happyxxx
JF-Expert Member
- Nov 14, 2020
- 568
- 1,847
Tangu amerudi amekuwa akitoa kejeli dhiaka na matusi kwa vijana na kina mama maskini wa kitanzania. Hata kama yeye ana pesa nyingi na amepata nafasi ya kuishi Canada kwa mgongo wa ukimbizi wa kisiasa kwa siasa alizopewa nguvu na hawa anaotukana leo basi enough is enough. Tumemchoka!
Kuna watu watakwambia Lema anasema ukweli. Sawa ni kweli bodaboda ni kazi ya kimaskini na ni hatari. Sawa mama zetu wanacheza vicoba kwa sababu ni maskini wamekimbia huduma za kibenki ambazo sio friendly kwao. So akishatusimanga hivyo what next? Watu wakiacha bodaboda waende wapi? Anasema mtoto wa Majaliwa hawezi kuwa bodaboda yeye mtoto wake ni lini alishiriki maandamano?