea nikajuwa kuwa NI YEYE kama Lissu anavosema. Basi bwana ile amenikaribia nikajagundua nimeingia cha kike WAAH chakike WAAH, kiufupi hakuwa yule niliomuona kwa dp.

Binti akaja, nikampa hi fresh fresh, nikamjulia hali anaendeleaje akanambia vizuri yukopoa kiasi. Nikamuabia sorry we ni Mwajuma (hili sio jina halisi ila lilikuja tu kichwani mda huo), nikajibiwa hapana nkajibu ohoo basi kuna mdada nlikuwa naye jeshini alikuwa anaitwa Mwajuma kafanana na yule wa kwenye dp yako, akajibu ile dp ye kaichukua tu mtandaoni naye yule mtu hamjui Daaah nkaona hii soo.

Nkampa juis yake nikampeleka ruum,tukaagana fresh. Nlitoka pale mnyonge nimepoteza hela ya miogo alafu mtu mwenyewe sio. NLIISHIWA nguvu kwa kweli nkawaza kupitisha masaa mengine kama 10 bila kula na kesho sina uhakika wa kupata hela ya mlo.

Huyu binti kimuonekano ni mrefu kiasi, mnene pia , ana bumps kiasi ,dimpoz, black beauty kiasi.

Kesho yake asbh nikamjulia hali akanambia anaendelea vzuri, mambo mengine tukaongea then tukapotezeana.
Nikaendelea mjulia hali siku hadi siku na kumpelekea vijizawad vdogo vdogo pipi chocolate nk ,hapa nlikuwa nshapata vijihela kidogo.

BAHARI ILIVYOANZA KUCHAFUKA.
Ikumbukwe lengo la kumtafuta huyu dada ilikuwa ni kuchat nae tu normal, lakini kadiri siku zinavoenda nikazidi kupokea sms za asbh mara umeshindaje.

Kuna siku nlipost picha ya mtoto, aka comment ni wako nikamjibu ndio, akanipa hongera, nkasema vp nawe unataka hapa ndio nlipoharibu. Akanambia mi nawewe ni marafiki hatuwez kuwa na mtoto ,nikamtania ahaa lakini mbona kuwa na urafiki sio kizuiz cha kutopata mtoto akazngua zngua namie nikapotezea kwakuwa yalikuwa ni masihara tu.

Basi kuna siku akanikumbushia hii issue nikamtell mie nina mke na mtoto (sina mke ila ni fukuza nzi tu) akasema sawa, akanambia lakini mi nawewe ni marafiki tuu, nikamjibu najua pia so usiwaze hatuwezi kuwa wapenzi kwakuwa siwez kuwa na mahusiano wakati ninamke tayari sipendi kucheat Kwa mama watoto.

Siku si nyingi mdada akanambia ananipenda, nikamjibu tu short nakupenda pia lakini jua Nina mke. Akajibu sawa, since then huyu dada amekuwa ananisumbua sana.
1Anapenda kugandana na mie sipendi kugandana kabisa ndomana sijihusishi na mapenzi shuleni mara nyingi.
2. Hana boom ,so akijua tu boom limeingizwa basi hapo nimekumiss nyingi sana Yan mara utumiwe picha mara nini sijui nywele zimefanyaje, hapa hadi mda huu nshatumiwa picha nne mida tofauti.
3.Anapenda sana vizawadi, sijui ni kwasabab nlimzoesha kumpa kipindi anaumwa basi asisikie uko mjini atataka zawadi, hajui kuna muda Sina hela na ukimgomea utasikia hunipendi nk

NACHOHITAJI.
Nataka nijiweke mbali nae coz nahitaji kukomaa na mambo yangu yalionileta hapa shule ukizingatia sikuwa na nia ya kudate nae wala KUMLA. Mbinu gani nitumie kumkwepa bila kumuumiza asijihisi vibaya.

USINIULIZE KUHUSU UMRI WANGU
Mkuu kweli kabisa story hii bila picha? 😷
 

ipulunganya

Member
Apr 18, 2021
76
125
Hao watoto wabaya ndio wazuri anakuwa wako peke yako,umepata pa kupumzikia unazingua wewe ni wa kiume au mwanaume
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom